Benjamini Netanyahu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2014
- 95,871
- 116,627
Nyie simpo kwenye SUK mnalalamika nini? ongeeni kwenye vikao vyenu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Namshangaa aliyebariki upumbavu ule.Yawezekanaje Mtu umestaafu, halafu upewe asilimia 33 na wao serikali wabaki 67.
1:Nikianzisha mradi wa milioni 20 tu na nyingine nilipe madeni sibakiwi nakitu
2:Nikifa baada ya miaka 2 familia inaendelea kuwa na mateso kama vile Marehemu hakuwa Mtumishi
Huu ni udhalilishaji na uonevu
1. Uhalisia wa fomula ya zamani kwa pssf ukoje, maama mtu anachangia 30m anapewa mkupuo 45m na monthly pension.TUCTA Inawauza Wafanyakazi: Kikokotoo Kipya cha Mafao Kitawaumiza Wastaafu.
Utangulizi:
Hivi karibuni, yametokea maamuzi makubwa kuhusu hatima ya wafanyakazi nchini, tangu Mei Mosi, kuanzia ongezeko la kima cha chini cha mshahara, ukomo wa umri wa wategemezi wa Bima ya Taifa ya Afya na kikokotoo cha mafao ya ustaafu, hatima ya fao la kujitoa. Shangwe za kupandishwa kwa mshahara, zimezima uhalisia wa maumivu ya kanuni za kikokotoo cha mafao ya uzeeni (kikokotoo cha mafao ambacho kinapunguza mafao yanayolipwa kwa mtumishi aliyestaafu)
Ukimya wa TUCTA na vyama vingine vya wafanyakazi juu ya maslahi ya wafanyakazi na wastaafu, umetustusha sana. Kama chama tumeona hali hii inaweza kuathiri mustakabali wa wafanyakazi na wastaafu nchini. Kukalia kimya kutetereshwa kwa mifumo ya hifadhi ya jamii ni sawa na jaribio la kuteteresha Maisha ya askari wanaojitoa kwa ajili ya kuliendeleza taifa, matokeo yake ni kuvunja ari, hamasa na ufanisi wa kazi kwa wafanyakazi waliopo.
Kwenye, uchambuzi wa chama cha ACT Wazalendo tutaenda kuzungumzia mambo mawili; mosi, ujio wa kikokotoo na kuanza kwake kutumika rasmi Julai Mosi 2022 na hatima ya fao la kujitoa.
A: Kikokotoo na hatma ya wafanyakazi
Serikali imetangaza (tarehe 26 Mei, 2022) kanuni mpya za mafao katika skimu ya hifadhi ya jamii. Miaka mitatu iliyopita (2018) Serikali ilipitisha Bungeni kanuni za mifumo ya hifadhi ya jamii iliyoambatana na kanuni mpya za kukokotoa mafao ya kustaafu ya wafanyakazi. Kanuni hii (kikokotoo) ilipingwa na wafanyakazi, wanaharakati na wanasiasa kila kona kwa hoja za wazi kabisa; Moja, hatari iliyotangazwa na Serikali ya kufilisika kwa mifuko (kwa kipindi hicho, PSPF na LAPF) ni hoja iliyokosa nguvu, kwa kuwa kufilisika kwa mifuko kulitokana na madeni ya Serikali iliyokopa kwenye mifuko hiyo. Hivyo, makosa ya Serikali na warasimu wa mifuko hiyo hayapaswi kubebeshwa kwenye mabega ya wastaafu kwa kuwapunja mafao yao. Pili, hoja ya kufilisika kwa mifuko ilitiliwa shaka, kwa kuwa inafahamika kuwa mifuko hiyo imewekeza kwenye miradi mingi mikubwa na fedha nyingine zimetumika kufadhili miradi ya Serikali.
Kutokana na hoja na kelele za wafanyakazi na wadau wengine, iliilazimisha Serikali kupitia Rais wa wakati huo (Hayati, John Pombe Magufuli), kusimamisha matumizi ya kanuni hizo na kuahidi kuanza kutumika 2023. Sababu za kusitishwa kwake ni pamoja na kuipa mifuko ya hifadhi ya jamii muda wa kujiimarisha kifedha ili baadaye ziweze kupata nguvu ya kuwahudumia wastaafu. Kutoa muda kwa Serikali kulipa madeni yake inayoidaiwa na mifuko hiyo ambayo ilikuwa zaidi ya trilioni 4.7, lakini Serikali haijalipa madeni yote inayodaiwa. Aidha, kupata mwafaka wa pande zote juu ya kanuni zinazoweza kutumika.
