Mwanamke: Dalili kwamba very soon utaisaliti ndoa yako

couple-e1291045828625.png

Katika mahusiano wanawake wanakabiliwa na changamoto nyingi. Kuna wakati mwanamke anaweza kujaribiwa na kujikuta akikabiliwa na hatari ya kumsaliti mwenzi wake.

Kujaribiwa huko kunaweza kukatokea katika mazingira mbalimbali kutegemea na mazingira yaliyomzunguka mwanamke. Lakini pia yapo mazingira yanayoweza kuchochewa na mahusiano yaliyopo kati ya mke na mume na mara nyingi kwa sababu wanawake ni viumbe wa hisia wanakuwa ni rahisi sana kugundua iwapo kutakuwa na tofauti katika mahusiano yake na mwenzi wake.

Hali hiyo inaweza kuamsha udadisi jambo ambalo linaweza kuleta matokeo ambayo si mazuri. Mara nyingi udadisi huo unaweza kugeuka kero kwa mwanaume na kuhisi kunangwa (Nagging) hivyo kuwa mkali na kusababisha kuwa na tafrani za mara kwa mara kitu ambacho siyo afya katika maisha ya ndoa.

Pale ambapo mahusiano yanapokuwa na hali ya kutoelewana kwa sababu ya mwanamke kuwa na hofu ya kusalitiwa mawasiliano ya wanandoa hao yanaweza kuwa mabaya na hivyo kusababisha mwanamke kutafuta mtu mwingine ambaye anadhani atamsikilizwa.

Ingawa kwa mara ya kwanza anaweza kuongea na baadhi ya marafiki zake wa kike ili kupata ushauri, lakini mara nyingi huvutika zaidi na jinsia ya kiume na ndipo hapo mwanamke anapojikuta akiwa na ukaribu na mwanaume ambaye anaonekana kuwa ni msikivu na mwenye busara.

Hapa chini nitaeleza baadhi ya dalili zinazoweza kumuweka mwanamke katika mazingira ambayo ni rahisi kuisaliti iwapo ndoa yake itakumbwa na hali niliyoieleza hapo juu.

madamenoire.com_.jpg

1. Unampenda lakini kuna ukame kitandani

Pamoja na kuwa unajitahidi kumuonyesha mapenzi ya dhati na kuhakikisha unajitahidi kujiweka katika mazingira ya kumvutia mwenzi wako kimapenzi lakini yeye wala haonyeshi kuvutiwa nawe na uwezo wake wa kushiriki tendo la ndoa unadorora siku hasi siku.

Unajaribu kuzungumza na mwenzi wako ili kupata suluhu lakini mwenzako hatoi ushirikiano.

Matokeo yake: Jambo hilo linaweza kumpa mwanamke wakati mgumu kiasi kwamba kama akipata kishawishi ni rahisi sana kwake kuisaliti ndoa yake.

date-11.jpg

2. Anaweza kuwa ni rafiki tu,....... lakini!

Una mgogoro na mwenzi wako, halafu unakuwa na rafiki wa kiume anayeteka hisia zako, inaweza ikawa ni mfanya kazi mwenzio au ni mwanaume uliyekutana naye katika mazingira ya aina yoyote na kujikuta ukiwa na ukaribu naye kiasi cha kuwa na mitoko ya mara kwa mara.

Matokeo yake: Hali hiyo haiwezi kuwa na mwisho mwema, ni mojawapo ya kiashiria kwamba bado kitambo kidogo utaisaliti ndoa yako.

Dating-woman-looking-out-window.jpg

3. Unamfumania live akiisaliti ndoa yenu

Unaweza ukamfumania mwenzi wako akiwa na mwanamke mwingine wakifanya tendo au ukamfumania akiwa na mwanamke mwingine katika mazingira ya kutia shaka au unaweza kufumania ujumbe mfupi wa simu katika simu yake kutoka kwa mwanamke mwingine.

Unapojaribu kumuuliza anakuwa mkali na hataki mjadili jambo hilo. Katika mazingira kama hayo unaweza kujikuta ukipoteza imani naye au ukajikuta mkiwa mnagombana mara kwa mara kwa sababu ya mambo madogo madogo.

Matokeo yake: Hali hiyo inaweza kumtia mwanamke kishawishi cha kuisaliti ndoa yake. “Kama yeye anafanya kwa nini na mimi nisifanye?” Mwanamke anawza kujiuliza. Hapo hakuna mjadala mwanamke anaweza kuisaliti ndoa yake wakati wowote

stk144383rke.jpg

4. Unakuwa na mitoko na marafiki zako bila kumuhusisha

Kutokana na hali ya kutoelewana na kukosekana kwa mawasiliano katika ndoa yenu, unaweza kuamua kuwa na mitoko na marafiki zako wa kike bila kumuhusisha mwenzi wako.

