Ewaaaa!hahaha.... Si nilikwambia kua huyo Fatma alikua anataka? Alafu shem si kuna ile ambayo wanaume huangalia kama atapata hapo anapo papenda ama lah! Akiona kua chances are slim wala hata haangaiki kabisa! lol
Nimekuelewa Big SISY,na ni kweli huwa wanajipanga hakurupuki kwa kuogopa vya mbavu,Kid sis mimi naamini saana the way wajipotray ndio hasa the way wachukuliwa.... Take note kama wewe watongozwa kila siku ya Mungu then kuna tatizo ambalo laweza kua ni wewe mwenyewe (maybe uvaaji), mazingira uliopo na mazoea yako dhidi ya walo kuzunguka. Naamini kua mwanamke ukijiheshimu na waonekana wajiheshim wale walo kuzunguka ikitokea kuna anae taka kukutongoza lazima ajipange kwanza.... na kama wanaokutongoza wajipanga kwanza haiwezekani kua utatongozwa ile mara kwa mara.... For watakuepo wale watakutamani but wataridhia kula kwa macho....
Umenipata dear?
Marahabaaaa.......... Hebu nambie, ulikuwa wapi siku zote hizi?:violin:
Orayt.... pole kwa matatizo. Ila hayahusiani na mitongozo wala mafumanizi, right?Ni matatizo tu ya hapa na pale ya kidunia babu lakini namshukuru Mungu niko salama............oooppsss sorry ADI kwa kuwa off topik......babu huyo
Kuna rafiki yangu amewahi kuniambia mapenzi ni sanaa (art) kama sanaa nyingine ingawa hii hufanywa na watu wengi zaidi. Sasa kwa hawa wasotongozwa/ -tongozeka AD my sis it is their very own duty to learn the theories na kuchagua paradigm ya kufanyia kazi and be cautious upon entering the volatile practical ground
Hivi kwani lazima kutongozwa bana? Mzukie mwenyewe tu, khaa mbona mbwembwe nyingi sana!!
AD,
Kumbe msipotongozwa nalo ni tatizo hata kama mnajua jibu litakuwa yes or no depending on many different issues?
Orayt.... pole kwa matatizo. Ila hayahusiani na mitongozo wala mafumanizi, right?
Sori ADI fo zis ofutopiki, (Source: Kbd)
Duhhhh
Mi nimesikia na nimeona wasichana/wanawake wanatongozwa hadi usumbufu.
Sijawahi sikia mwanamke ambae hajawahi tongozwa kabisa ...
Bi mkubwa,
Habari yako binafsi kwanza....
Huyo mwanamke ambaye hatongozwi huyo tena ni kiboko ua labda hajui matumizi ya mtandao.....
Maana siku hizi unatongozwa na mtu hata hamjuani matongozo meeengi mpaka uanshangaa huyu mtu ananijuaje mimi kama ni jini je???
JF unatongozwa, FB unatongozwa, Twita unatongozwa nk basi ni vurugu tupu
Orayt....Ohhh nooo! Hayahusiani kabisa. Asante, no mo off topik pls.
Lol. . mapenzi na mahusiano dah! mapenzi yanarun dunia! sababu nyingi zinasababishwa na infriority complex ya kaka zetu! mwanamke ajifanyishe wa chini ili atongozwe? yani ingekuwa kwa mila zetu mwanamke unaweza ukaanza ingekuwa bora sana jamani!
wengine nasikia huwa wanaoga mtoni saa kumi usiku maji ya bariiiiiidi kama barafu ile watongozwe
Fidel80 nadhani anajua vizuri
Lol. . mapenzi na mahusiano dah! mapenzi yanarun dunia! sababu nyingi zinasababishwa na infriority complex ya kaka zetu! mwanamke ajifanyishe wa chini ili atongozwe? yani ingekuwa kwa mila zetu mwanamke unaweza ukaanza ingekuwa bora sana jamani!
Hii sredi bado inaendelea au tuianze uchakachuzi?
Sori ADI for zis schupid ofutopiki lakini inayodizevu ka-LIKE kamoja.
:iamwithstupid::iamwithstupid:
Habari zako mamii?
Daaah hata sina la kusema, ila ukweli kuna matongozo mengine mpaka mwenyewe unasema hiki nini! Kunalijamaa limoja lilinitongoza kwa sms akidai alinishindwa kuniface yaani niliona aliniudhi sana na alinifanya nijiulize mara 10 10 kwa nini mimi? Niliona kama amenidharau sana.
