Mwanamke kumwambia ukweli Mtoto sio kumpa Sumu!

Mwanamke kumwambia ukweli Mtoto sio kumpa Sumu!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
MWANAMKE KUMWAMBIA MTOTO UKWELI SIO KUMPA SUMU!

Anaandika, Robert Heriel

Kuna kasumba mbaya Sana iliyoota mizizi ndani ya jamii kuwa Wanawake wanawapa sumu watoto wao ati wawachukie Baba zao. Jambo ambalo Kwa kiwango kikubwa ni uongo mkubwa.

Sio dhambi wala kosa Mama kumwambia m/watoto wake ukweli kuhusu Baba Yao. Sio kosa na wala sio sumu Kama wengi wanavyodai.

Hivi Kama Baba hutoi matumizi ya mtoto wako unategemea mama yake amuambie mtoto wako kuwa unatoa pesa, hivi unaakili kweli?

Kama haumjali mtoto wako unategemea Mama yake amuambieje, kuwa unamjali sio, CHIZI kweli wewe! Labda huyo Mama awe na akili za kijinga na kuendekeza ujingaujinga. Kwamba amfundishe mtoto unafiki/uongo kisa kuogopa atakuchukia?

Embu fikiria Scenario Kama hizi;

I. Mtoto kaenda shule Hana daftari au nguo za Shule zimechakaa, au kafukuzwa ada au hajala mchana, unataka Mama asimuambie Mtoto sababu ya yeye kuwa hivyo? Baba ni Provider/mtoa Huduma, mlinzi wa familia, mfariji, na kiongozi.

Sio jukumu la mama kumtunza Mtoto, sio jukumu lake, jukumu la kutunza watoto nila Baba.
Hivyo mama lazima amuambie mtoto kuwa Baba yako hakununulii daftari, nguo, na chakula ikiwa ni kweli hufanyi hivyo.

Mtoto lazima atataka kujua Kwa nini Baba hafanyi majukumu yake, yaani hata Mama asipomwambia sababu, Jambo la Kwanza litakalokuja Kwa mtoto ni kuwa Baba hampendi. Hiyo ndio sababu Namba moja mtoto atakayokuja nayo akilini.

Kuna Sisi wanaume wenye tabia ya kunyanyasa na Kupiga wake zetu bila sababu za maana, kisa ni mwanamke unapiga tuu, kisa ni mwanamke unamuumiza kihisia pasipo kujali lolote kisa wewe ni Baba. Huo ni upumbavu na unaofanywa na wanaume wapumbavu!

Jukumu Namba moja la Baba ni kuipenda Familia yake(Upendo),
Umpige Mke wako au mzazi mwenzako mbele ya watoto alafu hutaki mke asikusemelee Kwa watoto kuwa unamnyanyasa? Ati unaiita sumu! Hivi unajua maana ya sumu kweli?

Sumu ni Uongo.
Jambo likishakuwa kweli haliwezi kuwa sumu.

Oooh! Wanawake wanawapa sumu watoto, wanaume wenzangu tuache tabia za ajabu ajabu.
Watoto sio wajinga, watoto wanaakili, watoto ni Binadamu wanajua kipi ni chema kipi ni Kibaya.
Mtoto hata asipoambiwa anaelewa kuwa Mama ndio kakosea, Baba ndiye kakosea. Watoto wanaakili.

Sumu ni Ile ambayo Baba unahudumia watoto wako Kwa upendo lakini Mama anaongea uongo kuwa hautoi Huduma, sumu ni Ile unailinda familia yako iende katika njia sahihi alafu Mama anaongea uongo Kwa kufanya maasi yake.

Mfano, Baba unakuwa mkali watoto wasitoke toke nje hovyo au wasichelewe Kurudi NYUMBANI kabla ya jua kuzama, alafu mama apindishe kanuni hiyo Kwa kukupaka Baba matope kuwa huwapendi, hiyo ni sumu.
Hata hivyo Watoto wanaakili wanajua Baba yupo sahihi sema Kwa vile Kwa wakati ule wañatamani mambo ya utoto au ujana watakuwa hawapendi unavyowaambia Ila wanakuelewa.

Kutumia neno "sumu" isiwe kichaka Kwa Sisi wanaume kukitumia kujificha katika kujitetea katika makosa tuliyoyafanya. Ni ujinga, upumbavu, na unakuwa Baba jinga lisilojielewa.
Ni vizuri Baba kama ulikosea kuomba tuu Radhi kuwa ni kweli ulikosea labda ujana au Shetani au maisha yamekufunza Kwa njia ngumu na sio utafute mtu wa kumpa lawama Kwa makosa yako.

Ni kweli Sisi wanaume tunapenda Wanawake wengi Hali iñayopelekea baadhi ya matokeo mabaya kama hayo ya kushindwa kutoa Huduma Kwa wake/wazazi tuliozaa nao. Lakini isitufanye tukashindwa kuukubali ukweli na kuomba radhi kuwa tumekosea.