Serikali imerejesha kikokotoa kilekile kimya kimya
Tumestushwa sana na pendekezo la TUCTA la kikokotoo kinacho poromosha mafao na uamuzi wa Serikali kutangazo kanuni mpya zinatumia kikokotoo cha 1/580 badala ya 1540, pia malipo ya mkupuo ya mafao (kiinua mgongo) ya mtumishi aliyestaafu atalipwa kwa asilimia 33 badala ya 50% inayotumika sasa, umri wa kuhudumiwa mstaafu ni miaka 12.5 badala ya miaka 15.5. Kurejeshwa kwa kikokotoo hiki kikiwa na marekebisho madogo tu ya asilimia za mkupuo kutoka 25 iliyopendekezwa na Serikali, bado haiendi kuwasaidia wastaafu badala yake inaenda kuwaumiza.
Mfano, kwa mfanyakazi aliyestaafu akiwa amechangia kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii kwa miaka 30 na ikiwa mshahara wake wa mwisho ulikuwa Tsh. 1,200,000. Mafao ya Mtumishi huyu kwa kutumia kanuni hizi mbili yatakuwa kama yafuatayo;
Kwa kuangalia mchanganuo huo, hapo juu ni wazi kwamba kanuni mpya inaenda kumpunguzia mstaafu mafao yake karibia kila kipengele kinachohusika na mafao. Kwa uchambuzi tulioufanya inaonyesha dhahiri kuwa;
- Kanuni za zamani (Kikokotoo cha 1/540, miaka 15.5 na malipo ya mkupuo 50%);
- Pensheni ya mwaka (Full pension) ilikuwa Sh. 9,600,000.
- Malipo ya mkupuo/Kiinua mgongo (Lumpsum/commuted pension) ilikuwa Shilingi Milioni 74.4 (74,400,000).
- Pensheni ya Mwezi (Posho) ilikuwa Sh. 400, 000.
- Kanuni Mpya _mwaka 2018 (Na marekebisho ya 2022); (Kikokotoo cha 1/580, miaka 12.5 na malipo ya Mkupuo 33%)
- Pensheni ya mwaka (Full Pensheni) itakuwa Sh. 8,937,931.03
- Malipo ya Mkupuo/Kiinua mgongo (Lumpsum pension) itakuwa Sh. Milioni 36.8 (36,868,965)
- Pensheni ya Kila mwezi (posho) itakuwa Sh. 499,034.
Msimamo na Mapendekezo ya ACT Wazalendo kuhusu kikokotoo kipya
- Kikokotoo cha 1/580 kinaenda kupunguza mafao ya mtumishi aliyestaafu ya mwaka kwa asilimia 6.9
- Pia, kinapunguza malipo ya mkupuo (lumpsum) ya kiinua mgongo kwa asilimia 50.5 ukilinganisha na kanuni za awali.
- Vilevile, kinafupisha umri wa kuhudumiwa mstaafu kwa takribani miaka mitatu kutoka miaka 15.5 ya awali hadi 12.5
- Kwa kutumia ukokotozi wa wastani wa miaka mitatu ya mshahara wa juu badala ya kiwango cha mshahara wa mwisho kutashusha mafao ya wastaafu kwa asilimia 7.08
- Mwisho, kutakuwa na ongezeka kwenye posho ya kiinua mgongo ya kila mwezi kwa asilimia 24.7 lakini kwa kukokotolewa jumla ya mafao atakayepokea kwa miaka 12.5 yanaongezeka kwa asilimia 0.6 pekee kutokana na kufupishwa kwa miaka mitatu tofauti na awali.
Sisi, ACT Wazalendo tunaamini kuwa mfumo wa hifadhi ya jamii husaidia kulinda maisha ya watu na kutoa uhakika wa kuishi vizuri unapokutwa na majanga au kupoteza uwezo wa kufanya kazi kwa namna yoyote ile. Hatupaswi kuwaadhibu wazee wetu kwa kukubali kanuni hizi kandamizi zinazoenda kuwapunja mafao yao na kufupisha muda wa kuwahudimia kwa kuwakadiria kifo mapema zaidi. Aidha, hatukubaliani na uamuzi wa Serikali kuwabebesha wastaafu mzigo wa gharama kwa makosa ya utendaji mbovu wa menejimeti za mifuko na madeni ya Serikali.
