Ambassador
JF-Expert Member
- Jun 2, 2008
- 933
- 75
- Thread starter
- #41
Kuna jamaa yangu mmoja anafanya kazi shirika moja la kimataifa, siku moja kapata safari ya kikazi na akamuomba mkewe amuandalie nguo kwani safari ilikuwa ya ghafla na jamaa hakuwa na muda wa kupaki. Cha ajabu alipokuja kuchungulia kwenye begi akakuta shemeji kapaki pamba mbaya mbaya ambazo zilishapitwa na wakati. Ilibidi mshikaji aingie kabatini mwenyewe kimya kimya. Tulibaki tukijiuliza na jamaa yangu nini lilikuwa lengo la shemeji. Mimi nikawa namtania labda shemeji hataki upendeze huko uendako asije kuibiwa. Jamaa alibaki kucheka ingawa alinisupport na kuongeza wanawake wana wivu sana.