Lakini mwisho wa siku............"Never get Angry. Never make a Threat. Reason with people"
Mwanaume kumtongoza mke wa mtu sababu ni nyingi saana na hilo ambalo umesema ni moja wapo. But I do know for a FACT kua mwanaume anaweza penda mke wa mtu na asimtongoze tokana na heshima alo nayo juu yake. For mtu kua mke wa mtu haimaanishi kua wanaume wengine hawawezi muona na ku appreciate her beauty. Hata hivo kuna mwingine akimpenda mke wa mtu anaweza akamtongoza na akamaanisha na sio sababu ya dharau, thou in one in 50. Na pia mke wa mtu hutongozwa tokana na yeye the way alivo ji potray.... Take note: wanaume wengi ambao hutongoza mke wa mtu hufanya hivo kwa kujaribu na si kumaanisha hasa, ila ikitokea kakubali then ratiba itafuata kama kawaida.....
Ewaaaa!
Hakuna kitu mwanaume anachoogopa kama kupigwa kibuti. Ndo maana huwa haingizi neno kama mtongozwaji mwenyewe anaonekana katia pamba sikioni....
Mwanaume anayeingia kichwa kichwa afu akalimwa kibuti basi huyo SI MWANAUME BANA!
Nimekuelewa Big SISY,na ni kweli huwa wanajipanga hakurupuki kwa kuogopa vya mbavu,
Ila hawa wanaume bana hata hawaeleweki unakuta hata umeongozana na mdada kavaa ile km kamkusudia mtu,
Cha kushangaza ww ambae umejivalia zako kawaida ndio unapata usumbufu yule mwezio wakishachekean pale mkapita ndio basi lkn ww mwingine ndio lijamaa linaenda kujikoki mistari anakuibukia upya!!!!
Labda hapa tuseme kuna aina za tongozo,means kuna zile za serious na zile za kupigiana makele bara baran kutokana na uvaaji wa mtu,mie hizo za makelele bara baran sikutan nazo kwa namna ya uvaaji wangu,
Mie hapa naiongelea ile ya serious ambayo haihusiani labda na kumtega mtu kimavaz,isitoshe unajikuta unatokewa hata na watu wanaokufahamu ww umeolewa au uko kwenye relation!!!
Hehehehe.... kile kibuti chako cha staki nataka?.... Hata mi nlijua tu ulikuwa unakataa kimagumashi...Shem hapo in blue sio yategemea kweli? mbona your hommie enzi hizo alinitongoza mara 3 nikawa nampa za uso lakini hakukata tamaa mara ya 4 nikaingia line.... :redface: Na I know you know as I know kua ni Mwanaume hasa! lol
Asante AD for this post. Mie langu moja tu, hivi, kutongozwa ni kitu cha kidini au? Yaani , kinakubalika kidini ?==> na hence muongozo kuwa ni lazima itoke kwa wanaume tu?
Au ni a generic term ambayo inaweza kutoka hata kwa wanawake?
Hofu yangu kubwa ni kuwa , kama ni jambo linalotakiwa kutoka upande mmoja, tiyari lina set precedence na mazingira yanayompa superiority m-gender mmoja dhidi ya mwingine.
Na hasa tukizingatia kuwa wanaume wana list yao ya 'wanavyovipenda' au kuvitamani kwa jenda hii ingine na hali kadhalika, wanawake huwa wana yao, na bado kuna vigezo-changia-kote i.e vinavyokubalika na ku feature katika list zote mbili.
Mfano, mwanaume atavutwa na umbile na sura ( asilimia kubwa, sijasema wote, kabla hamjanitovoga na bisbisi machoni), atapenda labda mwenye haya kidogo , though wengine wanapenda macho makavu, wengine wanapenda mwanamke independent ila eti awe submissive ( hapo inakuwaga ngumu kubalansisha ikwesheni ila ndo hivyo)etc.
Wanawake nao hupenda ( walio wengi) security in a man - mara nyingi hili hupimwa na juhudi ya kazi , mara nyingine pesa , na historia ya mafanikio maana hiyo pia itamu assure maisha bora ( sio wote jamani); uaminifu ( kigezo kigumu kabisa), un-mkatili ( sijui ndio mpole, au sijui nini but antonym ya mkatili- hapa nakumbuka lile tangazo la kwenye luninga la mwanaume ambaye akiingia home, hadi watoto wanajificha katika makapu) .
Lakini pia kuna vile vigezo changia kote kama uaminifu na ukweli ambavyo havina jinsia.
Na hapa natoa heshima ( pay respect, lol) to ukweli kuwa sio tongoza zote zitaishia katika ndoa. Najua zingine ni patapotea lakini sijataka kuketi ( ku base) katika utongozaji wa kihuni tu wa tamaa ( one night stands), ila zaidi katika ule utaoleta mahusiano thabiti.