Kutokana na mtazamo huu, tunaitaka Serikali kufanya mambo yafuatayo ili kuhakikisha wafanyakazi wastaafu wananufaika na michago yao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii;
Tunaitaka Serikali kulipa madeni yote inayodaiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii kwa mkupuo mmoja ili kuiwezesha mifuko kujiendesha na kuhudumia wateja wake kwa wakati.
Ripoti ya CAG 2020/21 imeonyesha kuwa kuna deni la trilioni 1.5 ikiwa ni mikopo isiyolipwa na Serikali na taasisi zake mbalimbali. NSSF inadai Trilioni 1.17 (Mkopo 490.16 bilioni na riba 684.42 bilioni) na PSSSF inadai 323.98 bilioni. Madeni haya yana muda mrefu kati ya mwaka 1 hadi15. Pia, deni la Serikali linalotakana na michago yake ya wastaafu kabla ya mwaka 1999 (shilingi trilioni 2.45). Jumla, ya madeni ya Serikali kwenye mifuko ni trilioni 3.95. Madeni haya yakilipwa itaboresha uwezo wa mifuko kwa zaidi ya asilimia 40.
Tunaitaka Serikali kurejesha kanuni za zamani za mwaka 2017 (Social security Schemes- Pension benefits harmonization rules)
Tunaitaka Serikali kurudi kwenye kanuni za mwaka 2017 ambazo zinatoa mafao ya malipo ya mkupuo kwa 50%, kikokotoo kuwa ni 1/540, umri wa kuishi baada ya kustaafu ni miaka 15.5 na 50% inayobaki ya mafao ya mtumishi iwe pensheni ya kila mwezi. Vilevile, ichukue mshahara wa mwisho wa mstaafu badala kuchukua wastani wa mishahara mitatu ya juu. Kwa kutekeleza hatua ya kwanza tuliyoipendekeza hili litawekezana kwa urahisi zaidi.
Menejimenti za mifuko ya hifadhi ya jamii kufanya uwekezaji wa miradi itakayoleta faida kuendena na mahitaji ya wanachama.
Moja ya changamoto zinazopunguza uwezo wa mifuko ya hifadhi ya jamii (NSSF na PSSSF) kuhudumia wanachama wake ni kufanya uwekezaji usiolingana na faida inayopata. Kiwango cha faida za uwekezaji kwenye majengo na miradi mengine ni kidogo na kimekuwa kikishuka kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita kuanzia mwaka 2017 hadi 2021. Ongezeko la uwekezaji katika majengo ya uwekezaji haulingani na mapato halisi kwani yanaendelea kupungua.
Vyama vya wafanyakazi nchini vishikamane kama ilivyofanya miaka mitatu nyuma kupinga udhalimu huu.
Vyama vya wafanyakazi na wadau wengine tushikamane kupaza sauti ili kuhakikisha wafanyakazi wa nchi hii waone kustaafu ni heshima badala ya adhabu. Pia, wafanyakazi ni wastaafu watarajiwa, wasipopigania haki yao wakiwa na nguvu hawatoweza wakizeeka.
B: Mafao ya kujitoa
Mjadala wa fao la kujitoa ulihitimishwa kwa kupitishwa kwa sheria mpya ya hifadhi ya jamii ya mwaka 2017. Licha ya kelele kutoka kwa wadau mbalimbali, Serikali iliweka pamba masikioni na badala yake ikaanzisha fao la kukosa ajira. Uzoefu wa utekelezaji wa sheria hiyo unaonyesha wazi kuwa fao la kukosa ajira haliwezi kuwa mbadala wa fao la kujitoa. Hivyo basi, tunaishauri Serikali kufanya mapitio ya sheria ili kurejesha fao la kujitoa. Pia, fao la kukosa ajira lipanuliwe kwa kuhusisha watu wote walikosa ajira (ambao wenye sifa na haki ya kuajiriwa lakini kutokana na ukosefu wa ajira nchini wameshindwa kupata ajira) tofauti na ilivyo sasa.
