Mwanamke ninayeona anafaa kuwa mke hakubaliki mbele za watu, ninayemtilia shaka ndiye naambiwa anafaa

Mwanamke ninayeona anafaa kuwa mke hakubaliki mbele za watu, ninayemtilia shaka ndiye naambiwa anafaa

Habari, JF ni sehemu sahihi ya majibu sahihi.

Nipo kwenye hatua za mwisho kufanya maamuzi ya kupata mama watoto. Wapo mabinti wawili imekuwa ni mchuano mkubwa wa kupata selection.

Yupo mmoja yeye kila ninapomuonyesha mbele ya watu wangu wa karibu wanasema huyu ndio sahihi kuwa mke, kwangu mimi kwenye machaguo yangu kila nikiselect naona asiepewa nafasi ya kukubalika mbele za watu ndio anafit.

Hofu kubwa je huwenda macho yangu yamefunikwa na ukungu wa upendo mpaka kutokujua palipo sahihi ikanipelekea kukosea na kuharibu maisha yangu na kupata majutio makubwa.

Nimebaki njia panda...je, kwa maoni yako kwa maelezo yangu ni wapi palipokuwa sahihi?

Namalizia kwa kusema kosea kujenga ila usikosee kuoa..
Unaoa ili uwafurahishe watu, au unaoa mke atakaekuvumilia kwa kila hali?
 
Wanaosema hafai wanatoa sababu gani? Angalia kama zina mashiko vinginevyo fuata moyo wako usije ukalaumu watu siku za mbeleni
 
Above all, Tupe sifa za wanawake wote wawili.
 
Sikiliza moyo wako usisikilize maneno ya watu mwisho wa siku maisha ni yako na mke wako na si vinginevyo.
 
Ngoja nikupe uchawi kidogo tafuta kioo kidogo weka chini ya mto lala usiku yule utakaemuota kwenye ndoto ndie chagua sahihi Fanya hii mpaka utakapoona majibu
 
Njia hii ilinipa jibu sahihi yule niliyekuwa namdhania kumbe sio nadhani saizi ningekuwa najuta
 
Habari, JF ni sehemu sahihi ya majibu sahihi.

Nipo kwenye hatua za mwisho kufanya maamuzi ya kupata mama watoto. Wapo mabinti wawili imekuwa ni mchuano mkubwa wa kupata selection.

Yupo mmoja yeye kila ninapomuonyesha mbele ya watu wangu wa karibu wanasema huyu ndio sahihi kuwa mke, kwangu mimi kwenye machaguo yangu kila nikiselect naona asiepewa nafasi ya kukubalika mbele za watu ndio anafit.

Hofu kubwa je huwenda macho yangu yamefunikwa na ukungu wa upendo mpaka kutokujua palipo sahihi ikanipelekea kukosea na kuharibu maisha yangu na kupata majutio makubwa.

Nimebaki njia panda...je, kwa maoni yako kwa maelezo yangu ni wapi palipokuwa sahihi?

Namalizia kwa kusema kosea kujenga ila usikosee kuoa..
Kumbe mtu mwenyewe ni mlevi. Haya olea watu tuone.
 
Muoaji ni nani??? Wewe au hao watu???? Nani ataenda kuishi na huyo mwanamke kwa maisha yake yoteee yaliyosalia ni wewe au hao watu?????? Mchana mwema mkuu mm nasubiri kitimoto choma hapa
 
Wewe dogo si uliandika unatafuta kazi? Naona na huu uzi unataka kupata mke.
Utamlisha nini au tayari umeshapata kazi.?
Kila la heri!
 
Mke awe na chura tu, akili atatumia zako.... zama za teknolojia hizi ni muhimu mke aenee vema kwenye camera.
 
Kati ya hao wawili ni yupo anayekusumbua/au kuomba kuolewa na wewe muishi wote?
 
Back
Top Bottom