Back in days chuoni.
Demu fulani alinizimikia sana na me nilimzimikia sana penzi likawa moto sanaa, khaa miezi 7 baadae ananiambia anaona tuachane, namuuliza kwanini ananiambia haoni future kwangu. Ule ule muda nikamwambia sawa nimekuelewa,,nakumbuka ilikuwa majira ya saa mbili usiku nikarudi zangu hostel, nikaenda kuoga nikarudi kitandani cha kwanza nilifuta namba yake afu na kila aina ya kumbukumbu yake kwenye simu, nikalala lakini usingizi unagoma hautaki kabisa ni mawazo tu, usingizi unakuja kukubali saa 10 usiku huko toka saa tatu. Siku mpaka siku nikaanza kurecover taratibu baada ya miezi mi3 nikakaa sawa. Fara yule si kuna siku akanitafuta ananiambia nimsamehe , anahisi hakuwa yeye aliyesema maneno yake anahisi alirogwa. Nikamkaribisha upya moyoni nikampa nafasi ya kicheche tu this time yeye ndie alikoma mzee.