Hitimisho:
Hatua ya Serikali kung’ang’ania kutumia kanuni mpya ya kikokotoo baada ya mjadala wa miaka mitatu na mapendekezo mbalimbali ya kuboresha maslahi ya watumishi wa nchi hii. Ni dhahiri kuwa Serikali imeamua kupuuza sauti za muda mrefu za wafanyakazi na kuonyesha kuwa lengo lake ni kuwaumiza wastaafu. Ujio wa kanuni hizi, kwa kumlipa mstaafu asilimia 33 ya mafao ya mkupuo, kwa miaka 12.5 na kikokotoo cha 1/580 ni kuwakandamiza na kuwanyonya wazee wetu waliotumikia taifa hili kwa jasho na damu tena katika mazingira magumu ya mishahara kiduchu, ambayo inayowafanya kuishi kwenye mzunguko wa madeni kila uchao. Aidha, ni wazi kuwa kanuni hizi zitashusha ari, hamasa na ufanisi wa kazi kwa wafanyakazi wa nchi hii. Ni matumaini yetu kuwa mapendekezo tuliyotoa yanaenda kusaidia mifuko ya hifadhi ya jamii na watumishi kwa ujumla wake, ni muhimu kwa Serikali kuyafanyia kazi kwa nguvu zote kunusuru hali ya wafanyakazi.
Ndg. Mwanaisha Mndeme
Msemaji wa Sekta ya Uwekezaji, Mashirika ya Umma na hifadhi ya Jamii
mmndeme@actwazalendo.or.tz
ACT Wazalendo
30 Mei, 2022.
Kapewa ajira ya miaka 9 sahivi hasikii chochoteSuluhisho ni lipi? Nyinyi mko serikalini mnaunga mkono sera za CCM, usaidizi wenu uko wapi kwa hili? Inawezekana wewe unaona mapungufu ya CCM na kuwpo haja ya marekebisho, lkini Kiongozi wenu mkuu ni ndumila kuwili! naye ni sauti ya mwisho.
Wewe profesa uliyefundushwa na hao darasa la saba siyo? Kuwa na heshima Kwa waliokuwezesha kufika ulipo dogo, otherwise unaisaka laana ilikolala!Shida watumishi wenyewe darasa la saba
Sijawakataa ukiwambia waandamane hawawezi ndomana wanapelekwa tu wastaafu wote wasasa na watarajiwa mikaka 7 ijayo ni upe upe wote ,ukiwambia kitu hofu tupuWewe profesa uliyefundushwa na hao darasa la saba siyo? Kuwa na heshima Kwa waliokuwezesha kufika ulipo dogo, otherwise unaisaka laana ilikolala!
Dogo, Kuna vitu vingi Sana huvielewi katika nchi hii. Viongozi wote namaanisha wote wa vyama vya wafanyakazi ni either maofisa vipenyo na wengine no mainformer wa tiss.Sijawakataa ukiwambia waandamane hawawezi ndomana wanapelekwa tu wastaafu wote wasasa na watarajiwa mikaka 7 ijayo ni upe upe wote ,ukiwambia kitu hofu tupu
Pole yako Sana karatasi lako limelionaDogo, Kuna vitu vingi Sana huvielewi katika nchi hii. Viongozi wote namaanisha wote wa vyama vya wafanyakazi ni either maofisa vipenyo na wengine no mainformer wa tiss.
Hii maana yake ni kuwa wafanyakazi wakiwa na lengo la kuandamana au kugoma viongozi wao wanawasaliti Kwa kufikisha ujumbe kwenye Dola na Dola inajipanga kutisha na au kuwakamata wahusika wachache ili kufifisha mgomo au maandamano.
Huo ndio ukweli kuwa ccm imepandikiza mamluki wake na wanafiki kwenye vyama vya wafanyakazi ili kuwanyamazisha ndio maana unasikia wachache waliopo kwenye kihenge wanahomola TU ma kujijenga ilihali walio wengi ndio wanatarajia kutaabika na kufa mapema.
Mungu pekee aingilie kati kuwafyekelea mbali mabazazi hayo yaliyoshiriki kuileta na kuibariki sheria hiyo mbovu Dunia nzima akianzia na Jenister Mhagama aliyeiasisi ikimpendeza Mungu amuwahishe kabla ya kupata mafao yake na hata akiyapata watoto wake wakayatapanye na kuuza Kila alichokipata kikashindwe kustawi kikafilisike!
Mara sijui Mara mungu aingilie Kati Kama watumishi wenyewe mmekalisha tu huko Nani awapigie kelele nabado hamukawiagi kuazisha magroup yanayounga ccm mkonoDogo, Kuna vitu vingi Sana huvielewi katika nchi hii. Viongozi wote namaanisha wote wa vyama vya wafanyakazi ni either maofisa vipenyo na wengine no mainformer wa tiss.
