Mwanaharakati Zara Kay akabiliwa na mashtaka ya kuwa na uraia pacha nchini Tanzania. Hati yake ya kusafiria yachukuliwa na Vyombo vya Usalama

Kwanza kuwa na Uraia Pacha ni kosa kisheria. Na ikiwa ameingia Tanxania na passport ya Tanzania wakati yeye ni raia wa Australia hapo amejiweka mtegoni.

Pili bibie huyu ni mwana harakati dhidi ya Uislaam kupinga mila na Desturi za Wanawake kuvaa Hijab akisema wanalazimishwa na Wanaume. Na isitoshe ameukana Uislaam kwa sababu ya vazi tu! Ikisha Jambo hili sii kweli kwani hata Wanawake kuvaa ama kusuka nywele bandia hawajalazimishwa na Wanaume.
 
She is a a Christian convert former/ex Muslim. Alimkana mudi na kumkubali Yesu. Yesu atampigania tu
Umerudishiwa kichwa chako? Unaambiwa ni atheist, wewe unasema ni mkristu! tatizo la kushinda JF na elimu isiyoongezeka.
 
Hapo kosa ni kumkosoa Meko, hayo mengine ni ya kuokoteza tu,Hata Bongozozo akiukosoa huu utawala atatafutiwa kosa tu,tatizo anapenda kusifiwa kupitiliza
 
Umeongea vizuri ila baadhi humu wapotoshaji tu.

Mwaache aende segedansi akachezee JANDO kwanza ili akili imuingie
 
Wanaharakati wa kupost twitter,

Siku zinakwenda mbio sana,

Sasa kama kupost twitter nako nikuwa mwanaharakati kina Che guevara na Fidel sijui tuwaite kina nani??
Waite wanamapinduzi au revolutionalists, wameitwa hivyo siku zote hawajawahi kuitwa activists/wanaharakati
 
Wahenga walisema ukiishi ktk nyumba ya vioo usiwarushie wenzako mawe. Sasa mtu una passport za kughushi unaanza kuchokonoa wengine, utapata kesi tu
 
Tanzania ni nchi ya kisekula / secular haina dini na raia wake wapo huru kuchagua au kubadili imani wakati wowote

huyu hajachagua wala hajabadili imani, bali amesema habari ya Uislam na Mungu kwa ujumla "ni bullshit..."

Ambalo ni kosa la jinai. Pia ana passport mbili na anatumia sim card ya mtu mwingine.

Nawashangaa sana wanaoutema uraia lakini bado Tanzania inawawasha. Waende Australia wakahubiri kujikinga na COVID -19
 
Serikali inavyoanza kutumia uraia au sheria za uraia kudhibiti watu au kunyamazisha watu, hicho siyo kitu cha kikuunga mkono hata kama unaona huyu mwanaharakati anafanya makosa kwenye harakati zake. Ni kutokuona mbali. Leo huyu, kesho sheria inapitishwa au raisi anatoa tamko kufuta uraia wa wapinzani wa siasa ambao wanaonekana wanahatarisha usalama wa nchi au ni wasaliti. Haya mambo yameshafanyika hapa duniani kwa mfano nchi ya Bahrain. Na kama huamini hili linaweza kufanyika hapa unajidanganya tuu.
 
Sidhani anatumia pasipoti mbili. Alisema hakurudisha pasipoti ya Tanzania kwa sababu ilipotea pala Australia ambako alikuwa raia. Ile nukuu ya "mawi ya fahali" umepata wapi? Una ushahidi?
Kutumia simcard ya mtu mwingine - hiyo kweli jinai kali!!!!
 
Sidhani anatumia pasipoti mbili. Alisema hakurudisha pasipoti ya Tanzania kwa sababu ilipotea pala Australia ambako alikuwa raia. Ile nukuu ya "mawi ya fahali" umepata wapi? Una ushahidi?
Ushahidi wa hiyo kauli yake ya "mawi ya fahali" ipo humu, kwenye hiyo clip anayohojiwa na Mhindi. Nime assume una maanisha aliposema Uislamu na imani ya Mungu kwa ujumla ni mavi ya fahari.

Passport mbili kupotea, thibitisha, lete police report!

Passport yako au leseni au cheti au sim card au bunduki au gari lako likitumiwa na ma terrorist au jambazi wakaenda kuua huwezi kujitetea oooh ilipotea... mbona hukusema? Rebuttable presumption ni kwamba unajua ilipo!
 
She is a a Christian convert former/ex Muslim. Alimkana mudi na kumkubali Yesu. Yesu atampigania tu
si kweli. Sio christian. Ni kafiri...yaani haamini mungu. Anakana uwepo wa mungu. na ana-support 'u-gay' na anakashifu dini ya uislam ili apate umaarufu zaidi huko aliko. Na anaongoza organization ya kusaport wanaotoka kwenye dini na kuikashifu. Ni afiriti mkubwa! Kwa maoni yangu hakuna adhabu inayomtosha Taznania. Wamuache aende zake akaendelee kulaanika mbele ya safari asituharibie vizazi vyetu huku! Ni adhabu ya Allah tu ndio itakayomtosha huyu!
 
Passport mbili kupotea, thibitisha, lete police report
Huyu ni raia wa Australia. Hakuna sharti ya kutoa taarifa kwa polisi ukipoteza pasipoti ya nchi uliyoacha.
Sijaona dalili kwamba aliingia TZ kama raia wa TZ. Alifika kama raia wa Australia aliyeomba visa.
Nisipokosei hakuna sheria inayodai unahitaji kuomba kibali ukitaka kuacha uraia wa TZ. Ninavyojua mara umepata uraia wa nchi nyingine uraia wa TZ unakwisha.
Kama angetumia pasport ya TZ baada ya kuwa mwaustralia angedanganya. Sijaona habari hiyo.
 
Yan comment nyingi humu zinaonesha chuki ya raia dhidi ya serikali, sababu swala lipo wazi kuwa Tanzania hatuna uraia pacha lkn cha ajabu kila mmoja humu anaishambulia serikali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…