BAKIIF Islamic
JF-Expert Member
- Jul 11, 2021
- 600
- 1,843
Paka ni jamii ya wanyama wadogo, na mara nyingi hujulikana kama paka wa kufugwa ili kumtofautisha na wanyama wa mwituni. Paka anaweza kufugwa kama paka wa nyumbani, paka wa shambani au paka wa porini (Kimburu) ambaye yupo huru na huepuka kuwasiliana na binadamu.
Paka wa nyumbani huthaminiwa na wanadamu kwa urafiki na uwezo wao wa kuua panya. Paka ana mwili wenye nguvu unaonyumbulika, hisia za haraka, meno makali na makucha yanayoweza kurudishwa ili kukabiliana na kuua mawindo madogo.
Mawasiliano ya paka ni pamoja na milio kama vile kulia, kutamka, kupiga miluzi, kuzomea, kunguruma na kuguna na pia lugha ya mwili maalum ya paka. Pia hutumia maono ya usiku na hisia za harufu. Paka ana uwezo wa kusikia sauti hafifu sana ambazo mwanaadamu hawezi kuzisikia, kama vile zile zinazotengenezwa na panya na wadudu wengine wadogo.
Paka wa nyumbani huwa mchangamfu mchana na usiku, ingawa huwa na shughuli nyingi zaidi usiku. Paka wa kienyeji hutumia muda wao mwingi karibu na nyumba zao, lakini wanaweza kufikia mamia ya mita kwenda kutembea. Paka wa nyumbani wanaweza kuwa na shughuli nyingi asubuhi na jioni, na mchana ni muda wao wa kupumzika. Paka huhifadhi nishati kwa kulala zaidi kuliko wanyama wengine, haswa wanapokua.
MWANAMKE HUYU ALIADHIIBIWA
Mwanamke aliyeadhibiwa kwa ajili ya kumtesa Paka
Imepokelewa hadithi kutoka kwa swahaba ‘Abdullaah bin ‘Umar kwamba Mtume wa Mwenyezi MUNGU amesema: (Mwanamke fulani aliadhibiwa kwa sababu ya paka aliyemfungia ndani mpaka akafa kwa njaa, na mwanamke huyo akaingia motoni [kwa sababu] alipomfungia paka hakumpa chakula wala hakumnywesha maji wala hakumwacha aende akale vidudu ardhini)
Funzo kwa wanaotesa wanyama wanaowafuga kwa kuwafungia na kutokuwapa chakula au maji kwamba adhabu yao na wenyewe MUNGU atawaingiza motoni. Huruma ya Mwenyezi MUNGU ni pana mno hata kwa viumbe vyake vyote, mpaka wanyama wadogo. Kila kiumbe kapatiwa rizki yake, kama Anavyosema:
''Na hakuna kiumbe chochote kitembeacho katika ardhi isipokuwa riziki yake iko kwa Mwenyezi MUNGU; na (MUNGU) Anajua mahali pake pa kustakiri na pa kuhifadhiwa kwake. Yote yamo katika kitabu kinachobainisha. [QUR'AN (12: 6)]
Paka ni mmoja katika viumbe wa Mwenyezi MUNGU waliokuwa ni wenye kuishi na binaadamu na kuwazoea kwa ukaribu. (Paka ni rafiki wa kweli).
Siku moja Mtume (s.a.w) alipokuwa akitaka kutawadha na maji tayari yako katika chombo, mara akaja paka akataka kumywa maji ya udhu ya mtume (s.a.w.)
Mtume s.a.w akamuinamishia chombo Kile yule paka ili anywe, na akanywa paka huyo, mwanamke mmoja katika maswali akashangaa kwa hilo.
Akasema mtume s.a.w kumwambia mwanamke huyo :
"Unashangaa hili? hawa ni katika wanaukutembeleeni nyinyi ' yaani wako nanyi kila mara majumbani mwenu. Na kuna mwanamke aliingia motoni kwa sababu ya paka, alimfungia ndani na hakumpa chakula wala kumuacha atafute wadudu wa ardhini mwenyewe, mpaka akafa.
Siku nyingine kuna swahaba wa Mtume (s.a.w) aitwae Abd Shams Ibn Sakhr (Abu Hurairah) alisema
"Niliitwa Abu Hurairah kwa sababu nilikuwa nikichunga mbuzi wa familia yangu, na siku moja nilimkuta paka aliyepotea ambaye nilimweka kwenye mkono wangu. Niliporudi kwa watu wangu walisikia paka akiruka kwenye mkono wangu na wakauliza. “Ni nini hicho ewe Abd Shams?” Nikajibu, “Nimepata paka.” “Basi wewe ni Abu Hurairah (Baba wa paka),” walijibu na jina likakwama baada ya hapo jina likawa maarufu la ABU HURAIRAH (Baba wa paka)''
Na mwenye kuuwa paka wa mtu mwingine bila ya haki, atagharamishwa na kumlipa mwenye paka huyo thamani yake. Kwa sababu paka anahesabika kuwa ni Mali, na anafaa kisheria kufugwa na wala sio najisi mwili wake wala mate yake. .
Kwa hiyo haipasi Mwanaadamu kumzuilia mnyama chakula chake. Funzo kwamba wanyama wanapaswa kupewa haki zao kama viumbe vinginevyo. Bainisho la ruhusa ya kufuga baadhi ya wanyama nyumbani kama paka. Paka ameruhusiwa kufugwa nyumbani.
Muislamu ni lazima awe kielelezo chema katika kuwatendea viumbe wote wema na kuwapatia haki zao kikamilifu.