Kipindi cha afya hai ya uzazi wa mwanamke hutawaliwa na mizunguko ya hedhi ya kila mwezi ambayo hukoma baada ya kupata ujauzito, muda mchache baada ya kujifungua na pia baaada ya kufikia umri wa ukomo wa hedhi.
Kwa maana rahisi, mwanamke hawezi kupata ujauzito ikiwa hapati hedhi.
Hata hivyo, tumesikia mara kadhaa baadhi ya wanawake wakitoa madai kuwa wamepata ujauzito muda mfupi tu baada ya kujifungua, kabla hata hedhi yao ya kwanza haijarudi.
Madai haya yana ukweli kiasi gani?
Kwa maana rahisi, mwanamke hawezi kupata ujauzito ikiwa hapati hedhi.
Hata hivyo, tumesikia mara kadhaa baadhi ya wanawake wakitoa madai kuwa wamepata ujauzito muda mfupi tu baada ya kujifungua, kabla hata hedhi yao ya kwanza haijarudi.
Madai haya yana ukweli kiasi gani?
- Tunachokijua
- Baada ya kupata ujauzito, mifumo ya mwili wa mwanamke huzuia upevushaji wa mayai mengine ya uzazi ili kuzuia kutengenezwa kwa ujauzito mwingine.
Tendo hili huenda sambamba na kukoma kwa hedhi hadi pindi atakapojifungua.
Kwa mujibu wa Kituo Cha Udhibiti na Kinga ya Magonjwa (CDC), ndani ya kipindi cha unyonyeshaji cha miezi 6 ya mwanzo baada ya kujifungua, mwanamke anaweza asipate ujauzito ikiwa mambo matatu yatazingatiwa-
- Mtoto awe chini ya umri wa miezi 6
- Mtoto anyonye maziwa ya mama pekee pasipo kupewa vyakula, maji na maziwa mbadala kwa utaratibu wa kila baada ya saa 4 kwa muda wa mchana na saa 6 kwa muda wa usiku.
- Hedhi isiwe imerejea
Mimba itatokeaje kabla ya hedhi ya kwanza?
Kwa mujibu wa marejeo ya utafiti wa Obstetrics and Gynecology (2011), baadhi ya wanawake hupevusha mayai na kupata hedhi ya kwanza kati ya siku 45-94 baada ya kujifungua. Pia, baadhi yao hutumia muda mrefu zaidi ya huu ambao unaweza kufikia miezi 6 hadi mwaka mmoja.
Ili ujauzito uweze kutungwa, ni lazima kwanza mwanamke epevushe mayai yake kisha yakutane na mbegu za kiume.
Kutokea kwa hedhi hutoa maana ya kushindwa kuungana kwa yai na mbegu za kiume, hivyo ni tendo la mwisho linalofuata baada ya kupevushwa kwanza kwa mayai.
Hivyo, JamiiForums imebaini kuwa ikiwa mwanamke atashiriki tendo la ndoa kwenye siku zenye uwezekano mkubwa zaidi wa kupata ujauzito katika mwezi ambao hedhi yake ya kwanza ilipaswa kutokea, uwezekano wa kupata ujauzito upo hivyo hedhi ya kwanza haitaonekana.
Hii inatoa uthibitisho wa uwepo wa uwezekano wa mwanamke kupata ujauzito akiwa ananyonyesha, kabla hata hajapata hedhi yake ya kwanza baada ya kujifungua.
Ushauri
Ili kujiweka salama zaidi, mwanamke hushauriwa kunyonyesha kikamilifu kwa kuzingatia masharti yaliyoainishwa pamoja na kutumia njia mbadala za kujilinda na ujauzito wa mapema hasa ikiwa ataona dalili za kurejea haraka kwa hedhi yake kinyume cha matarajio.