Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Lucia Michael maarufu Mama Kulwa, mkazi wa Majengo Manispaa ya Shinyanga, amekutwa ameuwa na watu wasiojulikana, na mwili wake kutupwa nyuma ya Msikiti wa Majengo.
Picha: Polisi wakichukua mwili wa Marehemu
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, ambapo aligundulika na majirani majira ya saa 12 asubuhi, mara baada ya kuuona mwili wake ukiwa nyuma ya Msikiti wa Majengo jirani na makazi yao akiwa mtupu.
Akielezea tukio hilo mmoja wa majirani ulipokutwa mwili huo, Anastazia Amosi, amesema baada ya kupata taarifa, alifika eneo la tukio na kumkuta jirani yake akiwa mtupu huku akiwa amefariki, ndipo wakamfunika nguo na kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa mtaa.
"Mwanamke huyu ni jirani yetu ana watoto watatu, na kazi yake ni msusi maarufu sana hapa mtaani kwetu, tunasikitika sana kumkuta akiwa ameuawa tena kavuliwa nguo zote," amesema Amosi.
Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo Manispaa ya Shinyanga, Iddi Bwana, amesema mwanamke huyo huenda aliuawa na vibaka, sababu pulukushani zilianzia kwenye vichochoro, na kisha mwili wake kutupwa nyuma ya msikiti jirani na makazi ya watu.
Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, George Kyando, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kubainisha kuwa jeshi bado linafanya uchunguzi ili kubaini chanzo chake na wahusika.