Naomba kuwasilisha
Miaka kadhaa iliyopita, niliwahi kuishi mahala/mkoa fulani nikiwa kijana mdogo tu napata miaka 23 hivi na kwa kazi niliyokuwa nafanya, nilipewa nyumba ya kuishi kubwa tu, mwanzo tukishare na wenzangu wawili lakini baadae nikabakia peke yangu. Sasa kuna weekend moja akaja dada mmoja nyumbani kwangu (sikuwa nimemwalika! lakini ni dada ambaye nilikuwa namfahamu kidogo...ni mtu ambaye hata salamu ni mpaka mpishane karibu kabisa!)..ni mdada mrembo tu lakini kwa kumtizama tu alikuwa ni dada aliyenizi umri - ingawa nilikuwa na reserve shikamoo yangu (baadae katika stori niligundua anaishi kwa wazazi wake, hajaolewa, kanizidi miaka 6 na pia tayari ana mtoto mmoja!)....nikamkaribisha, nikampa muda wangu akasema kilichomleta, nikamsaidia alichokuwa anataka, na baada ya hapo hakutaka kuaga hivyo tukaendela kapiga stori za hapa na pale na muda wake wa kuondoka/au tuseme jua ndio lilikuwa limekuchwa akawa anaaga. Note muda wote huo, sikumtongoza wala kuonesha dalili kama nina nia ya kumtongoza (btw, nilikuwa sipendi ku date wadada walionizi umri sana) ingawa pia sikutaka kuashiria kuwa ningependa aondoke! Kwa kifupi zilikuwa ni stori za kawaida tu ambazo ningeweza kupiga na mwanamke yoyote au hata mwanaume mwenzangu. Na katika muda huo wa kukaa naye tulikuwa tayari tumetengeneza rapport ya aina fulani na hivyo ilikuwa rahisi kufanya 'vi' mzaha/au utani (lightly) kidogo. So wakati anaaga ilikuwa tayari kuna ka giza kameanza kuingia lakini alipokuwa anaaka sio mbali sana kutoka kwangua (some 10mins walk), so maagano yakwa hivi:
Mgeni: Nashukuru kwa msaada wako, Mungu akijalia tutaonana siku ingine.
SMU: Asante sana. Nilifikiri leo unalala hapa!?(ofcourse kwa mzaha/utani tu)
Mgeni: Kwani una kitanda cha wageni? (huku anacheka na kaaibu kwa mbaali!) - alikuwa anajuwa nilikuwa naishi na wenzangu na kwa muda huo wameondoka na vitu vyao (so vyumba vipo almost empty).
SMU: Nyumba mbona kubwa tu hii? Kitanda si nakupisha hata cha kwangu tu au kama vipi tunalala mzungu wa nne!(nadhani hapa ndipo nilivuka mpaka, so far, wa utani/mzaha na huyu dada - yeye alidhani nipo serious!)
Wote: Kicheko!.....kwi kwi kwi!
Mgeni: Nitalala siku nyingine...leo sijaaga nyumbani!
[SMU: Nimeingiwa na hofu kuwa sasa nimelikoroga, of course siwezi kumwambia asije tena!]
SMU: Wape salamu nyumbani
Mgeni: Nitazifikisha. Na wewe karibu nyumbani kwetu.
SMU: Asante (sikumsindikiza zaidi ya nje ya compund ya nyumba yangu!)
Baada ya wiki na nusu hivi, tukakutana na "Mgeni" katika mizunguko ya kazi. Tukasalimiana now kwa sababu ya kuzoeana tukasalimiana kwa karibu zaidi na kuulizana yaliyojiri tangu tulipoachana (kipindi hicho hakukuwa na mobile phones kama sasa maeneo mengi!). Wakati tunaagana Mgeni akasema atakuja nyumbani kwangu jumamosi inayofuata (siku hiyo ilikuwa jtano) - hakusema anakuja kwa shida gani na mimi sikutaka kumuuliza...nilikuja kufahamu baadae kuwa alikuwa anakuja kutimiza ahadi yake ("nitalala siku nyingine"!).
Dah..stori inakuwa ndefu...lakini to cut it short, alikuja hiyo jmosi. Kuna tofauti niliona...siku ya kwanza alipokuja alichagua kukaa kwenye kochi la single lakini mara hii alichagua kukaa lile la double:hand:!!!! na baade aliishia 'kulala' kwenye kitanda changu (...mzungu wa nne or otherwise...hili hatukupata muda wa kujadili tena!)
Kwa mwanamke kutongozwa hakukwepeki hata ukijipiga kininja, atakuja ustadhi na kibaragashia atakutongoza, ukijivika sura ya kilokole, pia ataibuka mjuaji ajifanye anakufundisha neno mwisho wa siku anamwaga sera.
Kuna watu wao kazi ni kudeal na wake za watu, na wana kimsemo eti mke wa mtu hana gharama.
Kwa wanawake kutongozwa ni jambo la kawaida (sunnah) kama mnavyosema, tatizo ni kukubali kila unapotongozwa mmh hapo ndio noma kumkubalia kila mwanamme anaekutongoza.
Kingine kwa mwanamke ni type ya huyo mtongozaji kama anaendana na ww, kama utaona wanakutongoza hamuendani type hapo pia kuna question mark......!
tatizo leo j3 mikazi kibao hata kujiachia katika huu uzi inakuwa tabu.