Mwanamke usimdanganye mumeo hujazaa!

Mwanamke usimdanganye mumeo hujazaa!

Wana JF mimi nipo tofauti na hili swala la kuhusisha makabila ya watu na hii tabia ya kuficha watoto wa ujanani. MSIMAMO WANGU NI HUU TABIA HII IPO KARIBU KILA KABILA NA INATOKANA NA MAKUZI YA FAMILIA HUSIKA NA SI KABILA

Mchango wangu kwa topic hii ni Wazazi na walezi wawafundishe watoto wawe wa kike au wa kiume KUWA WAKWELI na kwa kuwa wakweli ndipo jamii itaondokana na tabia mbalimbali zisizofaa km hii
I second that.
Ila swala la kusema wazazi wawafundishe watoto wao kuwa wakweli wakati wengi wao ndo hua wanasuggest iwe siri (kuogopa aibu) sidhani kama inawezekana.Sema watu wajifunze kuwa wawazi, there is nothing wrong about a child that was born before you mate your partner, usimfanye huyo mtoto ajihisi hana thamani au hafai.Sio haki kwake wala kwa huyo unayemuoa/olewa nae.
 
Ni kweli Lizy hao wadada wengi tu wanazaa wakiwa teenagers, say form two. Anayewafanya wafanye siri ni wazazi. Akili yao inawatuma kuwa mtoto wao akijulikana kuwa amezalia nyumbani atakosa mume au anavunja heshima ya familia. Kosa mara nyingi ni la wazazi.

I second that.
Ila swala la kusema wazazi wawafundishe watoto wao kuwa wakweli wakati wengi wao ndo hua wanasuggest iwe siri (kuogopa aibu) sidhani kama inawezekana.Sema watu wajifunze kuwa wawazi, there is nothing wrong about a child that was born before you mate your partner, usimfanye huyo mtoto ajihisi hana thamani au hafai.Sio haki kwake wala kwa huyo unayemuoa/olewa nae.
 
Tuwekane wazi ni kabila gani hilo?

nahisi na warangi wana hako katabia....

Yaani mi kila siku nasema wanaume huwa wanajidai wajanja ila wakitendwa wanajiskia wameonewa! With current relations, mi sizimii wala kustuka aisee. Nina ndugu aliwahi kuacha shule form 2, akaishi na mwanaume na kuzaa twins bahati mbaya wakafariki na wakaingilia kumrudisha yule dada shule.

Yuko married, mume ana wivu kama kichaa na ndugu tunaambiwa tukae mbali tusije tukamfundisha mkewe tabia mbaya na tamaa. Yeye mwenyewe huwa anacheka anasema ' hajui mie ndo mwalimu mkuu wa tabia mbaya maskini'.

Mshkaji wangu alioa mzulu, alikuja gundua kumbe mtoto alieambiwa ni wa dada alikua ni wa mumewe baada ya mama mkwe kufariki na kuwalazimu kukaa nae.

Ndyoko, cases ni nyingi tu! Binamu yangu alikaa russia na married woman for 5 yrs, wakazaa na mtoto. Dada akija likizo kwa mumewe kimyaa, mwanaume anabaki na mtoto.

Bahati mbaya lakini nzuri kwao yule kiddo akafariki. Wamerudi nchini kimya as if nothing happened! Issue ni usipate wazimu na mwenzio. Siku yakifunuka u cross the bridge there and then, period. Maisha mafupi haya, usijitie wazimu.

Mhhhhhhhhhh! naamini kwamba ukiona kwako kunafuka moshi ujue kwa mwenzio kunaungua. Ktk siku zote nona leo madam umefunguka haswaaaaaaaaa!
 
I second that.
Ila swala la kusema wazazi wawafundishe watoto wao kuwa wakweli wakati wengi wao ndo hua wanasuggest iwe siri (kuogopa aibu) sidhani kama inawezekana.Sema watu wajifunze kuwa wawazi, there is nothing wrong about a child that was born before you mate your partner, usimfanye huyo mtoto ajihisi hana thamani au hafai.Sio haki kwake wala kwa huyo unayemuoa/olewa nae.
wewe mwanamke hakika ubarikiwe wewe na uzao wako, naona unaielewa vema jamii yako ya ki tz
 
Mie nawataja kama wataniua waniue ila ukweli ndio huo..... Wanawake wa kabila la kirangi wengi wana hiyo tabia sana ya kuficha watoto...



Back to topick: ni ulimbukeni wa hali ya juu na naungana na aliyesema kuwa ni kumnyima mtoto haki yake ya msingi...kama mwanaume kakupenda hata ukimwambia umezaa watoto 10 hawezi kukuacha, kwani kuwa na mtoto/watoto ni dhambi kwenye jamii? Tena basi hakuna dhambi mbaya kama mwanamke mzima na akili zako unabeba mimba miezi 9 kisha unazaa kwa uchungu afu eti unakutana na mtoto wa mwanamke mwenzio unamkana mwanao loooh.... Ni aibu kumtelekeza mtoto kijijini kwa bibi na kumlazimisha akuite shangazi/ dada/ mamdogo n.k..