Watoto wetu nao watapitia tuliyoyapitia lazima tuwafundishe Kwa vitendo yaani tuwajibike ili iwe funzo kwetu na kwao.
Tusione shida kuwajibika Kwa makosa yetu. Huo ni ushetani, yaani tunatafuta sababu za kuhalalisha dhambi na makosa yetu.

i. Wanawake ni watu wa kutafuta pakulilia, asipomlilia mumewe basi atamlilia mwanaye hiyo ni saikolojia ya wanawake. ii. Wanawake ni watu wakushtaki, asiposhtaki kwako Kama mumewe basi atashtaki Kwa watoto wako.

iii. Wanawake ni watu wa kutafuta kupendwa. Usipowapa upendo watatafuta upendo Kwa watoto wao.

iv. Wanawake ni viumbe dhaifu visivyopenda kulaumiwa. Hata kama vinamakosa.
Wanaume tusiwe Kama wanawake Kama tunamakosa Kwa nini tuone shida kupokea lawama ya makosa yetu? Huo ni udhaifu.
Mwanaume kamili anayejitambua akikosea haoni shida kukiri kosa na kuomba Msamaha

v. Wanawake ni viumbe wenye chuki ambao wanatafuta kufundishwa upendo na wanaume. Usipokuwa mwalimu mzuri wa upendo Kwa mwanamke basi tegemea chuki zake zitafanya kazi.
Wanawake ukiwapa upendo wakakupenda hata kama utashindwa Kuwatunza wao na watoto wao, watabaki kukupenda na kujivunia wewe.

Lakini ukiwa mtu wa majivuno, kiburi na jeuri, hata ungewapa pesa na Kuwatunza bado wasingehesabu ni chochote kwao na watoto wao.

Sio kwamba Wanawake hawawezi Kulea watoto wao peke Yao, mbona wengi wanafanya hivyo, iwe Kwa shughuli halali au haramu mbona hata Sisi wanaume tunfanya shughuli halali au haramu kuhakikisha familia zetu zinaishi vizuri. Kitu wanachotaka wanawake ni Upendo Kwa wanaume.

Ni hatari kuishi au kuingia kwenye mahusiano na Mwanamke aliyenyimwa upendo. Mara nyingi huwa aggressive, roho mbaya na huwa Shetani.

Wanawake WA siku hizi wapo walivyo kwa kukosa upendo kutoka kwetu wanaume.
Ingawaje tunawalaumu lakini ukiangalia kiini kikubwa cha wao kuwa hivi walivyo ni Sisi wanaume wenyewe.

Niliwahi andika; Usimuonee huruma Mwanamke soma hapa👉👉Usimuonee huruma Mwanamke

Na hii ni kutokana na kuwa mwanamke hahitaji huruma isipokuwa UPENDO.
Uwe naye Kwa sababu unampenda sio Kwa sababu unamvumilia. Hiyo lazima itakusumbua tuu Dunia ingalipo.

Ingawaje wapo wanawake walinishutumu na kunitusi wala sitowalaumu Kwa sababu kuwa na akili ndogo sio kosa Lao kwani ndivyo walivyozaliwa.

Kila Jambo Lina misingi yake.

Sumu inahusu amri isemayo; usimshuhudie jirani yako Uongo. Hiyo ndio sumu.
Lakini kama mwanamke au mwanaume anamuambia mtoto wake ukweli hiyo sio sumu. Ila anajaribu kumueleza mwanaye kuwa Baba yake hawajibiki.
Kimsingi mama anapaswa amuombe mtoto Msamaha Kwa kumchagulia Baba bogus.

Hata hivyo Taikon nawashauri wanawake ambao mpo na wanaume wanaoonyesha kujitahidi kutunza watoto wao hata Kwa kidogo walichonacho muendelee kuwaombea na kuwavumilia.
Na Wale wenye tabia za tamaa za kijingajinga kusumbua wanaume na kutaka gharama za juu zisizoendana na uchumi wa Mwanaume dawa yenu ni kuwazingua to the maximum, watoto wanajua ukweli. Na huo ushahidi ninao.

Mwisho, tuache uzinzi, tumche Mungu Kupunguza hizi kadhia zitokanazo na mambo ya uzinzi. Tupendane Kama wanandoa, tukiamua kuoa au kuolewa tufanye kweli. Mambo ya kuachana sio mazuri na matokeo yake ndio kama haya.

Pili wanawake mkubali kuolewa wake wengi. Mambo ya kukutesa na Mke mmoja wengine hatuwezi. Na Hilo sio suala la Siri hii itaepusha michepuko.
Tamaduni za kiafrika hatuna kitu kinaitwa MICHEPUKO isipokuwa tunakitu inaitwa NDOA ZA MITALA.
Tuoe hata wake ishirini Sawa tuu ilimradi tunauwezo wa kumudu mahitaji.

Ni Yule Shahidi

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Mzee baba unapoint ilaaaaa........ngoja niishie hapo kwanza swali la nyongeza
Una mke?
 
Kiufupi mwanaume ukiona maisha huna usitie mimba condom zipo ukishindwa sana nenda kahasiwe usije kusumbua watu
 
Back
Top Bottom