Mwanamke Akishaamua Kukuacha, Yamekwisha

Mwanamke Akishaamua Kukuacha, Yamekwisha

Back in days chuoni.
Demu fulani alinizimikia sana na me nilimzimikia sana penzi likawa moto sanaa, khaa miezi 7 baadae ananiambia anaona tuachane, namuuliza kwanini ananiambia haoni future kwangu. Ule ule muda nikamwambia sawa nimekuelewa,,nakumbuka ilikuwa majira ya saa mbili usiku nikarudi zangu hostel, nikaenda kuoga nikarudi kitandani cha kwanza nilifuta namba yake afu na kila aina ya kumbukumbu yake kwenye simu, nikalala lakini usingizi unagoma hautaki kabisa ni mawazo tu, usingizi unakuja kukubali saa 10 usiku huko toka saa tatu. Siku mpaka siku nikaanza kurecover taratibu baada ya miezi mi3 nikakaa sawa. Fara yule si kuna siku akanitafuta ananiambia nimsamehe , anahisi hakuwa yeye aliyesema maneno yake anahisi alirogwa. Nikamkaribisha upya moyoni nikampa nafasi ya kicheche tu this time yeye ndie alikoma mzee.
Dawa ni moja, akikwambia tuachane mwambie sawa...unajua nini?😂😂😂😂
 
Hakuna wa kukucheka mkuu kwasababu kila mtu hupita huko
Nasemaje huyo mwanamke kuna alichonacho na wanawake wengine hawana ndio maana uka mtongoza

Kijana ndio maana una wanawake wawiliwawili unawapima na wewe unajua kuna mmoja ana vigezo uvitakavyo mwingine hana

So wanawake hawafanani.. mfanano wao upo kwenye mood swings but vinginee vyote hawafananii
Ndio maana kuna kubwa ndogo chuchu saa. 10 na chuchu saa 1… namba 8 na namba 27 mfupi kwa mrefu… mlokole kwa mtu wa club so we are deferent
Hii naitaka sana, huna kapicha ka sample 😅
 
Back in days chuoni.
Demu fulani alinizimikia sana na me nilimzimikia sana penzi likawa moto sanaa, khaa miezi 7 baadae ananiambia anaona tuachane, namuuliza kwanini ananiambia haoni future kwangu. Ule ule muda nikamwambia sawa nimekuelewa,,nakumbuka ilikuwa majira ya saa mbili usiku nikarudi zangu hostel, nikaenda kuoga nikarudi kitandani cha kwanza nilifuta namba yake afu na kila aina ya kumbukumbu yake kwenye simu, nikalala lakini usingizi unagoma hautaki kabisa ni mawazo tu, usingizi unakuja kukubali saa 10 usiku huko toka saa tatu. Siku mpaka siku nikaanza kurecover taratibu baada ya miezi mi3 nikakaa sawa. Fara yule si kuna siku akanitafuta ananiambia nimsamehe , anahisi hakuwa yeye aliyesema maneno yake anahisi alirogwa. Nikamkaribisha upya moyoni nikampa nafasi ya kicheche tu this time yeye ndie alikoma m
Daah kiukwel mapenz yanauma sana ila ikitokea mmeachana ndiyo basi tena
 
...

Kaka yangu… acha kujidanganya. Acha kujipa matumaini yasiyokuwepo. Mwanamke akishaamua kukuacha, yamekwisha. Naomba nikueleze kitu—hawezi kurudi. Hawezi hata kusikiliza kilio chako.

Unajua ni kwanini?
Ni Kwa sababu hakukuacha leo. Hakukuacha jana. Alikuacha kitambo. Muda mrefu kabla hujagundua. Alianza kuondoka taratibu, polepole, hadi siku ile alipokusimamia kwa macho baridi macho makavu na kukuambia "hatuwezi kuendelea hivi." Lakini ukweli ni kwamba, siku hiyo ilikuwa mwisho kwa upande wako tu, kwa upande wake, ilikuwa ni hatua ya mwisho ya safari aliyokwishaianza mda sana .

Ulishawahi kuhisi yule mtu unayempenda anabadilika? Sauti yake ikawa baridi? Macho yake yakaacha kuwa na mwanga ule wa zamani? Mapenzi yake yakawa ni hisani badala ya hisia? Ndiyo, kaka yangu, haya yote yalikuwa ishara, lakini hukuwa tayari kuziona. Ukaziipuuza.

Nakuelewa kaka, inauma. Inauma kwa namna ambayo hutaweza kueleza kwa mtu yeyote. Ni kama kisu cha moto kinapita taratibu moyoni mwako, ukinyakua kila matumaini uliyokuwa nayo. Ni kama dunia imesimama, na wewe umetelekezwa ukiwa peke yako, ukiwauliza majirani na marafiki "Nilikosea wapi?" Lakini hakuna atakayekujibu.

Muda wa mwisho mlikuwa pamoja, uliona alivyokuwa tofauti. Hakukuchekea tena kwa furaha ile ya dhati ulioizoea. Alianza kukaa mbali. Alianza kukosa hamu ya kuwa na wewe. Kila ulipomgusa, aliinama pembeni. Kila ulipojaribu kumwambia "nakupenda," alijibu tu "Asante."

Na sasa amekwambia hadharani—yamekwisha. Mwisho.

Unataka umwambie nini ili abaki? Kwamba bado unampenda? Kwamba umebadilika? Kwamba utakuwa bora zaidi? Haijalishi, kaka. Haijalishi. Moyo wake umeshakufa ndani yako. Hisia zake zimezikwa. Huwezi kufufua mfu.

Labda amepata mwingine, mtu anayempa kile ulichoshindwa kumpa. Labda alishapata yote aliyohitaji kutoka kwako, na sasa huna maana tena. Au labda, amechoka tu, na hakuna unachoweza kufanya kumrudisha.

Inauma sana. Inavunja moyo. Inakufanya ujihisi mdogo, mnyonge, duni, asiye na thamani. Utabaki ukikumbuka sauti yake, harufu yake, mguso wake, kicheko chake
vyote vikitesa nafsi yako kwa kukukumbusha kuwa si vyako tena.

Lakini kaka… japo inauma, japo machozi yanakufunika macho, japo moyo unataka kupasuka, lazima ukubali. Huwezi kumbembeleza arudi. Huwezi kumlazimisha akupende tena. Mtu akikupoteza, usijipoteze na wewe pia.

Siku moja, utapona. Lakini kwa sasa, lia. Lia mpaka machozi yaishe. Umia mpaka uchoke. Lakini usirudi nyuma. Kwa sababu kilichokufa hakiwezi kufufuka.

Imekwisha. Mwisho. Piga moyo konde, maisha yanaendelea.

ibn kimweri.
Mbona linajulikana hili.
 
Dah imenigusa sana, mwezi wa kumi huu nambembeleza arud nyumban tuendelee na ndoa hanielew, juzi nusu nife kwa ulevi uliopindukia kisa yey dah so sad, nmeshndwa kuendelea bila yeye nachakaa yeye akipendeza 😪😪😪, miaka 7 mahusiano, 5 kwenye ndoa dah
 
Back
Top Bottom