Mwanamke Akishaamua Kukuacha, Yamekwisha

...

Kaka yangu… acha kujidanganya. Acha kujipa matumaini yasiyokuwepo. Mwanamke akishaamua kukuacha, yamekwisha. Naomba nikueleze kitu—hawezi kurudi. Hawezi hata kusikiliza kilio chako.

Unajua ni kwanini?
Ni Kwa sababu hakukuacha leo. Hakukuacha jana. Alikuacha kitambo. Muda mrefu kabla hujagundua. Alianza kuondoka taratibu, polepole, hadi siku ile alipokusimamia kwa macho baridi macho makavu na kukuambia "hatuwezi kuendelea hivi." Lakini ukweli ni kwamba, siku hiyo ilikuwa mwisho kwa upande wako tu, kwa upande wake, ilikuwa ni hatua ya mwisho ya safari aliyokwishaianza mda sana .

Ulishawahi kuhisi yule mtu unayempenda anabadilika? Sauti yake ikawa baridi? Macho yake yakaacha kuwa na mwanga ule wa zamani? Mapenzi yake yakawa ni hisani badala ya hisia? Ndiyo, kaka yangu, haya yote yalikuwa ishara, lakini hukuwa tayari kuziona. Ukaziipuuza.

Nakuelewa kaka, inauma. Inauma kwa namna ambayo hutaweza kueleza kwa mtu yeyote. Ni kama kisu cha moto kinapita taratibu moyoni mwako, ukinyakua kila matumaini uliyokuwa nayo. Ni kama dunia imesimama, na wewe umetelekezwa ukiwa peke yako, ukiwauliza majirani na marafiki "Nilikosea wapi?" Lakini hakuna atakayekujibu.

Muda wa mwisho mlikuwa pamoja, uliona alivyokuwa tofauti. Hakukuchekea tena kwa furaha ile ya dhati ulioizoea. Alianza kukaa mbali. Alianza kukosa hamu ya kuwa na wewe. Kila ulipomgusa, aliinama pembeni. Kila ulipojaribu kumwambia "nakupenda," alijibu tu "Asante."

Na sasa amekwambia hadharani—yamekwisha. Mwisho.

Unataka umwambie nini ili abaki? Kwamba bado unampenda? Kwamba umebadilika? Kwamba utakuwa bora zaidi? Haijalishi, kaka. Haijalishi. Moyo wake umeshakufa ndani yako. Hisia zake zimezikwa. Huwezi kufufua mfu.

Labda amepata mwingine, mtu anayempa kile ulichoshindwa kumpa. Labda alishapata yote aliyohitaji kutoka kwako, na sasa huna maana tena. Au labda, amechoka tu, na hakuna unachoweza kufanya kumrudisha.

Inauma sana. Inavunja moyo. Inakufanya ujihisi mdogo, mnyonge, duni, asiye na thamani. Utabaki ukikumbuka sauti yake, harufu yake, mguso wake, kicheko chake
vyote vikitesa nafsi yako kwa kukukumbusha kuwa si vyako tena.

Lakini kaka… japo inauma, japo machozi yanakufunika macho, japo moyo unataka kupasuka, lazima ukubali. Huwezi kumbembeleza arudi. Huwezi kumlazimisha akupende tena. Mtu akikupoteza, usijipoteze na wewe pia.

Siku moja, utapona. Lakini kwa sasa, lia. Lia mpaka machozi yaishe. Umia mpaka uchoke. Lakini usirudi nyuma. Kwa sababu kilichokufa hakiwezi kufufuka.

Imekwisha. Mwisho. Piga moyo konde, maisha yanaendelea.

ibn kimweri.
Huu ujumbe ni wa Azizi Ki au na sisi unatuhusu?
 
Kuachwa na mwanamke ndiyo uandike gazeti lote hilo?
Hatuoi wanawake kwa ajili ya mbunye bali stability, peace of mind, respect....
 
