1. Tuwafundishe na ombaomba wetu wanaojimudu kiasi fulani kimaumbile wasiwagande sana wengine kwa kuwafanya kitegauchumi chao ilhali wanaweza kabisa kujitafutia kipato halali kwa juhudi na hali zao za ulemavu.
2. Wale wanaowatumia walemavu kama chuma-ulete, jehanamu inawahusu.
3. Walemavu wanaowanyanyasa watoto na wanafamilia, ndugu, jamaa, na marafiki kuwatembeza kila mahali ili kuombaomba, huku wangeweza kutulia mahali na kufanya kazi fulani ya kipato kulingana na ulemavu na pia uwezo wao, wanapaswa kuelimishwa kubadili fikra na mtazamo wao.
4. Walemavu wasidhani kwamba wanawadai watu ^wazima^ eti tu kwa kuwa wao ni walemavu.
#Disability Is Not Inability