Ila warangi wajameni........ya kweli hayo SL??? Mbona mi sijawahi kuona wala kusikia, ngoja leo nimdadisi mama yangu! Ila mi nawafahamu wadada watatu kutoka makabila tofauti tofauti, mmoja huwa anaenda kwa siri kumsabahi mwanae, mwingine walishirikiana mama na mtoto mtu kumficha mchumba ili asijue, na wa tatu hivo hivo hadi akawa anauliza aanzie wapi kumueleza mumewe coz alihisi kama kimesanuka!!
 
kwa hiyo uyo jamaa alikuwa akiishi kwa mwanamke? maana umesema alifungasha kurud dar
 
Afu mi naona watoto waliokuwa kind of rejected na wazazi wao huwa wanakuwa na tabia tofauti kidogo.
1. defensive nature, hujamguza lakini atakavyokuja na ushahidi kwamba hakufanya yeye kosa ni mkubwa kweli
2. Kutojiamini, mkiwa naye anahisi mnamchukia hata kama hakuna haja ya kuhisi hivyo
3. trust, haamini mtu hata mmoja ile ya kiukweli siku zote yko kimachale machale tu haamini mtu hata mmoja
4. Love, hata unconditional affection kwa mtu hata. Anampenda mtu foa a reason labda anapata kitu fulani toka kwake na aina hizo. Lakini kumpenda mtu freely ngumu sana kwao
5. Kisasi, du bahati mbaya umeingia kwenye kumi na nane yake kisasi chao huwa ni kikali kweli. Wanaishi by jino kwa jino rule.

Basi mie huwa napata shida kuwa nao katika mtiririko wa kila siku wa maisha maana wako siwezi hata elezea hadi ukae nae ndo labda mtanielewa hapa.

kuna ukweli hapo.
 
Tena umesema kweli, kuna bro. mmoja nafanya kazi naye ofisi moja alikuwa na mke wakapata wototo wawili, bahati mbaya mke akafariki mtoto wao wa pili akiwa mdogo sana (1.5yrs). Baadaye akaoa mdada mwingine ambaye alimkuta na kabinti kake. Mkaka aliwatambulisha kwa mke wake huyu wale watoto wawili tu wa marehemu, kumbe mshikaji ana msululu wa watoto kabla ya ndoa yake ya kwanza. Sasa ameshaona yule mke yuko fair kwa wototo aliowakuta ameamua kuleta kundini mtoto mmoja baada ya mwingine na ameshaleta watatu mpaka sasa. Mdada anajiuliza sijui christmas hii atapata mtoto mpya ama la . Na zote ni ndume copy right na baba yao mpaka kuwatoa nduki nomaaaaaa. Kwa hiyo ni yetu sote waume kwa wake.

we acha tu ndugu yangu huu mchezo haufai kabisa! Hapo mtu akigoma ni kubebeshwa mizigo ya lawama na kuitwa ana roho mbaya! Basi tu kwa sababu watoto hawana kosa unaweza kuwapokea japo na maswali mengi kichwani. Hata kama ukimwambia awakusanye wote awalete, bado utabaki na wasiwasi wa idadi kuongezeka. Dah.......
 
Hakuna mtu anayempenda mtu muongo,leave aside awe ndo mwenza wako wa maisha. Maana utajiuliza mengi sana mfano ni mangapi mengine aloficha.

Upendo hauko hivyo,unapoanza kuweka masharti unakua umetoka kwenye upendo tayari.Kwanini ujiulize kama umedaeganywa mengine?Wanadam tunapenda kuwazia mabaya tu,kwanini usiwaze ni hilo tu amekudanganya?
 
Upendo hauko hivyo,unapoanza kuweka masharti unakua umetoka kwenye upendo tayari.Kwanini ujiulize kama umedaeganywa mengine?Wanadam tunapenda kuwazia mabaya tu,kwanini usiwaze ni hilo tu amekudanganya?
Kupenda hakutakiwi kumfanya mtu mjinga.

Na swala la kuwazia mabaya linaletwa na hiyo siri/uongo ambao ni mkubwa kuliko. Mtu kumkana mtoto wake mwenyewe na kujifanya sio wake sio jambo la mchezo hata kidogo. Yani katika vitu ambavyo mtu anaweza/ruhusiwa kuficha akiwa kwenye mahusiano hicho sio kimoja wapo.
 
Kuhusu watu wa Singida sina data; ila Wahaya ngoja niwatetee.

Wahaya kuzalia nyumbani ni bonge la nuksi kwa familia, na ndio maana ni very rare kukuta binti wa kihaya kazaa bila kuolewa. Na hii inawahusu hata watoto wa kiume. Kijana haruhusiwi kuoa binti alokwisha zaa kama first wife; yaani unachekwa kabisa ukioa binti mwenye mtoto na wazazi na ukoo wanaweza wakasusia harusi.

Hilo la kuficha mtoto ulozaa sijawahi sikia kwani kwanza wahaya wanachunguza saana kabla ya kuoa hivyo watakushika tu.

Hao kundi la pili ndio zao sana!
 
Back
Top Bottom