Akotia
JF-Expert Member
- Dec 16, 2016
- 590
- 1,405
Wana JF
Wakati mwingine, tunahitaji siasa za kimya. Siasa zenye kutafakari, kusamehe, kuponya, na kujenga. Dunia imejaa kelele, vurugu, na giza . Tanzania bado ni kisiwa cha amani. Hii si bahati. Ni hekima ya viongozi wetu na kwa sasa, hekima hiyo imevaa sura ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Kuna watu wanapenda maneno kama “mapinduzi,” “uasii,” “kuamka,” na “mabadiliko ya kasi.”
Historia imetuonyesha mapinduzi si lelemama. Angalia Libya, Sudan, Syria, Haiti, Ethiopia. Nchi hizi zimejaa damu na machozi kwa sababu walikumbatia mabadiliko ya ghafla bila busara.
Mapinduzi si suluhisho la matatizo mara nyingi huwa ni mlango wa kuharibu kile tulichojenga kwa miaka mingi:
The Rebel – Albert Camus (1951)
Mama Samia amekuja na roho tofauti. Roho ya utulivu. Roho ya kuunganisha. Roho ya mabadiliko ya polepole lakini yenye mizizi.
Yeye hafanyi kelele anafanya kazi.
Na leo hii, Tanzania imetulia. Amani imerejea. Dunia inatusikiliza tena. Bado kuna watu wanachochea fitina wakidai maendeleo hayatoshi. Wanataka moto uwake ili wajipate kwenye moshi. Kukifuka moshi wao ndio wanajipata
Je?, Watanzania wa kawaida wako tayari kulipa gharama hiyo?
Wengi tunaishi kwa mlo wa siku moja. Wakulima wetu hawajui chochote kuhusu “strategic politics” wanahitaji tu mbegu tu ,mvua, na soko la kuuza. Mama Samia ameanza kuwajali bila makelele.
Wazazi wetu vijijini wanahitaji dawa hospitalini, sio siasa za vikao.
Tanzania si nchi ya fujo. Ni nchi ya busara. Ya taratibu. Ya maendeleo ya kimya.Na hilo ndilo Mama Samia analinda. Na kwa hilo, anapingwa si na wapinzani, bali na watu waliotaka urais huo. Hili si jambo geni katika historia ya siasa mara nyingi mlinzi wa amani huwa hapendwi na wale wenye tamaa ya vyeo.
Ukombozi wa kweli si mapinduzi ni utulivu unaoleta maendeleo ya polepole lakini ya kweli.
Ninyi mnaotaka kumuangusha Samia kwa jina la “kasi mpya” je, mko tayari kuona mamilioni wakiumia kwa sababu ya siasa zenu?