Mwanamke akikujibu SMS yako hivi acha haraka sana kuchat nae

Mwanamke akikujibu SMS yako hivi acha haraka sana kuchat nae

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,401
Reaction score
1,610
Ukiona umemtumia mpenzi wako/mchumba wako/mchepuko wako/mke wako au hata rafiki wa kike wakati mwingine SMS ya kawaida tu kwaajili ya kumsalimia lakini yeye akakujibu moja kati ya majibu yafuatayo, tafadhali sana usiendelee kuchat nae maana kinachofuata hapo ni majanga tu.

KWA MFANO:
1. Ukimtumia sms ''Mambo mpenzi wangu?'' akikujibu ''mambo mabaya'', usimuulize kwanini mambo mabaya, ukimuuliza atakwambia kuwa ''sina hela dear''

2. Ukimtumia sms ''Maisha yanasemaje kipenzi changu'' akikujibu ''maisha magumu hubby wangu we acha tu'' usimuulize kwanini, ukimuuliza kwanini atakwambia ''nimefulia mwenzio kama nini sijui''

3. Ukimtumia sms ''Mbona kimya sana mchumba wangu, umenitupa kiasi hicho'' akikujibu ''sijakutupa wangu yaani mambo hata hayaendi'' usimuulize kwanini mambo hayaendi, ukimuuliza atakwambia kuwa ''yaani sina kitu mpenzi wangu, simu ilikuwa haina hata hela ya kubeep''

4. Au ukiona mwanamke anaanza kwa kukwambia nikwambie kitu? We mkatalie kiutani utani tu, mwambie usiniambie, hata akikomaa vipi akwambie mwambie sitaki uniambie huku unafanya kama utani lakini moyoni unakuwa upo serious.

Ni mara chache sana mwanamke akikwambia kuwa mambo mabaya, maisha magumu au mambo hayaendi huwa na matatizo mengine kama kuumwa, misiba.... n.k lakini THE REST ni wapigaji mizinga tu. Akikwambia maisha magumu mjibu ''pole wangu, mambo mengine vipi?''

Ukipewa majibu kama hayo, chagua moja, either usiendelee kuchat nae mpaka badae kidogo au mbadilishie maada ili kukwepa huo mzinga ambao unakuja mbele yako.

 
sasa kama huna msaada unauliza ya nini?" si ufunge kinywa chako....... unajichetua na maswali ya mtego nikwambie mazuri wakati kiuhalisia ni mabaya hapana kwa kweli......''Maisha yanasemaje kipenzi changu'' nitakujibu maisha yanataka hela na sina hela embu nitumie laki 5 hapo mar moja......
 
hao uwasemao wewe wanajifunza kupiga mizinga, wataalam halisi hawapigi mizinga kwenye msg au sim. Mzinga unapigwa live bila kupepesa macho .... utatoa tu penda usipende!

Heh..mwambiee,.jicho linalegea ukiomba face to face na inatolewa bila ubishi
 
Unajibu tu akiomba hela huru kukataa au kukubali. Kwani atakuja kuzitoa mfukoni mwako si mpaka umpe? Yawezekana ana ishu nyngne ya muhimu zaidi ya kupiga mznga.
 
hao uwasemao wewe wanajifunza kupiga mizinga, wataalam halisi hawapigi mizinga kwenye msg au sim. Mzinga unapigwa live bila kupepesa macho .... utatoa tu penda usipende!

hapa nadhan ni kwa wale ambao kupiga mizinga ndo profession zao.
 
Back
Top Bottom