Mwanamke Jasusi wa wakati wote aliyeitesa Israel

Moja ya wanawake ambao taifa la Israel halitakaa limsahau. Mwanamke ambaye Israel ilichezea kichapo kitakatifu na kudhalilika vibaya mno. Mwanamke mzalendo aliyeiabisha Israel na kuivua nguo ikabaki uchi wa mbuzi mee. Huyu ndiye mwanamke Jasusi wa wakati wote ambaye Taifa la Israel halitaki kumsikia kabisa.
Ina maana kukamatwa kwa Samsoni kuliidhalilisha na kuiacha uchi Israel? Tuambie kivipi? Na Samson alipojitoa muhanga kwa kuangusha jengo la Wafilisti na kuwauwa wengi ikiwemo Wafalme wao na mungu wa Wafilisti (Sanamu ya Dagoni) huku akiwa kipofu ilikuwa kumdhalilisha nani?
 
Ukweli ni kuwa kipindi Samson anazaliwa, Israel haikuwa na Mfalme. Yeye alizaliwa kama Muamuzi wa kuamua baina ya waisrael na kuwatetea dhidi ya maadui zao. Kitendo cha Kaka Sam kuingia kwenye kumi na nane za Kachero Delilah kuliingiza Israel katika taabu kwa maana baada ya Kaka Sam kutiwa nguvuni taifa la Israel lilikosa mtetezi hali iliyosababisha kuonewa.

Kifo cha Kaka Sam licha ya yeye kulipa kisasi na kufa na adui zake hakiondoi mateso ya Waisrael kwani taifa hilo liliendelea kupokea mateso ya Wafilisti. Muendelezo wa mateso hayo uliendelea mpaka anapokuja Mfalme Sauli alimaarufu kama Fimbo ya Mungu. Lakini Kuzaliwa kwa Daudi ndipo kulimaliza mateso ya Waisrael kutoka kwa mahasimu wao Wafilisti.

Kaka Sam alilipa kisasi chake binafsi na si kisasi cha taifa lake. Ndio maana hata ombi lake kwa Mungu lipo kiubinafsi na si kitaifa. Tunajifunza nini hapa; Ni kuwa kuna watu kwenye jamii wanapaswa waache mambo yao binafsi kwa maslahi ya taifa. Kujiua kwa Samson hakukuondoa mateso ya Waisrael dhidi ya Wafilisti bali kulisuuza moyo wa Sam kwa kulipa kisasi.

Maelezo haya akili yako iamue sasa ni nani alivuliwa nguo katika ngazi ya taifa.
 
Nimekuelewa!
 
Nimekuelewa!

Sawa Mkuu.

Hujiulizi kwa nini kisa hicho kiliandikwa kwenye Bible Mkuu. Mbinu hiyo Israel waliiga na kuitumia kwa Malkia Ester na ikafanya kazi. Hata kitabu cha Tobiti kama sijakosea kinakisa mfano wa hiki
 
Ni kweli! Kwenye biblia kuna Visa kadhaa jinsi wanawake walivyotumika kuokoa taifa (rejea kitabu cha waamuzi kisa cha Debora, Baraka na Mfalme Sisera au Malkia Esta,Modekai na Hamani) na kuangusha wafalme na kuharibu nchi (rejea kisa cha mfalme Ahabu na mkewe Yezebeli) hii inaonesha wanawake wanaweza kuwa chanzo cha kuinuka au kuanguka kwa Taifa.
 
Haswa, sasa njoo kwa Maria Antonete mke wa Mfalme Louis IX kama sijakosea wa Ufaransa
 
Kwa kurejea hayo matukio ya kwenye biblia na mke wa mfalme Louis IX Je unahitimisha ni halali wanawake kupewa fursa sawa na Wanaume (yaani 50/50) katika ngazi zote maana wameonekana ni chanzo cha kuinuka na kuanguka kwa Taifa?
 
Binafsi hili nalipinga ikibidi kifo
 
Hakuna mwanamke ambae aliitikisa Israel kama YEZEBELI, hata Nabii Eliya alimkimbia ila kwa upanga wa YEHU Yezebeli alianguka na maiti yake ililiwa na kungura shambani.
 
Back
Top Bottom