Mwanamke usifurahie kutongozwa mara kwa mara, ni tatizo

Mwanamke usifurahie kutongozwa mara kwa mara, ni tatizo

Boss Man

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2022
Posts
458
Reaction score
991
Matumaini yangu wote ni wazima humu (Mungu ni mwema) hii mada itawalenga moja kwa moja Wasichana/Wanawake ila pia Mwanaume ukisoma utajifunza kitu

Asilimia kubwa ya wanawake wakitongozwa huwa wanahisi raha sana, hiyo feeling wanayojisikia haijalishi kwake kama kamkubali huyo Mwanaume au Kamkataa bila yeye kujua kitu gani kimesababisha yeye kutongozwa, unaweza sema ni uzuri sawa inawezekana ni uzuri wako ndio umemvutia Mwanaume hadi kukutongoza lakini labda nikwambie kitu pengine ulikuwa hujui, kama wewe ni Mwanamke na 'Unavutia' kitu kinachosababisha wewe kutongozwa mara kwa mara basi tatizo ndio linaanzia hapo

Kuna Mwanamke mwenye Magnetism na Mwanamke mwenye Attraction, mwenye attraction anavutia (havuti).

Kuna tofauti kati ya mtu anayevutia na mtu anayevuta, wanawake wengi waliopo Duniani sasa hivi wanajikita katika sector ya kuvutia badala ya kuvuta.

Gari linalovutia na gari linalovuta ni tofauti, Gari linalovuta kwa bomba distance inakuwa maintained (na mwenye mvuto ndio mwenye control) lakini linalovutia kwa kamba hana control (kamba hai-maintain distance) yeye anagongwagongwa vibaya vibaya maana yake hadhi hakuna.

Mvuto unatengeneza Vacuum yani mtu anayekuona kwa mbali anavutiwa akusogelee lakini hawezi kusogea kwasababu ya hadhi na heshima uliyonayo. Lakini kuvutia watu ni kwamba hakuna pressure katikati mtu anakutizama tu na anakuja na akija hakuna kinachokukinga kwasababu hadhi na heshima hakuna.

Watu wanadhani mvuto ni kuvutia tu, Mvuto ni Magnetism ni scientific power ambayo ipo obvious katika sayansi lakini ki-philosoph Magnetism (Mvuto) ni uwezo wa kukufanya uwe kama Star bila jitihada yani kusogelewa sio rahisi.

Mtu unatongozwa hovyo hovyo, hapo huna mvuto bali unavutia
 
Wanamke hujilinganisha urembo na thamani zao kupitia mitongozo

Wengi huamini kutongozwa ni ishara ya kwamba bado wapo moto

Mkuu amini kwamba mwanamke asipotongozwa analoose confidence kutokana na kilometers (umri wake) unatembea

Mi naona kwamba namba A ila kwa namba D ni kisanga lazima atatupia viwalo ili aonekane
 
Matumaini yangu wote ni wazima humu (Mungu ni mwema) hii mada itawalenga moja kwa moja Wasichana/Wanawake ila pia Mwanaume ukisoma utajifunza kitu
Sidhani kama slay queens wetu watakubaliana na wewe.
 
Wanamke hujilinganisha urembo na thamani zao kupitia mitongozo

Wengi huamini kutongozwa ni ishara ya kwamba bado wapo moto

Mkuu amini kwamba mwanamke asipotongozwa analoose confidence kutokana na kilometers (umri wake) unatembea

Mi naona kwamba namba A ila kwa namba D ni kisanga lazima atatupia viwalo ili aonekane
Ndicho kinacho wapoteza, kutongozwa sio ishara ya kwamba Bado [emoji91] ni wao wenyewe wametengeneza mazingira ya kujirahisisha ili kuvutia wanaume, na kama unavyojua kwa Mwanaume chochote kinawezekana, Kuna baadhi ya wanaume wanaweza kulala Hadi na vichaa ili mradi tu wamalize haja zao
 
Back
Top Bottom