Mitoko hiyo inaweza kuwa ni kwenye klabu au kwenye pub mahali ambapo ni rahisi kukutana na watu mbalimbali. Kutokana matatizo ya ndoa uliyo nayo, inawezekana akatokea mwanaume akaamua kuanzisha mazungumzo na wewe.

Matokeo yake: Iwapo mwanaume huyo atakuwa na sifa anazozihitaji au kama anaweza kumudu kuziba pengo la kihisia ambalo mwenzi wake ameshindwa kuliziba, ni dhahiri kwamba mwanamke atakuwa kwenye hatari ya kuisaliti ndoa yake.

black_couple_bar.jpg

5. Unajikuta unashindwa kusema wazi kama umeolewa.

Kama mwanamke katika mazingira ya kawaida unaacha kuvaa pete ya ndoa na unashindwa kusema kuwa ameolewa, ni dhahiri kwamba hutaki watu wajue kuwa umeolewa na hivyo unajiweka katika nafasi ya kutongozwa.

Haina maana kwamba mwanamke aliyeolewa hatongozwi la hasha, kuna baadhi ya wanaume wachache sana wenye ujasiri wa hali ya juu (kasoro mimi) ambao hawaoni aibu kumtongoza mke wa mtu, lakini haiwezi kuwa kwa kiwango cha mwanamke asiyeolewa.

Matokeo yake: Kwa kawaida mwanamke asiyeolewa anaingilika kirahisi na hivyo anaweza kutongozwa na mwanaume yeyote, sasa asipovaa pete ya ndoa na asipoweka wazi kwamba yeye ni mke wa mtu anatarajia nini….
COUPLE+FIGHTING+DAVID+CASTILLO+DOMINICI.JPG

6. Unalianzasha mara kwa mara

Kama mwanamke anajikuta hana mwasiliano ya kueleweka na mwenzi wake na anakabiliwa na ukame wa tendo la ndoa chumbani, ni rahisi sana kuhemkwa na kuwa na kisirani cha ajabu.

Hali hiyo inaweza kusababisha ugomvi wa mara kwa mara na mwenzi wake jambo ambalo halitoweza kuleta suluhu zaidi ya kujenga ufa katika ndoa yao. Kama hali hiyo ya ugomvi ikiendelea bila kupatiwa suluhu mwanamke anaweza kuingiwa na ibilisi wa kuisaliti ndoa yake ili kutafuta nafuu ya kihisia.

Matokeo yake: Kama mwanamke mwenye changamoto hii ya ndoa atakutana na mwanaume anayejua anachokikosa kwa mwenzi wake hatasalimika…..

King'asti, Husninyo, snowhite, Fixed Point, Chocs, MankaM, BADILI TABIA, Kongosho, Munkari, Heaven on Earth,

Somo zuri,ila mbona hujasema ukiona ule motisha,hamu ya kuombea ndoa yako imepungua pia ni dalili?
 
Mie picha zako tu mtambuzi unazowekaga zinaendana kabisa na uzi hasa hiyo ya bidada amekaa kitandani na sura ya mawazo huku jamaa amepiga mbonji hana habari (inaendana na namba moja) ila namba 5 umetuchomekea wewe ni miongoni mwa wanaume wachache jasiri wa kutokea wake za watu na ukibisha naweka evidence kama zile picha za Capt Komba. By the way uzi upo poa ila kama kila mtu kwenye mahusiano tungeelewa kwamba kutofautiana mtazamo/mawazo/hisia ndo sifa kuu ya binadamu mahusiano/ndoa zingedumu
 
Hahaha wanaume kitovu cha mabadiliko! Sasa hapa unataka tuelewe nini?

mwanamke anamfumania mumewe afu anapigwa na mume na kutukanwa na hawara. Unataka mwanamke aelewe nini hapo?

mume anarudi usiku wa manane daily, na akirudi ananuna utadhani kang'atwa na manyuki na hakuvuna asali alikotoka! Mke aelewe nini hapo?

kisirani mwanaume kanuna kushinda mwanamke mjamzito. Hata kama anacheat basi mgao kwa mke uwepo, nehi nehi! Unategemea mwanamke aelewe nini hapo?

kama mmekaa mnasubiria mke atengeneze ndoa, agiza kahawa ya baridi (iced coffee) afu tulia hapo hapo
Somo zuri lakueleweka Mtambuzi ila hao wanawake wakukuelewa sijui wako wapi?
 
