Jokajeusi
JF-Expert Member
- Jun 1, 2018
- 6,323
- 10,813
Habari wakuu!
Moja kwa moja kwenye mada.
Moja ya wanawake ambao taifa la Israel halitakaa limsahau. Mwanamke ambaye Israel ilichezea kichapo kitakatifu na kudhalilika vibaya mno. Mwanamke mzalendo aliyeiabisha Israel na kuivua nguo ikabaki uchi wa mbuzi mee. Huyu ndiye mwanamke Jasusi wa wakati wote ambaye Taifa la Israel halitaki kumsikia kabisa.
Wengi wanamfahamu, mwanamke wa shoka ambaye wengine pasi na kujua wanamlaumu na kumuona kana kwamba ni msaliti lakini kumbe alikuwa kwenye majukumu ya kijasusi. Na kwa hakika Mwanamke huyu alitekeleza majukumu yake kwa asilimia mia moja.
Delilah ndiye mwanamke Jasusi ambaye mpaka sasa rekodi yake haijavunjwa na mwanamke yeyote. Hakika Delilah anastahili pongezi kwa watu wenye akili na hekima. Ni mwanamke shujaa na mzalendo kwa taifa lake.
Wito wangu kwa wana JF na dunia kwa ujumla kuanzia sasa Delilah asionekane ni msaliti kama tunavyoaminishwa huko makanisani bali tukubali kuwa Delilah alikuwa ni mzalendo kwa taifa lake la Wafilisti kama alivyokuwa Jasusi Malkia Ester kipindi wakiwa chini ya Waashuru.
Delilah Mwanamke Jasusi aliyeitesa Israel.
Karibuni kwa mjadala