Mwanamke akipendeza anamfurahisha nani?

Mwanamke akipendeza anamfurahisha nani?

Kuna jamaa yangu mmoja anafanya kazi shirika moja la kimataifa, siku moja kapata safari ya kikazi na akamuomba mkewe amuandalie nguo kwani safari ilikuwa ya ghafla na jamaa hakuwa na muda wa kupaki. Cha ajabu alipokuja kuchungulia kwenye begi akakuta shemeji kapaki pamba mbaya mbaya ambazo zilishapitwa na wakati. Ilibidi mshikaji aingie kabatini mwenyewe kimya kimya. Tulibaki tukijiuliza na jamaa yangu nini lilikuwa lengo la shemeji. Mimi nikawa namtania labda shemeji hataki upendeze huko uendako asije kuibiwa. Jamaa alibaki kucheka ingawa alinisupport na kuongeza wanawake wana wivu sana.
 
Sizani kama Mwanamke anapendeza akikaa Uchi.
Mwanaume alikuwa na haki ya kumwangalia Mkewe na Nguo anazovaa ili asije akawa kituko kwenye shughuli za watu.
Nguo fupi huwa ni za Machangu, Sasa yeye alikuwa ana ng,ang,ania nini?
Inawezekana huko walikokutana kabla ya kuoana walikutana huko Ohio.
Kama ni hivyo inabidi amkubalie.
Kubendeza kwa Mwanamke pia si kwa faida ya Mtu ila ni kujiweka nadhifu iliuonekane miongoni mwa mwatu wastarabu waliopo kwenye shughuli.
Na sivinginevyo.
Na mavazi yawe ya heshima sio kila ukipita watu wanakushangaa na kukucheka kwa kuvaa kipedo.
 
...Kuna wanaovaa wapendeze, na kuna wanaovaa ili kutoa ujumbe fulani...

Ukikubali mkeo atoke katinga kivazi cha ushawishi ilhali wewe ndio "kioo" chake, ...jiandae na adha za "wateja" wataovutika na hizo "adverts"
 
Binafsi navaa nijipendezeshe, siyo kuwa kuvaa nguo fupi ndo kupendeza laa!..kuvaa nguo inayoendana na umbo langu na niwe huru nayo!..
Raha sana kupendeza na kujijua leo kuna vazi nimevaa na nimelipuka!..
 
.........Upande wa mavazi huwa sipendi mtu aniingilie, navaa mimi nipendavyo.
 
Binafsi navaa nijipendezeshe, siyo kuwa kuvaa nguo vupi ndo kupendeza laa!..kuvaa nguo inayoendana na umbo langu na niwe huru nayo!..
Raha sana kupendeza na kujijua leo kuna vazi nimevaa na nimelipuka!..

.........Upande wa mavazi huwa sipendi mtu aniingilie, navaa mimi nipendavyo.

mtapigwa talaka nyie........... shauri yenu!!!!!!!!!!!!!!!!!!11
 
Utata uko wapi shem? au na wewe hupendi kuingiliwa kwenye upande wa mavazi?

utata uko kwenye tungo yenyewe....unapenda uingiliwe wapi (it sounds ambiguous shem)

mi navaa nnachotaka af far as kitaniweka comfortable, confident na ni decent
nguo niinunue mwenyewe afu tena inifanye mtumwa hapana!!!

hamna anayeniingilia kwenye mavazi.........
 
ha, hujajin tu?????????, mbona unaongea kama una bonge la experience!!!!!!!!!

Kwenye uhusiano niliopo tu experience ni tosha mana full makeke!..Tofauti tu ni kuwa ndoa ni kitanzi zaidi na mnakuwa mmefungwa na kiapo...Yanayojiri mengine yanaendana!!
 
Kwenye uhusiano niliopo tu experience ni tosha mana full makeke!..Tofauti tu ni kuwa ndoa ni kitanzi zaidi na mnakuwa mmefungwa na kiapo...Yanayojiri mengine yanaendana!!

nafikiri kwenye ndoa kuna mengi zaidi. hayo uliyotaja ukiingia kwenye ndoa huongezeka intensity. halafu kuna ishu wanasema wajuaji inaitwa kuzoeana na wengine kuchokana. yaani kama kwenye uhusiano kuna kiu, kwenye ndoa hufikia kiasi cha kukinaiana sasa hapo ndo a number of implications zinaanza ................
 
mtapigwa talaka nyie........... shauri yenu!!!!!!!!!!!!!!!!!!11
.........Hakuna cha kupigwa talaka wala nini,inategemea na jinsi alivyonikuta napendelea kuvaa mavazi ya aina gani.
Kwanza mie sikubalini na dhana kwamba mavazi yanaelezea tabia ya mtu.Kama mtu una tabia chafu ni chafu tu...........hata uvae vazi refu linatambaa hadi chini kama tabia yako mbaya ni mbaya tu.
 
Back
Top Bottom