Under-cover
JF-Expert Member
- Nov 13, 2023
- 1,834
- 3,042
Mwenye hekima hufikiri sana, kuwa makini broo, yani kuwa makini haswa huyo ana target fulani,Habari wakuu,
Nahitaji wenye uzoefu au mifano halisi katika hili nisije ingia mkenge au kufanya maamuzi sio mazuri
Nilikutana katika ofisi napofanya kazi na Mwanamke ambae tuliwahi kusoma wote miaka mingi Chuo kikuu lakini hatukuwahi kuwa karibu. Zaidi ya kusalimiana mara chache tunapopishana corridor za chuoni
Kweli nilipomuona nkatoka ofisini kwangu nimsalimie pia nimkumbushe sababu yeye alidai kanisahau
Tukabadilishana namba tukawa tunawasiliana hatukuzidi miezi 4 tukaanza Mahusiano. Kikwazo kikubwa tupo mikoa tofauti na yeye yupo NGO'S na Mimi nipo Serikalini.
Kweli ni mwanamke ambae kanishinda maendeleo ameshajenga ana viwanja na asset na mshahara mkubwa simpati
Kweli hatuna mwezi katika Mahusiano yetu lakini wimbo wake Tuzae. Mpaka namwambia hatujawahi kuwa karibu hata kuchunguzana kwa muda mfupi tunaishi mikoa tofauti kwasasa itakuaje katika malezi.
Yeye anasema atamhudumia mtoto anachotaka tu Mimi nitambulike kwao.
Na maisha ya kwao kweli ni Mazuri.
Nimebaki njia panda kwanini aharakishe haya masuala na Mimi nimemuambia anipe muda kusudi nijipange procedure za kumuoa kwanza nianze tupate muda kufahamiana kwa ukaribu zaidi.
Nisaidieni mawazo yenu.