Hii maana yake ni kuwa wafanyakazi wakiwa na lengo la kuandamana au kugoma viongozi wao wanawasaliti Kwa kufikisha ujumbe kwenye Dola na Dola inajipanga kutisha na au kuwakamata wahusika wachache ili kufifisha mgomo au maandamano.
Huo ndio ukweli kuwa ccm imepandikiza mamluki wake na wanafiki kwenye vyama vya wafanyakazi ili kuwanyamazisha ndio maana unasikia wachache waliopo kwenye kihenge wanahomola TU ma kujijenga ilihali walio wengi ndio wanatarajia kutaabika na kufa mapema.
Mungu pekee aingilie kati kuwafyekelea mbali mabazazi hayo yaliyoshiriki kuileta na kuibariki sheria hiyo mbovu Dunia nzima akianzia na Jenister Mhagama aliyeiasisi ikimpendeza Mungu amuwahishe kabla ya kupata mafao yake na hata akiyapata watoto wake wakayatapanye na kuuza Kila alichokipata kikashindwe kustawi kikafilisike!
Waongeze Umri wa Kustaafu iwe 75 Ili Wengi wafie kazini wasilipe Pensheni.Ukweli ni kuwa, Serikali inatamani Sana watumishi wanapokaribia kustaafu wafe ili irithi hizo fedha, hata ukistaafu wanatamani ufe haraka kwa kukupa fedha kidogo ili kama hukujipanga ndani ya Mwaka mmoja tu parapanda inaimbwa.
Wanaofanya maamuzi haya kwa Sheria hii haiwagusi kabisa.
Waongo wakubwa!! Lengo lenu ni kutaka kujinasua kisiasa kwa kutumia hoja ya kikokotoo. Kwani kikokotoo hiki kimeanza leo kufanya kazi?? Tangu hiyo 2018 kikokotoo hiki hiki kimekuwa kikitumika kulipa mafao ya watumishi wote wa umma waliokuwa wanachama wa PPF na NSSF kabla ya kuanzishwa kwa PSSSF. Je muda wote huo ACT eti "wazalendo" mlikuwa wapi kutetea?TUCTA Inawauza Wafanyakazi: Kikokotoo Kipya cha Mafao Kitawaumiza Wastaafu.
Utangulizi:
Hivi karibuni, yametokea maamuzi makubwa kuhusu hatima ya wafanyakazi nchini, tangu Mei Mosi, kuanzia ongezeko la kima cha chini cha mshahara, ukomo wa umri wa wategemezi wa Bima ya Taifa ya Afya na kikokotoo cha mafao ya ustaafu, hatima ya fao la kujitoa. Shangwe za kupandishwa kwa mshahara, zimezima uhalisia wa maumivu ya kanuni za kikokotoo cha mafao ya uzeeni (kikokotoo cha mafao ambacho kinapunguza mafao yanayolipwa kwa mtumishi aliyestaafu)
Ukimya wa TUCTA na vyama vingine vya wafanyakazi juu ya maslahi ya wafanyakazi na wastaafu, umetustusha sana. Kama chama tumeona hali hii inaweza kuathiri mustakabali wa wafanyakazi na wastaafu nchini. Kukalia kimya kutetereshwa kwa mifumo ya hifadhi ya jamii ni sawa na jaribio la kuteteresha Maisha ya askari wanaojitoa kwa ajili ya kuliendeleza taifa, matokeo yake ni kuvunja ari, hamasa na ufanisi wa kazi kwa wafanyakazi waliopo.
Kwenye, uchambuzi wa chama cha ACT Wazalendo tutaenda kuzungumzia mambo mawili; mosi, ujio wa kikokotoo na kuanza kwake kutumika rasmi Julai Mosi 2022 na hatima ya fao la kujitoa.
A: Kikokotoo na hatma ya wafanyakazi
Serikali imetangaza (tarehe 26 Mei, 2022) kanuni mpya za mafao katika skimu ya hifadhi ya jamii. Miaka mitatu iliyopita (2018) Serikali ilipitisha Bungeni kanuni za mifumo ya hifadhi ya jamii iliyoambatana na kanuni mpya za kukokotoa mafao ya kustaafu ya wafanyakazi. Kanuni hii (kikokotoo) ilipingwa na wafanyakazi, wanaharakati na wanasiasa kila kona kwa hoja za wazi kabisa; Moja, hatari iliyotangazwa na Serikali ya kufilisika kwa mifuko (kwa kipindi hicho, PSPF na LAPF) ni hoja iliyokosa nguvu, kwa kuwa kufilisika kwa mifuko kulitokana na madeni ya Serikali iliyokopa kwenye mifuko hiyo. Hivyo, makosa ya Serikali na warasimu wa mifuko hiyo hayapaswi kubebeshwa kwenye mabega ya wastaafu kwa kuwapunja mafao yao. Pili, hoja ya kufilisika kwa mifuko ilitiliwa shaka, kwa kuwa inafahamika kuwa mifuko hiyo imewekeza kwenye miradi mingi mikubwa na fedha nyingine zimetumika kufadhili miradi ya Serikali.