Hakuna wa kukucheka mkuu kwasababu kila mtu hupita huko
Nasemaje huyo mwanamke kuna alichonacho na wanawake wengine hawana ndio maana uka mtongoza

Kijana ndio maana una wanawake wawiliwawili unawapima na wewe unajua kuna mmoja ana vigezo uvitakavyo mwingine hana

So wanawake hawafanani.. mfanano wao upo kwenye mood swings but vinginee vyote hawafananii
Ndio maana kuna kubwa ndogo chuchu saa. 10 na chuchu saa 1… namba 8 na namba 27 mfupi kwa mrefu… mlokole kwa mtu wa club so we are deferent
Hata mm ni wa kipekee kwake na ndio maana kati ya makumi ya wanaume walio mtongoza alinichagua na kunikubalia mm na kuwakataa wengine.
Acha kukaza shingo yaani mwanamke asiye changia chochote katika maisha yangu zaidi ya kunipanulia mapaja ndo nikonde na nishindwe kufanya mambo yangu kisa kaondoka? labda awe ameniroga lakini kama nina akili zangu timamu hicho kitu hakiwezi kutokea.
Ukiona mwanaume anajiliza kisa mwanamke ujue anakasoro kubwa katika uanaume wake.
Tatizo la wanaume wa sasa ni kudhani kuwa mapenzi ya mwanaume kwa mwanamke ni wajibu lakini mapenzi ya mwanamke kwa mwanaume ni hisani na ndio maana vijana wa sasa wamekuwa watumwa wa wanawake.
 
Sasa ni wewe ndio unaokutana na hao wanawake wasio na mchango kwako zaidii ya kukupanulia.. wenzako wanakutana na wanawake ambao kwa 70% wameinuka kiuchumi kupitia wao ndio maana wanaumia so usimcheke mwenzio Kama hayajakukuta
 
01e576edca1c4a549da81fa90498a222.jpg
 
Back in days chuoni.
Demu fulani alinizimikia sana na me nilimzimikia sana penzi likawa moto sanaa, khaa miezi 7 baadae ananiambia anaona tuachane, namuuliza kwanini ananiambia haoni future kwangu. Ule ule muda nikamwambia sawa nimekuelewa,,nakumbuka ilikuwa majira ya saa mbili usiku nikarudi zangu hostel, nikaenda kuoga nikarudi kitandani cha kwanza nilifuta namba yake afu na kila aina ya kumbukumbu yake kwenye simu, nikalala lakini usingizi unagoma hautaki kabisa ni mawazo tu, usingizi unakuja kukubali saa 10 usiku huko toka saa tatu. Siku mpaka siku nikaanza kurecover taratibu baada ya miezi mi3 nikakaa sawa. Fara yule si kuna siku akanitafuta ananiambia nimsamehe , anahisi hakuwa yeye aliyesema maneno yake anahisi alirogwa. Nikamkaribisha upya moyoni nikampa nafasi ya kicheche tu this time yeye ndie alikoma mzee.
Ilikuajee? Em maliziaa.

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
 
Ahahahahah.. haya mambo haya bwana. Yana furahisha na kuchekesha na kusikitisha humo humo.
Mi naendelea kujifunza tu.
 
Dah imenigusa sana, mwezi wa kumi huu nambembeleza arud nyumban tuendelee na ndoa hanielew, juzi nusu nife kwa ulevi uliopindukia kisa yey dah so sad, nmeshndwa kuendelea bila yeye nachakaa yeye akipendeza [emoji25][emoji25][emoji25], miaka 7 mahusiano, 5 kwenye ndoa dah
Aisee poleee sanaa.

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
 
Kuumizwa na mahusiano kupo.

Kwa mfano, mpenzi wangu akiiba ATM card kwenda benki kutoa pesa zangu, hapo nitaumia.

Au aniibie hati ya kiwanja akauze na kutokomea.

Yaani niumie kisa ameondoka tu?!

Siyo kweli. Eti mazoea!

Sikatai wapo wanaoumizwa, ila ni wanaume dhaifu sana na ni wapumbavu tu.

Mwanaume kuendekeza hisia ni ujinga wa kishamba.

Nasema hivi, huyo mwanamke hakuna alichonacho ambacho wengine hawana. Wapo wengi tu wanamzidi kwa kila sifa aliyonayo.

Lazima ujue, kwa asilimia zaidi ya 90, mwanamke ni liability kwa mwanaume, yaani nikae kulilia liability!, si watanicheka watu.
Mimi kilichoniumiza kwangu ni family. Kwangu kuijenga familia was my serious buziness and my delicate investiment i ever though i had. Hivyo wife alichonifanyia haikuniuma haswa kwakua ni mapenzi ila niliona amenikatili kwa kuzamisha iwekezaji wangu wa ober 15 years.
Mapenzi sio ki vile ila i considered her as a very significant pillar of my life kwakua ndoto zangu katika ujenzi wa familia kwa kiwango kikubwa alikua na umuhimu mkubwa.
Kumbe wewe unatumia akili sana yeye anatumia hisia sana. Hapa ndio shida.
 
Back
Top Bottom