Mwanaidi Sinare Maajar - Balozi Mpya Marekani

Mwanaidi Sinare Maajar - Balozi Mpya Marekani

- Huyu mama amekuwa akitaka kurudi nyumbani kulifufua shirika lake la sheria kwa muda mrefu sana sasa, nijuavyo ni kwamba yuko matayarishoni kurudi nyumbani bongo kwenye shirika lake la sheria na wala sio siri among the tops, maana huwa hafichi akiwa na wakulu in private!

- Sefue is doing a great job kule haendi kokote ni dua la kuku tu!

Respect.

FMEs!

-Ni kweli mkuu.Mimi naona Balozi Ombeni Sefue anaifaa sana Marekani.Huyu mkulu namkubali kwa diplomasia
 
Duh.....habari haijathibitishwa mnairusha angalieni msije mkamponza mama wa watu bure akarudi kukalia benchi bongo
 
Kwa wale wanaojua government workings aliyefungua hii thread hata kama ilikuwa ni kwa nia njema basi ajue kalikoroga,Serikali huwa hazipendi mtu kuzi jumpstart.Wadau mnakumbuka yaliyomkuta Balozi Juma Mwapachu enzi za Mzee Mkapa baada ya gazeti la Rai kudokeza uteuzi wake?

yatamkuta kama jina lako!
 
So sick buddy! JT is costing us with his dic k....Nadhani ni strategies za kuboresha mahusiano kwa faida ya Tanzania. Mama Kichwa sana UK ilikuwa haijawahi kuwa na muwakilishi makini mwenye kutetea maslahi ya nchi yake. Ubalozi wetu UK ameubadili sana hata attitude za watendaji pale.
Unatafutwa wewe
 
na we una matatizo yako kati ya watu wote wa kuwasilimia umeshindwa kujizuia kutaja hili jina.. haya akija na miye nitamsalimia.
Usishangae, jamaa sio matatizo yake, bali ni recognition kati ya Watanzania wote mashuhuri walioko US, ukimwondoa Naibu Katibu Mkuu na mabalozi, Mzee Mwanakijiji nawe ummo!,
Angalizo:hapa nazungumzia mashuhuri na sio maarufu!
 
Hivi ile sheria inayowapa kikomo wafanyakazi kwenye balozi zetu wasikae zaidi ya miaka kadhaa huko nje unafuatiliwa kweli au basi ni sheria butu ambayo kila moja ana haki ya kuidharau?
.
Hakuna sheria hiyo bali ni kanuni tuu ambayo bado ipo ila kutokana na ukata, kuwarotate wote baada ya kila miaka 4 kumeshindikanika.
 
Kwa wale walisoma Sheria UDSM wanamjua na pia sijui kwanini JK aliamua kumteua mdogo mtu na sio dada yake?
.
Dada mtu ni kichwa cha ukweli, alipokuwa akifundisha UD, Investment Law, alisema wazi kwenye sheria real money lies in contracts na legal opinion na sio kwenye litigations.

Alijitolea pesa yake mfukoni kuprint madesa ya somo lake na kuyagawa bure, wakati walimu wengine wakitoa desa kwa ma class rep wanayapeleka kwenye vile photocopy na wanafunzi wanalipia.
 
Inafurahisha kusoma dondoo za wenye habari za ndani kuhusu mtu binafsi kiasi cha kusifu tabia na utendaji wake. Kwa siye tunaotegemea taarifa rasmi tu inatupa shida kidogo. Balozi anaposifiwa kwa kuleta mabadiliko makubwa kituoni kwake tunajiuliza kama kuna taarifa ya kuboreka (improve) kwa vitu kama mawasiliano ya ki-biashara, utalii, manufaa ya kimkakati, huduma bora kwa wa-Tanzania na wengineo, n.k.

Mimi binafsi nimekuwa napiga chenga sana kupitia balozi zetu ninapokuwa safarini hata kwa kusalimia tu kutokana na negative attitude nazokutana nazo mara nyingi. Kuna wakati karibu nishindwe kuwasilisha mzigo wa mwana-ubalozi mmoja niliotumwa na nduguye baada ya kila mmoja kuogopa kunisikiliza kwenye simu tu nikiwa hotelini (niliposalimia kwa kiswahili tu) hadi walipopata taarifa kutokea kwa mtumaji.

Natumaini Mrs. Maajar kaleta change we can believe in (kwa wanaomsifia) na, hivyo, ndugu zetu wa US wakae mkao wa kufaidi. Lakini, huyu si mmoja wa wale waliokuwa wakihusishwa na kampuni ya wanasheria iliyofanikisha mikataba ya Deep Green and the like?
 
.
Dada mtu ni kichwa cha ukweli, alipokuwa akifundisha UD, Investment Law, alisema wazi kwenye sheria real money lies in contracts na legal opinion na sio kwenye litigations.

Alijitolea pesa yake mfukoni kuprint madesa ya somo lake na kuyagawa bure, wakati walimu wengine wakitoa desa kwa ma class rep wanayapeleka kwenye vile photocopy na wanafunzi wanalipia.


Kuna integrity yoyote kwa watu wanaosoma law UDSM?

Mizengwe yoyote inawakilishwa na malawyer waliosoma hapo!
 
Haya, moshi umefuka wee, sasa tumeona moto.

Mama Maajar huyoo kaenda US, ila watu wa US wameonya asiende kufungua matawi ya nanihii.
Mimi binafsi niko UK lakini hayo matawi ya nanihii wala sijishughulishi nayo. Nawaachia wenyewe.
Ila kweli, balozi zisigeuzwe recruitment centres! Sijui Mama Maajar alikuwa anafanya kwa nia au kwa shurba?

