Mwanamke anayejiweza kimaisha

  • Thread starter Thread starter JS
  • Start date Start date
Kuna mdada alijifukarisha baada ya kuona hapati mchumba. Aliuza gari lake, nyumba na mali nyingine ili apate mchumba!

Haya mambo ni magumu jamani tusifanye mzaha.Ila binafsi sitamshauri mdada ajifanye maskini kisa kakosa mwanaume. Kama alivyosema Boss hapo juu, inategemea mtu na mtu. Wapo wenye uchache na hawaoni kama ni ishu.Inapokuja mahusiano, huwa tayari kupenda kwa misingi ile ile ambayo ingetawala uhusiano hata pale hakuna mali wala nini.
 

unajua wos funny thing haya mambo
wanaume ndio huwa tunakumbana nayo sana...
i mean ukiwa na pesa its tough sometimes kujua
unapendwa kweli au umeopoa a gold digger????
yaani mwanamke mwenye pesa atakuwa hapati mchumba..
but mwanaume mwenye pesa utapata wengi,but huwezi jua which one
is for real.....unaona?????
 

I HEAR YOU mKUU!
 
Wewe hujaelewa nilichoandika hapo hebu soma tena vizuri halafu kama umeelewa nigongee thanks kwa this post then nitakuPM sawa...........haya am waiting

mi nimeshatimiza wajibu wangu hapo juu kabisa ila bado ujumbe wako uko vague. Naomba nibakie kuelewa nilivyoelewa. Now play your part
 
.......Mhhh inawezekana kuna kaukweli fulani kwamba mwanamke ukiwa na pesa/mali kupata mwanaume makini wa kutangaza nia kazi. Sio kwamba hupati wanaume kabisa hapana, wanaume watakuja kwako lakini wengi wao wanaogopa wakiona binti amejitosheleza kwa kila kitu.

......Kuna mdada naye hivyo hivyo umri wake sasa ni 35, ana kazi nzuri kwenye shirika kubwa na mshahara mzuri, usafiri wa maana na nyumba yake ya maana lakini masikini hapati mwanaume wa kumuoa........mwenyewe utakuta analalamika tena anasema kabisa watoto wadogo mnaolewa lakini yeye hapati mume.Yaani huyu mdada ana tabia nzuri na mpole lakini wanaume wanamuogopa kwa uwezo aliokuwa nao. Labda siku moja atakuja kupata mume mie huwa namuonea huruma.
 

really?
Yupo hapa hapa dar?
 
Nimesoma post zote, nilichokiona jamii nzima ina mfume dume, hata baadhi ya wanawake wanasupport hicho kitu, binafsi naona mapenzi hayana uhusiano kabisa na pesa,elimu, umri na vitu vingine, unavyoaamua kumpenda mtu mpende kwa jinsi alivyo, sio kwa sababu ya abc alizonazo, niujuavyo upendo una mambo mengi sana, hueshimu,huthamini, huudijadai, hauhesabu mabaya wala mazuri, na mengine mengi mazuri, sasa mnahangaika kwa sababu 2 eti mwanamke kakuzidi pesa, then u married a wrong woman, wa kwako yupo some where
 

Dada Pretty
Ebu niunganishe kwake..
 
samahani lakini eti the boss iyo avatar yako,kweli?
 
- Kusema ukweli mimi nikiwa kama mzazi sikubali mwanangu awe na Kauwezo kake halafu anapata mwanaume mlofa kisha nimkubalie aoe mwanangu,NEVER sikubali kbs. Lofa atafute malofa wenzie Na huo ndio ukweli vinginevyo ndoa hiyo haitadumu. tumeshuhudia ndoa nyingi sana za aina hiyo.

- Turudi kwenye mpango wa Mungu ni kwamba Mwanaume ndo anaetakiwa kumtunza na kumpenda mke. Mke yeye kazi yake ni kumheshimu na kumtii tu.:smile-big:
 

kazi ipo.....
 


well said Boss...
 
Ramwai ...................huyo mwanao kama mapesa kayapata kwa nguvu yake sidhani kama atakusikiliza sana kuhusu nani amkubali kumuoa. Lakini jipe moyo huenda.......:smile-big:
 
kwahiyo mwanamke aache kila kitu kwa ajili ya kuolewa au just to help guys with their insecurity problem?
 

Tema mate chini ndugu yangu hapo penye rangi nyekundu. Ni kweli kila mzazi hutamani the best kwa mwanaye lakini wakati mwingine huwa ngumu. Wazazi wanajitahidi hata kuwaleta pamoja watoto wao ( Familia kwa familia) ili angalau waoane wenye levels za kufanana.Kuna waliofanikiwa kuwaoza watoto wao lakini ndoa hizi nazo wakati mwingine hazidumu. Ili mwisho wa siku tukubali kuwa "mwanamke mwenye nacho anatisha"... wanaume wengi hujiona duni kwa mdada wa namna hiyo au hujistukia kila mara hata pale pasipo na sababu. Kinachotakiwa kuzuia/kupunguza hali hii ni kuacha mambo yachukue mkondo. Kuolewa mapema huenda ni suluhisho na hapa akina dada wawe wepesi kukubali vigezo minimum ( kwangu mimi the minimum non-negotiables ni elimu ya "kutosha"maana itaonyesha potential for growth, heshima, usafi binafsi wa mwili na mazingira anamoishi, mcha Mungu, mkarimu/mcheshi, mchapa kazi, mwenye kiu ya maendeleo) .. msichana asitafute mwanaume tajiri au makuu zaidi. Hapo ataolewa mapema akiwa bado hajajilimbikizia mali. Halafu watatafuta mali pamoja.
 


Sasa Boss tangaza nia basi mmmh..............:A S 8::A S 8::A S 8::A S 8::A S 8:
 
WOS umeongea point i muhimu, lakini wengine wanaipata chenji mapema sana...........mtu 25 anakuwa mambo yake mazuri tayari, by the time akifika 27 wanaume wanampiga chenga hata kumsogelea hawamsogelei.🙁


noname hamna kuacha kutafuta pesa kwa kuogopa insecurities za wanaume, atatokea tu atakaekupenda wewe na pesa zako japo itachukua muda kidogo.
 

Dada G, nadhani hakuna aliyesema kuwa mwanamke asitafute pesa kwa sababu akizipata hataoelewa. Wewe ndo ulisaidia sana kuleta evidence za kisayansi kabisa kuonesha nini wanaume na wanawake wanazingatia wakati wa kutafuta wenza watarajiwa. Kwa hiyo tumejaribu kueleza hali halisi ili mwanamke hata akiwa na pesa basi ajue hali inayoweza kumkuta. Hata hivyo bado kuna exceptions ingawa sina hakika kama kuna mtu anaweza ku-bet ili aingie kwenye hilo kundi kwani zinatokea kwa bahati. Tungekuwa katika jamii nyingine nisingesita kuunga mkono hoja. Binafsi nimefanya kazi na dada mmoja toka UK ambaye alikuwa na PhD na wakati huo mume wake alikuwa baba wa nyumbani analea mtoto. Ila kwa wanaume wa kibantu nadhani hiyo ni adhabu sawa na kuwa Ukonga au Segerea!
 
kwahiyo mwanamke aache kila kitu kwa ajili ya kuolewa au just to help guys with their insecurity problem?

shangaa na wewe dearest, ili kupata ndoa naona kuna masharti mengi sana, yaani hata ka kazi inabidi nikaache nirudi kijijini kwetu katelelo ili nipate mchuchu,kazi kweli kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…