Mwanamke huyu anadaiwa kuwa nyuma ya mafanikio ya Dokta Cheni

Kuna kitu mtu kanikumbusha, huyo Zahir Zorro nimesoma nae Primary Dar. Nilimsahau kabisa. Alikuwa darasa moja nyuma yetu, Kisarawe Primary School.
Huyo Shagy hatujamfahamu wote, AbdulKareem tuliowafahamu ni kama nilivyokueleza juu huko, na anaefanana na jina Shagy, ni Shedi Sheni, mtoto wa gerezani huyu alikuwa anapiga organ, Mwenyezi Mungu amrehem.

Kuna mtu mwingine nyumba uliyoitaja alikuwa akiitwa Hamza. Halafu wengine tuliwajuwa ni kina marehem Jerry Riyami, hao wote tukijuwana sana utotoni, mtaa huo huo lakini kama unarudi kwenda shule ya Zanaki.

Siku nikimpata au nikimkumbuka ntakujulisha lakini mpaka sasa picha yake haiji kabisa katika watu niliowafahamu enzi hizo mitaa hiyo.

Ukitoka nyumba hiyo unayoisema ukienda kama unaelekea Muhumbili kulikuwa kina Bate, ndugu watatu mabaharia na baba yao alikuwa Captain wa meli. Nadhani wanaishi Australia hivi sasa kasoro mmoja nilikuwa naonana nae Kariakoo, anaitwa Othman, wenhine ni Farouq na Mustafa. hawa ni mitaa hiyo unayosema na walikuwa hawatoki hiyo nyumba, walikuwa na kijiwe chao kinaitwa Black September.

Hapo hapo kwa kina Bate walikuwa Waunguja, kwa Mzee Musa, kina marehem Selemani Mabalungi na dada zake wawili walikuwa marafiki zangu.
 
Kuna vijana wanapiga hesabu hapa muda ambao bi Salma yuko nyuma ya nondo ndio muda ambao ulipotea jukwaani.. Alivyotoka nawe ukarudi kwa kasi ya 5G..

Nawasilisha....
 
Shosti angu faiza umekula maisha iaseeh,yaelekea ulikuwa mrembo Sana🤣hongera kwa umri na bata ulilokula enzi hizo
Saivi naona unashinda ndani tu,ukila,ukichat na kutumia penshen yako taratibuuu.
 
Shosti angu faiza umekula maisha iaseeh,yaelekea ulikuwa mrembo Sana🤣hongera kwa umri na bata ulilokula enzi hizo
Saivi naona unashinda ndani tu,ukila,ukichat na kutumia penshen yako taratibuuu.
Atakuwa toto la kimanga, shomboshombe flani hivi kama Fatma Karume.

Eti FaizaFoxy wewe na Fatma ni rika moja?
 
Atakuwa toto la kimanga, shomboshombe flani hivi kama Fatma Karume.

Eti FaizaFoxy wewe na Fatma ni rika moja?
Fatma Karume ni mdogo sana kwangu. Fikiri ikiwa Zahir Zorro alikuwa darasa moja nyuma kwangu, primary school. Babake banana Zorro ndiyo rika langu.

Nifah kumbe hujaniona? Toto la kishombe la haja, si mchezo mchezo. Mbona picha yangu niliiweka JF.

Nikuwekee?
 
Kuna vijana wanapiga hesabu hapa muda ambao bi Salma yuko nyuma ya nondo ndio muda ambao ulipotea jukwaani.. Alivyotoka nawe ukarudi kwa kasi ya 5G..

Nawasilisha....
Salma wala sikuwa na habari kama kafungwa mpaka nilipousoma uzi huu wa Nifah.

Mpaka sasa naamini alikuwa innocent, na nimejithibitishia hilo kwa kujiridhisha kuwa kweli alifungwa lakini kashinda rufaa yake na kaachiwa huru.

Kupiga hesabu ndiyo maarifa, usilishwe matango na kina #@Nifah hapa, si kama hivyo nimepiga hesabu na imeonekana kweli alikuwa na kesi za kubambikiwa. Na ushahidi wa kesi aliouleta Nifah post namba moja hauhusiani kabisa na kesi alizofungwa, hiyo aliyoweka attachment Nifah ni kesi ya ya madai ya mirathi.

Mpaka sasa Salma, mahakama zimeamuwa kuwa ni innocent, msimpakazie kijinga.
 
Basi nimepata kufahamu rika lako, Zahir nae mjanja sana mzee wa mjini yule hakubali kuzeeka mpaka leo anavaa kama kijana wa miaka 20!

Nakumbuka uliweka picha katika Avatar yako ukasema ndio wewe, kama sivyo basi nimepitwa.

Naomba ufanye hivyo, niwekee.
 
Nimeingia katika uchunguzi rasmi juu ya madai ya Salma kuwa huru, nitaleta majibu kama wewe ulivyofanya.

Kwa sasa naomba nisiongelee masuala ya kesi yake bali mahusiano na Cheni ambayo ndio lengo hasa la uzi huu.
 
Hapana siyo ya kwenye avatar, niliwachia full body, vijana wakajiumize na "selfie", nyoko zao, ngunga siku hizi wanaita "selfie".
 
Nimeingia katika uchunguzi rasmi juu ya madai ya Salma kuwa huru, nitaleta majibu kama wewe ulivyofanya.

Kwa sasa naomba nisiongelee masuala ya kesi yake bali mahusiano na Cheni ambayo ndio lengo hasa la uzi huu.
Mahusiano ni kitu cha kawaida hicho, mwanamke hana mume na pesa anazo na kijana ana njaa, kibaya ni kuwa Mwanamke wa Kiislam ilitakiwa aolewe na asifanye zinaa na uasherati. Tunafundishwa zinaa inaleta umasikini, na kilichompata ni ushahidi kamili kuwa uasherati na zinaa vinaleta umasikini na ni uchafu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…