Mwanamfalme wa Uingereza Harry kufunga ndoa na muigizaji wa Marekani Meghan Markle

Nyota wa filamu, wanamuziki pamoja na watu wengine wenye ushawishi dunia ni baadhi ya mamia ya wahudhuriaji wa harusi ya mwanamfalme Harry na mwigizaji wa Kimarekani Meghan Markle inayofanyika leo mchana.

Nyota hao wamekuwa wakiwasili katika kanisa na Mtakatifu George huku wengine wakiwa wameambatana na wenza wao.

Mchezaji soka wa zamani David Bekham akiwa amefuatana na mkewe Victoria wamewasili kwenye sherehe hiyo.

Wengine ni mwendeshaji wa vipindi vya televisheni nchini Marekani, Oprah Winfrey na mwanamuziki wa Uingereza, Elton John.

Wengine wanaohudhuria ni mwigizaji wa Kimarekani, Idris Elba, mwanamuziki James Blunt. Mchezaji tenisi Serena Williams aliandika katika mtandao wake wa Instagram kuwa anajiandaa kuhudhuria harusi hiyo.

Picha za televisheni zimemwonyesha pia, mpenzi wa zamani wa Harry, Chelsy Davy akiwasili eneo la tukio. Wawili hao walikuwa na uhusiano uliodumu wa miaka saba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…