Kutokana na hoja na kelele za wafanyakazi na wadau wengine, iliilazimisha Serikali kupitia Rais wa wakati huo (Hayati, John Pombe Magufuli), kusimamisha matumizi ya kanuni hizo na kuahidi kuanza kutumika 2023. Sababu za kusitishwa kwake ni pamoja na kuipa mifuko ya hifadhi ya jamii muda wa kujiimarisha kifedha ili baadaye ziweze kupata nguvu ya kuwahudumia wastaafu. Kutoa muda kwa Serikali kulipa madeni yake inayoidaiwa na mifuko hiyo ambayo ilikuwa zaidi ya trilioni 4.7, lakini Serikali haijalipa madeni yote inayodaiwa. Aidha, kupata mwafaka wa pande zote juu ya kanuni zinazoweza kutumika.
Serikali imerejesha kikokotoa kilekile kimya kimya
Tumestushwa sana na pendekezo la TUCTA la kikokotoo kinacho poromosha mafao na uamuzi wa Serikali kutangazo kanuni mpya zinatumia kikokotoo cha 1/580 badala ya 1540, pia malipo ya mkupuo ya mafao (kiinua mgongo) ya mtumishi aliyestaafu atalipwa kwa asilimia 33 badala ya 50% inayotumika sasa, umri wa kuhudumiwa mstaafu ni miaka 12.5 badala ya miaka 15.5. Kurejeshwa kwa kikokotoo hiki kikiwa na marekebisho madogo tu ya asilimia za mkupuo kutoka 25 iliyopendekezwa na Serikali, bado haiendi kuwasaidia wastaafu badala yake inaenda kuwaumiza.
Mfano, kwa mfanyakazi aliyestaafu akiwa amechangia kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii kwa miaka 30 na ikiwa mshahara wake wa mwisho ulikuwa Tsh. 1,200,000. Mafao ya Mtumishi huyu kwa kutumia kanuni hizi mbili yatakuwa kama yafuatayo;
Kwa kuangalia mchanganuo huo, hapo juu ni wazi kwamba kanuni mpya inaenda kumpunguzia mstaafu mafao yake karibia kila kipengele kinachohusika na mafao. Kwa uchambuzi tulioufanya inaonyesha dhahiri kuwa;
- Kanuni za zamani (Kikokotoo cha 1/540, miaka 15.5 na malipo ya mkupuo 50%);
- Pensheni ya mwaka (Full pension) ilikuwa Sh. 9,600,000.
- Malipo ya mkupuo/Kiinua mgongo (Lumpsum/commuted pension) ilikuwa Shilingi Milioni 74.4 (74,400,000).
- Pensheni ya Mwezi (Posho) ilikuwa Sh. 400, 000.
- Kanuni Mpya _mwaka 2018 (Na marekebisho ya 2022); (Kikokotoo cha 1/580, miaka 12.5 na malipo ya Mkupuo 33%)
- Pensheni ya mwaka (Full Pensheni) itakuwa Sh. 8,937,931.03
- Malipo ya Mkupuo/Kiinua mgongo (Lumpsum pension) itakuwa Sh. Milioni 36.8 (36,868,965)
- Pensheni ya Kila mwezi (posho) itakuwa Sh. 499,034.
Msimamo na Mapendekezo ya ACT Wazalendo kuhusu kikokotoo kipya
- Kikokotoo cha 1/580 kinaenda kupunguza mafao ya mtumishi aliyestaafu ya mwaka kwa asilimia 6.9
- Pia, kinapunguza malipo ya mkupuo (lumpsum) ya kiinua mgongo kwa asilimia 50.5 ukilinganisha na kanuni za awali.
