Asante AD for this post. Mie langu moja tu, hivi, kutongozwa ni kitu cha kidini au? Yaani , kinakubalika kidini ?==> na hence muongozo kuwa ni lazima itoke kwa wanaume tu?
Au ni a generic term ambayo inaweza kutoka hata kwa wanawake?
Hofu yangu kubwa ni kuwa , kama ni jambo linalotakiwa kutoka upande mmoja, tiyari lina set precedence na mazingira yanayompa superiority m-gender mmoja dhidi ya mwingine.
Na hasa tukizingatia kuwa wanaume wana list yao ya 'wanavyovipenda' au kuvitamani kwa jenda hii ingine na hali kadhalika, wanawake huwa wana yao, na bado kuna vigezo-changia-kote i.e vinavyokubalika na ku feature katika list zote mbili.
Mfano, mwanaume atavutwa na umbile na sura ( asilimia kubwa, sijasema wote, kabla hamjanitovoga na bisbisi machoni), atapenda labda mwenye haya kidogo , though wengine wanapenda macho makavu, wengine wanapenda mwanamke independent ila eti awe submissive ( hapo inakuwaga ngumu kubalansisha ikwesheni ila ndo hivyo)etc.
Wanawake nao hupenda ( walio wengi) security in a man - mara nyingi hili hupimwa na juhudi ya kazi , mara nyingine pesa , na historia ya mafanikio maana hiyo pia itamu assure maisha bora ( sio wote jamani); uaminifu ( kigezo kigumu kabisa), un-mkatili ( sijui ndio mpole, au sijui nini but antonym ya mkatili- hapa nakumbuka lile tangazo la kwenye luninga la mwanaume ambaye akiingia home, hadi watoto wanajificha katika makapu) .
Lakini pia kuna vile vigezo changia kote kama uaminifu na ukweli ambavyo havina jinsia.
Na hapa natoa heshima ( pay respect, lol) to ukweli kuwa sio tongoza zote zitaishia katika ndoa. Najua zingine ni patapotea lakini sijataka kuketi ( ku base) katika utongozaji wa kihuni tu wa tamaa ( one night stands), ila zaidi katika ule utaoleta mahusiano thabiti.
Naomba kuwasilisha