Last edited by a moderator:
Tatizo watu wanakosa upendo wakweli na uvumilivu ndiyo maana kunausaliti toka pande zote !
 
Madhara ya kuoana kwa kusukumwa na tamaa za mwili badala ya Upendo ndo haya,kukinaiana ,therefore michepuko plus hatari ya HIV/AIDS!.Sooo sad!
 
Hapo ndipo umesema kweli. &[HASHTAG]#304[/HASHTAG];la kwa mwanaume kucheat ni inevitable. kwahiyo wanaume tucheat re&[HASHTAG]#351[/HASHTAG];ponsibly. Baaas.
Mi si cheat na bado naisoma namba!
 
Mwanamke akiamua kukutesa dunia utaiona chungu mbona!
Ni kweli usemayo,ila kwanini akutese embu jitafakari umesimama kwenye zamu yako? Kichwa cha nyumba hakiwezwi kuteswa bali hutoa direction ambapo mwili wote utafuata,angalia ulikosea wapi? Kama hakuna ulipokosea basi huyo hakuwa ubavu wako, umechukua mbavu ya mtu mwingine kufit kwako itakuwa ngumu,basi tuombe rehema za Mungu tu na Neema yake mbavu hii ikitoshe.
 
couple-e1291045828625.png

Katika mahusiano wanawake wanakabiliwa na changamoto nyingi. Kuna wakati mwanamke anaweza kujaribiwa na kujikuta akikabiliwa na hatari ya kumsaliti mwenzi wake.

Kujaribiwa huko kunaweza kukatokea katika mazingira mbalimbali kutegemea na mazingira yaliyomzunguka mwanamke. Lakini pia yapo mazingira yanayoweza kuchochewa na mahusiano yaliyopo kati ya mke na mume na mara nyingi kwa sababu wanawake ni viumbe wa hisia wanakuwa ni rahisi sana kugundua iwapo kutakuwa na tofauti katika mahusiano yake na mwenzi wake.

Hali hiyo inaweza kuamsha udadisi jambo ambalo linaweza kuleta matokeo ambayo si mazuri. Mara nyingi udadisi huo unaweza kugeuka kero kwa mwanaume na kuhisi kunangwa (Nagging) hivyo kuwa mkali na kusababisha kuwa na tafrani za mara kwa mara kitu ambacho siyo afya katika maisha ya ndoa.

Pale ambapo mahusiano yanapokuwa na hali ya kutoelewana kwa sababu ya mwanamke kuwa na hofu ya kusalitiwa mawasiliano ya wanandoa hao yanaweza kuwa mabaya na hivyo kusababisha mwanamke kutafuta mtu mwingine ambaye anadhani atamsikilizwa.

Ingawa kwa mara ya kwanza anaweza kuongea na baadhi ya marafiki zake wa kike ili kupata ushauri, lakini mara nyingi huvutika zaidi na jinsia ya kiume na ndipo hapo mwanamke anapojikuta akiwa na ukaribu na mwanaume ambaye anaonekana kuwa ni msikivu na mwenye busara.

Hapa chini nitaeleza baadhi ya dalili zinazoweza kumuweka mwanamke katika mazingira ambayo ni rahisi kuisaliti iwapo ndoa yake itakumbwa na hali niliyoieleza hapo juu.

madamenoire.com_.jpg

1. Unampenda lakini kuna ukame kitandani

Pamoja na kuwa unajitahidi kumuonyesha mapenzi ya dhati na kuhakikisha unajitahidi kujiweka katika mazingira ya kumvutia mwenzi wako kimapenzi lakini yeye wala haonyeshi kuvutiwa nawe na uwezo wake wa kushiriki tendo la ndoa unadorora siku hasi siku.

Unajaribu kuzungumza na mwenzi wako ili kupata suluhu lakini mwenzako hatoi ushirikiano.

Matokeo yake: Jambo hilo linaweza kumpa mwanamke wakati mgumu kiasi kwamba kama akipata kishawishi ni rahisi sana kwake kuisaliti ndoa yake.

date-11.jpg

2. Anaweza kuwa ni rafiki tu,....... lakini!

Una mgogoro na mwenzi wako, halafu unakuwa na rafiki wa kiume anayeteka hisia zako, inaweza ikawa ni mfanya kazi mwenzio au ni mwanaume uliyekutana naye katika mazingira ya aina yoyote na kujikuta ukiwa na ukaribu naye kiasi cha kuwa na mitoko ya mara kwa mara.