- Vilevile, kinafupisha umri wa kuhudumiwa mstaafu kwa takribani miaka mitatu kutoka miaka 15.5 ya awali hadi 12.5
- Kwa kutumia ukokotozi wa wastani wa miaka mitatu ya mshahara wa juu badala ya kiwango cha mshahara wa mwisho kutashusha mafao ya wastaafu kwa asilimia 7.08
- Mwisho, kutakuwa na ongezeka kwenye posho ya kiinua mgongo ya kila mwezi kwa asilimia 24.7 lakini kwa kukokotolewa jumla ya mafao atakayepokea kwa miaka 12.5 yanaongezeka kwa asilimia 0.6 pekee kutokana na kufupishwa kwa miaka mitatu tofauti na awali.
Sisi, ACT Wazalendo tunaamini kuwa mfumo wa hifadhi ya jamii husaidia kulinda maisha ya watu na kutoa uhakika wa kuishi vizuri unapokutwa na majanga au kupoteza uwezo wa kufanya kazi kwa namna yoyote ile. Hatupaswi kuwaadhibu wazee wetu kwa kukubali kanuni hizi kandamizi zinazoenda kuwapunja mafao yao na kufupisha muda wa kuwahudimia kwa kuwakadiria kifo mapema zaidi. Aidha, hatukubaliani na uamuzi wa Serikali kuwabebesha wastaafu mzigo wa gharama kwa makosa ya utendaji mbovu wa menejimeti za mifuko na madeni ya Serikali.
Kutokana na mtazamo huu, tunaitaka Serikali kufanya mambo yafuatayo ili kuhakikisha wafanyakazi wastaafu wananufaika na michago yao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii;
Tunaitaka Serikali kulipa madeni yote inayodaiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii kwa mkupuo mmoja ili kuiwezesha mifuko kujiendesha na kuhudumia wateja wake kwa wakati.
Ripoti ya CAG 2020/21 imeonyesha kuwa kuna deni la trilioni 1.5 ikiwa ni mikopo isiyolipwa na Serikali na taasisi zake mbalimbali. NSSF inadai Trilioni 1.17 (Mkopo 490.16 bilioni na riba 684.42 bilioni) na PSSSF inadai 323.98 bilioni. Madeni haya yana muda mrefu kati ya mwaka 1 hadi15. Pia, deni la Serikali linalotakana na michago yake ya wastaafu kabla ya mwaka 1999 (shilingi trilioni 2.45). Jumla, ya madeni ya Serikali kwenye mifuko ni trilioni 3.95. Madeni haya yakilipwa itaboresha uwezo wa mifuko kwa zaidi ya asilimia 40.
Tunaitaka Serikali kurejesha kanuni za zamani za mwaka 2017 (Social security Schemes- Pension benefits harmonization rules)
Tunaitaka Serikali kurudi kwenye kanuni za mwaka 2017 ambazo zinatoa mafao ya malipo ya mkupuo kwa 50%, kikokotoo kuwa ni 1/540, umri wa kuishi baada ya kustaafu ni miaka 15.5 na 50% inayobaki ya mafao ya mtumishi iwe pensheni ya kila mwezi. Vilevile, ichukue mshahara wa mwisho wa mstaafu badala kuchukua wastani wa mishahara mitatu ya juu. Kwa kutekeleza hatua ya kwanza tuliyoipendekeza hili litawekezana kwa urahisi zaidi.
Menejimenti za mifuko ya hifadhi ya jamii kufanya uwekezaji wa miradi itakayoleta faida kuendena na mahitaji ya wanachama.
Moja ya changamoto zinazopunguza uwezo wa mifuko ya hifadhi ya jamii (NSSF na PSSSF) kuhudumia wanachama wake ni kufanya uwekezaji usiolingana na faida inayopata. Kiwango cha faida za uwekezaji kwenye majengo na miradi mengine ni kidogo na kimekuwa kikishuka kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita kuanzia mwaka 2017 hadi 2021. Ongezeko la uwekezaji katika majengo ya uwekezaji haulingani na mapato halisi kwani yanaendelea kupungua.
Vyama vya wafanyakazi nchini vishikamane kama ilivyofanya miaka mitatu nyuma kupinga udhalimu huu.
Vyama vya wafanyakazi na wadau wengine tushikamane kupaza sauti ili kuhakikisha wafanyakazi wa nchi hii waone kustaafu ni heshima badala ya adhabu. Pia, wafanyakazi ni wastaafu watarajiwa, wasipopigania haki yao wakiwa na nguvu hawatoweza wakizeeka.
