Mwanamke mpumbavu huivunja ndoa yake mwenyewe

Mwanamke mpumbavu huivunja ndoa yake mwenyewe

mapipando

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Posts
2,922
Reaction score
3,559
Iko hivi,

Kuna jamaa ni jirani yangu anapiga mishe kwenye duka la wachina hapo gerezani, wanauza aina mbalimbali za vyuma na mabati ya mageti.

Inavyoonekana jamaa ni anapiga hela ndefu kinyama kwa hao Wachina maana nyumba yake ameiboresha kwa kiwango cha juu sana tangu alipoanza kufanya nao kazi hawa jamaa. Jamaa sasa hivi ana kitambi sio mchezo unaambiwa.

Kutokana na mshikaji kuwa na kipato cha kutosha aliamua kumfungulia mkewe biashara ya nguo za kike na urembo pale Tandika Plaza na akawa analipa kodi ya fremu na kuendelea kutoa pesa za matumizi ya nyumbani kama kawaida. Jamaa alitegemea baada ya muda duka lingezidi kukua kwasababu mkewe hakuwa akilipa gharama zozote zile lakini waaapi.

Jamaa akaanza kufuatilia mwenendo wa mkewe na kugundua anatumia kiasi kikubwa kuhonga vibwana vidogo dogo ili vikampe show ya kibabe (yawezekana jamaa na kile kitambi amekuwa ni mzee wa kimoko chaliii)

Baada ya kugundua hivyo ikawa ugomvi mkubwa na jamaa akaacha kulipia frem, akapeleka watoto boarding na kuacha kutoa hela ya kula, wife kuona vile akaamua kumpeleka jamaa kwenye dawati la jinsia, Jamaa akawaambia sasa hivi anatafuta hela kwa ajili ya watoto wake na mkewe atafute hela kwa ajili ya mabwana zake.

Na jana tu watu wa vikoba walienda kwake kumfilisi maana anadaiwa 1.5M ila hawakukuta mtu.

Na huko Tandika kwenye frem sijui anadaiwa kiasi gani shubaamit zake.

Ujumbe: Mwanamke mpumbavu huivunja ndoa yake mwenyewe.
 
Binadamu mnasikitisha sana. Unasema jamaa anapiga hela kwa wachina, wakati inawezekana kabisa kwamba yeye badala ya kupeleka hela zake kwa malaya na pombe, anaipeleka kwenye maendeleo. Binadamu ni kazi sana.
 
Mkuu, ulichokileta hapa hakikuhusu, ni heri ukatulia na ikawa siri yako mwenyewe kuliko kuwasemea hapa. Je, unafaidika na kitu gani kufanya ivyo!
 
Stori Muruwaa sana na inafundisha Wanawake wajifunze kuwa Mwanamume hawazi kutoa Dozi ile ile wakati yu kijana mpaka anazeeka mwili hua unaanza kuzeeka taratibu.
Sio kweli.....
ukweli ni kwamba huwezi piga kitu kile kile...
siku zote kwa speed ile ile....
 
Mkuu, ulichokileta hapa hakikuhusu, ni heri ukatulia na ikawa siri yako mwenyewe kuliko kuwasemea hapa. Je, unafaidika na kitu gani kufanya ivyo!
Na wewe ungebaki kimya pengine ingekuwa bora,umefaidika na kitu gani kuniambia hivyo?
 
Mfungulie biashara ye anakua msimamizi tu ila biashara inakua ya familia. Mahesabu pia na wewe unayakagua, hiyo ya kumpa mtu mtaji wa mbei mbaya eti aendeshe biashara ilhali hujui kama anaweza kufanya biashara au lah ni kumuonea tu, lazima aone ni hela nyingi atatumia hovyo na kupata ushauri wa mashosti mwisho uje kumlaumu bure.
 
Back
Top Bottom