Hongera tena Mama Maajar!
 
Kuna reshuffle ya mabalozi. Balozi Mwanaidi Maajar kuhamishiwa Washington, Kuchukua nafasi ya Balozi Sefue.

More to come


sasa ndiyo tunaendelea kuona wazi wazi udini wa kikwete..yaani jamani embu pitieni vya kutosha teuzi zake zoote mtajionea jinsi atoavyo shavu kwa wana vibandiko..
 
Hongera sana mama Majaar, wengi tutakumiss sana kwa hapa UK.

Kazi yako hapa UK imeonekana na tunakuombea uendelee na moyo huo huo wa uchapaji kazi na kujituma hata kama walio juu watajaribu kukwamisha juhudi zako.

Mafanikio mema.
 
Kwa hiyo kazi yake kubwa ilikuwa ni kusimamia Chama ama Serikali?.Je Uk alikuwa anawawakilisha wana CCM au Watanzania wote bila kujali chama?.Je hakuna wanaupinzani Uk waliohitaji huduma yake?.Basi kama alikuwa akisimamia chama basi hafai kuwa Balozi.

Nawakilisha

Mkuu kazi ya balozi ni kufuata anachotumwa na aliyemteua. Kwa hiyo kama huyu mama kafanya chochote unacho kiona siyo basi inabidi ujiulize kwanza ni kwa maagizo ya nani. Don't blame her for doing her job. Ubalozi kidogo ni kama jeshini...you follow commands bila kuuliza uliza maswali mengi....ukishindwa una jitoa.
 
Hili la matawi ya CCM nafikiri huyu mama kaponzwa na mume wake ambaye alitumia nafasi hiyo kupata kitu cha kufanya hapa UK. Huenda makosa ya balozi yalikuwa kutokuliona hilo na hivyo kumkataza bwanake.

Binafsi ninapinga ufunguaji wa matawi ya CCM nje ya nchi na nimeweka msimamo wangu wazi na wala sijihusishi na hayo matawi.

Huku nje ni bora wote tukijulikana kama Watanzania na kusisitiza zaidi juu ya Utanzania wetu kuliko hayo mambo ya vyama.

Pamoja na hilo tatizo bado naona mama Majaar kajitahidi kurudisha heshima ya ubalozi kwa watanzania wote tuishio UK. Anasikiliza matatizo ya wananchi na kujaribu kusaidia pale anapoweza. Anasikiliza ushauri juu ya namna nzuri ya kuboresha utendaji wa ubalozi na nchi kwa ujumla. Ni mtu wa mabadiliko na alijaribu kufanya mabadiliko katika vitu mbalimbali kwa faida ya nchi hata kama baadhi ya hayo mambo wakubwa walikwamisha. Amejaribu kuandaa utaratibu ambao ungeufanya ubalozi wetu ujitegemee kwa kutumia mapato kutoka kwenye apartments ambazo zingejengwa kwenye viwanja vinavyomilikiwa na ubalozi ambavyo sasa vinakaribia kunyang'anywa lakini nafikiri wenye nchi waligonga nyundo.

Kwasasa nchi inatumia mamilioni ya pounds kukodisha maeneno ya kukaa watu mbalimbali wanaokuja kwa muda mrefu. Lengo lilikuwa wakae kwenye hizo apartments kwa bei nafuu na wakati huo huo ubalozi ukitengeneza pesa.
 
In two years time, Shirikisho la Afrika Mashariki litakapoanza, Jamhuri ya Afrika Mashariki itakuwa inawakilishwa na balozi mmoja. Hii itasaidia kutupatia wawakilishi mabalozi kila mahali, na pia itapunguza gharama!

Bring it on EAC!
Ml,
Hiyo beti ya wimbo imekubalika, kwangu angalau.
 
Mwanakijiji na wadau wengine natumaini mmeshamwandalia mama mapokezi. Natumaini hayatakuwa ya 'kichama chama'
 
na we una matatizo yako kati ya watu wote wa kuwasilimia umeshindwa kujizuia kutaja hili jina.. haya akija na miye nitamsalimia.

MM, angalia ...maana wengi wanjua wewe ni mr invisible sasa utamsalimu na kujitambulishaje?
 
The biggest PROBLEM I have na huyu mama especially alipokuwa UK..ni hii kuendekeza U-CCM sana. Everything was about CCM. Thats why unaona kabisa watu wengi...(like minded..??) wanalose interests na hizi balozi. Maana wengine..we are simply tired of politics za nchi yetu through CCM. Wanataka kuona tunayatafuta maendeleo kwa udi na uvumba. Sasa hata kiongozi wa serikali akija..utakuta watu wamevaa sare za CCM! ..Damn!!

Kuna aliyesema kwamba mume wa balozi ndo alimponza mama kwa kudhania kwamba anawakilisha CCM baadala ya serikali yetu. Perhaps Membe aangalia namna ya kuwa-keep busy ma-spouse wa mabalozi! Itasaidia hawa jamaa kuwa na shughuli productive ....

Angalizo: Sipingi wanachama wa CCM kuwa na shughuli zao za kichama. Tatizo langu linakuja pale ambapo watendaji wa serikali wanajikuta wakiwa busy na shughuli za chama.

Otherwise, mama Maajar namtakia kila lakheri katika kituo chake kipya cha kazi.
 
Back
Top Bottom