I might be a woman but I know a lot about men
Yaani wanaume mmeshajiwekea kwamba mkiwa kwenye mahusiano basi mwanamke anatakiwa awe malaika yaani asikukosee wala asikasirike yaani muda wote awe sawa na mwenye furaha ili akupetpet na akuliwaze wewe tu hata kama umemkwaza au umemfokea yeye atabasamu na acheke tu
Na ikitokea kipindi anakuwa kinyume na hivyo basi tayari anaanza kuonekana mjeuri na kiburi kwamba analeta dharau na kejeli hivyo hafai kuwa mke na anastahili kuchezewa
Ila mwanaume hata akiwa malaya, mkorofi, mnyanyasaji na asiyejali haina shida na mwanamke anatakiwa amvumilie tu maana yeye ni mwanaume na yuko tofauti na mwanamke, ndicho wanaume wengi wa kibongo mnachokitaka kwenye uchumba na ndoa hicho