B: Mafao ya kujitoa
Mjadala wa fao la kujitoa ulihitimishwa kwa kupitishwa kwa sheria mpya ya hifadhi ya jamii ya mwaka 2017. Licha ya kelele kutoka kwa wadau mbalimbali, Serikali iliweka pamba masikioni na badala yake ikaanzisha fao la kukosa ajira. Uzoefu wa utekelezaji wa sheria hiyo unaonyesha wazi kuwa fao la kukosa ajira haliwezi kuwa mbadala wa fao la kujitoa. Hivyo basi, tunaishauri Serikali kufanya mapitio ya sheria ili kurejesha fao la kujitoa. Pia, fao la kukosa ajira lipanuliwe kwa kuhusisha watu wote walikosa ajira (ambao wenye sifa na haki ya kuajiriwa lakini kutokana na ukosefu wa ajira nchini wameshindwa kupata ajira) tofauti na ilivyo sasa.
Hitimisho:
Hatua ya Serikali kung’ang’ania kutumia kanuni mpya ya kikokotoo baada ya mjadala wa miaka mitatu na mapendekezo mbalimbali ya kuboresha maslahi ya watumishi wa nchi hii. Ni dhahiri kuwa Serikali imeamua kupuuza sauti za muda mrefu za wafanyakazi na kuonyesha kuwa lengo lake ni kuwaumiza wastaafu. Ujio wa kanuni hizi, kwa kumlipa mstaafu asilimia 33 ya mafao ya mkupuo, kwa miaka 12.5 na kikokotoo cha 1/580 ni kuwakandamiza na kuwanyonya wazee wetu waliotumikia taifa hili kwa jasho na damu tena katika mazingira magumu ya mishahara kiduchu, ambayo inayowafanya kuishi kwenye mzunguko wa madeni kila uchao. Aidha, ni wazi kuwa kanuni hizi zitashusha ari, hamasa na ufanisi wa kazi kwa wafanyakazi wa nchi hii. Ni matumaini yetu kuwa mapendekezo tuliyotoa yanaenda kusaidia mifuko ya hifadhi ya jamii na watumishi kwa ujumla wake, ni muhimu kwa Serikali kuyafanyia kazi kwa nguvu zote kunusuru hali ya wafanyakazi.
Ndg. Mwanaisha Mndeme
Msemaji wa Sekta ya Uwekezaji, Mashirika ya Umma na hifadhi ya Jamii
mmndeme@actwazalendo.or.tz
ACT Wazalendo
30 Mei, 2022.
Hii kanuni ndio inatumika siku zote huko NSSF mbona zito alikuwa m-zito sana kuizungumzia toka enzi za swaiba wake DAU!!1. Uhalisia wa fomula ya zamani kwa pssf ukoje, maama mtu anachangia 30m anapewa mkupuo 45m na monthly pension.
2.Hii mifuko haiendeshwi kisiasa.
Kiongozi wenu ZZK alikuwa mwenyekiti wa PAC miaka kumi na mwenyewe ni mfaidi wa ufisadi wakati wa Dau, wajumbe wa board akiwa mwenyekiti kaboyonga, mjumbe assad(ambae alinunua nyumba za nssf Tanga Kifisadi) na zzk kampuni ya lake tagete(nikikosea nisamehe) alichota pesa na pia akashiki ufisadi mkubwa wa stand ya kigoma kununua eneo ambalo hadi leo liko tu, mbona yeye alikuwa anaona yanayoendelea na hakufungua mdomo kuelezea hali ya mifuko.
Hilo nalo ni neno japo ni neno mufilisi!! Vijana wataandamana!! La muhimu hata viongozi wa kisiasa wastaafu na miaka 62!! Kwenye siasa wamejaa wazee, hii si sawa!! Hata kiti cha juu kabisa kinakaliwa na mtu ambaye alipaswa kuwa ameshastaafu miaka miwilim ilityopita!!Waongeze Umri wa Kustaafu iwe 75 Ili Wengi wafie kazini wasilipe Pensheni.
Waongo wakubwa!! Lengo lenu ni kutaka kujinasua kisiasa kwa kutumia hoja ya kikokotoo. Kwani kikokotoo hiki kimeanza leo kufanya kazi?? Tangu hiyo 2018 kikokotoo hiki hiki kimekuwa kikitumika kulipa mafao ya watumishi wote wa umma waliokuwa wanachama wa PPF na NSSF kabla ya kuanzishwa kwa PSSSF. Je muda wote huo ACT eti "wazalendo" mlikuwa wapi kutetea?Kama umetumea kaa kimya Kwenye Maumivu ya Wazee