Mwanamke aliyekatwa Mkono akiamua ugomvi Uchunguzi wakwama, Polisi wadai Bajeti imekosekana

Mwanamke aliyekatwa Mkono akiamua ugomvi Uchunguzi wakwama, Polisi wadai Bajeti imekosekana

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mwanamke aitwaye Nancy Simon, Balozi wa mtaa wa Olekeriani, kata ya Olasiti jijini Arusha, ambaye alikatwa mkono akijaribu kumuokoa mwanamke aliyekuwa akishambuliwa na mume wake, ameeleza kuwa uchunguzi wa kesi yake umegonga mwamba. Askari mpelelezi wa tukio hilo amesema kuwa kesi hiyo haiwezi kuendelea hadi bajeti itakapotengwa na serikali.

Nancy, akizungumza na GADI TV, amesema kesi hiyo imekwama kwa zaidi ya miezi sita, na hajapata msaada wowote kutoka kwa viongozi wa chama chake cha CCM wala Serikali, licha ya miaka kumi ya kuwahudumia wananchi kama Balozi wa mtaa.

Nancy amepata msaada wa mkono wa bandia hivi karibuni kutoka kwa shirika moja lisilo la kiserikali baada ya mahojiano na GADI TV kufichua madhila aliyopitia. Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Justine Masejo, kwa maelezo zaidi juu ya tukio hilo zimegonga mwamba baada ya simu yake kutopokelewa.
Pia, Soma:
 
Back
Top Bottom