Nimeishi sana Tabora, na napajua vizuri tu. Wanawake wengi wa Tabora wanajua sana mapenzi na ni wasafi mno, lakini pamoja na hayo yote wengi wao hawana kipato au kazi za kueleweka kwa hyo maisha yao mengi yanaendeshwa kutokana na kuhudumiwa na mwanaume aliyenaye.....wana uaminifu wa kuwa na mwanaume mmoja sio wasumbufu sana kwenye mapenzi katika kuwapata, na wana adabu sana mbele ya mwanaume. Tatizo lao kuu ni wanajua kung'ang'ania mwanaume haswaa, na kwenye kung'ang'ania huko ni lazima aende kwa Mganga. Na asilimia kubwa ya waganga wa Tabora sio matapeli, akimpa dawa huwa inafanya kazi kweli, na dawa za waganga wa Tabora ni very cheap ziko hata za buku 1 mpaka buku 5.... ndugu yenu katengenezwa na hapo hamumchomoi kirahisi, na mkilazimisha aachane na huyo mwanamke basi ni rahisi kwa huyo mwanaume hata kujiua au kuwapotezea nyie ndugu zenu mazima.....