MWANAMKE MWENYE MAKELELE
Tarehe 9/10/2021 nipo stendi ya mabasi Iringa, nimekaa karibu na wakatisha tiketi za mabasi waliokuwa wakifanya mazungumzo yao, na katika mazungumzo yale ninawasikia wakijibiza. "USIRINGE WEWE SI USHUKURU NDOA YAKO HAINA MAKELELE, MI MWENYEWE HAPA NI MNENE, BASI TUU KWA VILE MKE WANGU ANA KELELE NDIO MAANA NIMEKONDA HIVI”
Maongezi yale na majibizano ya wale watu yakaingia haswaa ndani ya moyo wangu, na yakanifanya kutafakari sana, MWANAMKE MWENYE MAKELELE, NDOA YENYE MAKELELE, ni nini hiki? Kwanini mwanaume huyu ajione kwamba afya yake imedhoofu kwasababu mke wake ana kelele?, nikawaza zaidi kwanini suala la kelele za mwanamke ni kero sana kwa wanaume?
Kile nilichokisikia kutoka kwa wanaume wale kikanipa kurudisha fikra zangu nyuma na kutafakari baadhi ya wanaume ambao nimekuwa nikihusiana nao kuanzia na mume wangu, kaka zangu, marafiki na ndugu wengine, nikagundua karibu wanaume wote hawa hawapendi kelele
Nikajiuliza zaidi, kelele ni nini mbele ya macho ya wanaume? Hii ikanikumbusha kile neno la MUNGU linasema katika kitabu cha MITHALI 21:9, 19 na MITHALI 25:24, hebu soma na mimi maandiko hayo hapa chini;
MITHALI 21:9, 19
9 Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi
19 Ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika; Kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi.
MITHALI 25:24
24 Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi.
Ukisoma maandiko hayo katika tafsiri nyingine hayo maneno mwanamke mgomvi na mchokozi yametafsiriwa kama mwanamke msumbufu, mwenye kelele na mwanamke mbishi
Nyika ni mahali ambapo ni pakame, hapana maji, pana joto kali, hapana kivuli kwasababu hapana miti, na kwasababu ni mahali pakame, basi hata uzalishaji huwa ni mgumu.
Dari pia ni sehemu pweke, ni sehemu ya maficho na ni sehemu yenye giza na isiyo na uzuri kwa mtu kuishi huko.
Sasa basi, Neno la Mungu linataja maeneo haya mawili nyikani na darini kuwa ni afadhari mtu akae huko kuliko kukaa na mwanamke mgomvi, mwanamke mchokozi na mwanamke msumbufu, hii ni hatari.
Hebu tutafakari pamoja hapa yaani eti bora kwenda kukaa nyikani au darini kuliko kukaa na mwanamke?
Kwani wanawake tuna kasoro gani hadi tuogopwe kiasi hiki?
Tunatisha kwa kiwango gani hadi watu wawe radhi kwenda kuishi katika nchi kame kuliko kuishi na sisi?
Haya ni maswali ambayo kila mwanamke anapaswa kujiuliza, na kuona ni kwa kiwango gani mwanamke anapaswa kuwa makini.
Ugomvi, uchokozi na usumbufu wa mwanamke ndio unaoogopwa, unaudhi na ni kero kiasi ambacho watu huona ni bora wakakae peke yao nyikani, au darini, sehemu ya upweke kuliko kukaa na wanawake.
Sauti kali na kelele katika maongezi yetu ya kila siku inatufanya kuwa wanawake wagomvi na wakorofi, hii ni hatari.
Sauti kali, sauti yenye kelele ni sauti ya mwanamke mgomvi na mkorofi.
Kelele zinakera, kelele zinaumiza, kelele zinavuruga utaratibu, kelele zinaondoa amani
Kelele ni ishara ya ukaidi – MITHALI 7:11
Kelele ni ishara ya fujo
Makelele ya mwanamke yanaweza kuharibu na kuvuruga afya ya mwanaume kabisaaa
Ni maombi yangu kwamba MUNGU atupe neema sana kama wanawake, yapo mambo mengi ambayo tunatakiwa kuyatilia maanani ili tuweze kuwa wanawake bora, wakati mwingine mambo mengine yanaonekana ni kama sio rahisi, mengine yanaweza onekana ni kama ndivyo mtu alivyozaliwa, lakini maadamu tunaye MUNGU muumbaji wetu, tukiwa tayari kubadilika, tukajinyenyekeza kwake anaweza kutufanya kuwa watu bora zaidi
Mdomo wa mwanamke unapaswa kuepuka Mzozo/Ubishi, Malalamiko, Upinzani/Upingaji, Lugha za mashambulizi na Sauti kali/kelele. Badala yake kila mwanamke anawajibika kujifunza namna anapaswa kuzuia kinywa chake kisinene mabaya, kusoma mazingira ya nini aongee na kwa wakati gani, lakini Zaidi sana kumuomba MUNGU aweke mlinzi na mngojezi katika kinywa chake, mlinzi atakayemsaidia kunena mema na si mabaya.
MITHALI 9:13
Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu
©️Cecilia Charles
Fb: Cecy de Charles
Instagram: Cecydecharles