Mwanamke aliyevunja rekodi ya kuwa na ndevu nyingi

Mwanamke aliyevunja rekodi ya kuwa na ndevu nyingi

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Harnaam Kaur wa Slough, Uingereza amekuwa ni kijana ambaye anawavutia wengi kwa rekodi yake. Ameweza kusimama baada ya mika mingi ya kudhihakiwa na kutaniwa na walio wengi kuhusu muonekano wake. Vijana wengi wanavutiwa na uajsiri na moyo alionao kushinda dhihaka za watu hao

Alipokuwa na umri wa miaka 24 ndio alivunja rekodi hiyo. Yeye ni msichana mdogo ambaye ana ndevu nyingi kuliko wote duniani. Amekubali taji la rekodi hiyo baada ya miaka ya kudhihakiwa

Alikutwa na polycystic ovary syndrome, ambao unasababisha nywele zikue katika uso wake kwa kuwa ana testosterone nyingi. Harnaam aliwahi kunyoa ndevu zake zote lakini alipopata nguvu ya kuzishinda dhihaka akaacha zikue

Harnaam anasema alishindwa kuelewa nafasi yake katika dunia hii kwa kuwa mwanamke mwenye ndevu. Lakini alijifunza kusimama juu ya dunia na kujivunia kama mwanamke mwenye kuonyesha kujiamini kwa jinsia zote mbali na fikra za jamii. Na aliamini amezaliwa kuwasaidia watu kujiamini na kuridhika jinsi walivyo

1581514190074.png


1581513001731.png

Harnaam Kaur​
 
Back
Top Bottom