Matokeo yake: Hali hiyo haiwezi kuwa na mwisho mwema, ni mojawapo ya kiashiria kwamba bado kitambo kidogo utaisaliti ndoa yako.

Dating-woman-looking-out-window.jpg

3. Unamfumania live akiisaliti ndoa yenu

Unaweza ukamfumania mwenzi wako akiwa na mwanamke mwingine wakifanya tendo au ukamfumania akiwa na mwanamke mwingine katika mazingira ya kutia shaka au unaweza kufumania ujumbe mfupi wa simu katika simu yake kutoka kwa mwanamke mwingine.

Unapojaribu kumuuliza anakuwa mkali na hataki mjadili jambo hilo. Katika mazingira kama hayo unaweza kujikuta ukipoteza imani naye au ukajikuta mkiwa mnagombana mara kwa mara kwa sababu ya mambo madogo madogo.

Matokeo yake: Hali hiyo inaweza kumtia mwanamke kishawishi cha kuisaliti ndoa yake. "Kama yeye anafanya kwa nini na mimi nisifanye?" Mwanamke anawza kujiuliza. Hapo hakuna mjadala mwanamke anaweza kuisaliti ndoa yake wakati wowote

stk144383rke.jpg

4. Unakuwa na mitoko na marafiki zako bila kumuhusisha

Kutokana na hali ya kutoelewana na kukosekana kwa mawasiliano katika ndoa yenu, unaweza kuamua kuwa na mitoko na marafiki zako wa kike bila kumuhusisha mwenzi wako.

Mitoko hiyo inaweza kuwa ni kwenye klabu au kwenye pub mahali ambapo ni rahisi kukutana na watu mbalimbali. Kutokana matatizo ya ndoa uliyo nayo, inawezekana akatokea mwanaume akaamua kuanzisha mazungumzo na wewe.

Matokeo yake: Iwapo mwanaume huyo atakuwa na sifa anazozihitaji au kama anaweza kumudu kuziba pengo la kihisia ambalo mwenzi wake ameshindwa kuliziba, ni dhahiri kwamba mwanamke atakuwa kwenye hatari ya kuisaliti ndoa yake.

black_couple_bar.jpg

5. Unajikuta unashindwa kusema wazi kama umeolewa.

Kama mwanamke katika mazingira ya kawaida unaacha kuvaa pete ya ndoa na unashindwa kusema kuwa ameolewa, ni dhahiri kwamba hutaki watu wajue kuwa umeolewa na hivyo unajiweka katika nafasi ya kutongozwa.

Haina maana kwamba mwanamke aliyeolewa hatongozwi la hasha, kuna baadhi ya wanaume wachache sana wenye ujasiri wa hali ya juu (kasoro mimi) ambao hawaoni aibu kumtongoza mke wa mtu, lakini haiwezi kuwa kwa kiwango cha mwanamke asiyeolewa.

Matokeo yake: Kwa kawaida mwanamke asiyeolewa anaingilika kirahisi na hivyo anaweza kutongozwa na mwanaume yeyote, sasa asipovaa pete ya ndoa na asipoweka wazi kwamba yeye ni mke wa mtu anatarajia nini….
COUPLE+FIGHTING+DAVID+CASTILLO+DOMINICI.JPG

6. Unalianzasha mara kwa mara

Kama mwanamke anajikuta hana mwasiliano ya kueleweka na mwenzi wake na anakabiliwa na ukame wa tendo la ndoa chumbani, ni rahisi sana kuhemkwa na kuwa na kisirani cha ajabu.

Hali hiyo inaweza kusababisha ugomvi wa mara kwa mara na mwenzi wake jambo ambalo halitoweza kuleta suluhu zaidi ya kujenga ufa katika ndoa yao. Kama hali hiyo ya ugomvi ikiendelea bila kupatiwa suluhu mwanamke anaweza kuingiwa na ibilisi wa kuisaliti ndoa yake ili kutafuta nafuu ya kihisia.

Matokeo yake: Kama mwanamke mwenye changamoto hii ya ndoa atakutana na mwanaume anayejua anachokikosa kwa mwenzi wake hatasalimika…..

King'asti, Husninyo, snowhite, Fixed Point, Chocs, MankaM, BADILI TABIA, Kongosho, Munkari, Heaven on Earth,
Duuh
 
Back
Top Bottom