Habari za wakati huu wakuu,
Mwanamke wangu niliyeishi naye kwa miaka mitatu amenifanyia jambo la kikatili sana katika maisha yangu. Ni mwanamke pekee niliyempeleka nyumbani kwetu kumtambulisha.
Hatimaye siku ya jana nimeweza kujua ukweli kuwa amenisaliti.
Nilimuaga kuwa nasafiri kikazi na nitakaa wiki mbili mkoani, lakini matokeo yake nilikaa wiki moja tu.
Niliporudi kutoka mkoani, nilifika nyumbani na kumkuta hayupo. Nikawauliza majirani, wakaniambia huyu mtu hayupo yapata wiki sasa na aliwaambia anaenda kwao kusalimia.
Nikampigia simu kumuuliza yuko wapi, akaniambia yuko nyumbani. Nikamwambia, "Mbona mimi niko nyumbani toka jana na sijakuona?" Nikamwambia arudi nyumbani haraka sana.
Baada ya kupita lisaa limoja akarudi nyumbani.
Nikamuuliza alikuwa wapi wiki nzima na kwa nini hakuwa nyumbani. Akaniambia alikuwa kwa rafiki yake kwa sababu aliona kukaa peke yake atakuwa mpweke.
Nikamuuliza, "Wakati unaondoka kwa nini hukinipa taarifa yoyote?"
Nikachukua simu na kumpigia rafiki yake aliyesema yupo kwake. Maajabu, rafiki yake alikataa kuwa huyo mtu hakuwa kwake hata siku moja.
Nikaanza kumpiga huku nikimwambia aseme kweli alikuwa wapi. Akaendelea kuapa kuwa alikuwa kwa huyo huyo rafiki yake ambaye amemkataa.
Nikachukua simu yake na kufanya upekuzi. Ndipo nilipobaini namba ya simu ambayo imefutwa na ilikuwa imesaviwa "Mine♥️".
Hapo ndipo alipoanza kutetemeka na kulia huku akisema kuwa huyo jamaa amekuwa akimtongoza mara kwa mara na kumkataa, huku akiwa analia na kuapia kwa jina la Mungu. Wakati huo na kipigo kinaendelea.
Nikaamua kuipiga ile namba kwa kutumia simu yake.
Jamaa alipokea na kumuita mke wangu. Roho iliniuma sana.
Nikamwambia mimi ni kaka yake huyu binti kapata matatizo. Jamaa akasema, "Sawa, nakuja hapo fasta."
Nilishangaa kuwa jamaa anapajua mpaka ninapokaa.
Alivyofika nikamwambia, "Huyu ni mwanamke wangu wa muda mrefu, na anasema alikuwa kwako. Je, ni kweli?"
Jamaa akaniambia, "Kweli alikuwa kwangu kwa muda wa wiki nzima."
Nilijisikia vibaya mpaka nguvu ziliniishia mwilini na nikakaa chini.
Nikamuuliza mwanamke wangu, "Je, ni kweli ulikuwa kwa huyu jamaa?"
Mwanamke wangu akaniambia, "Ni kweli nilikuwa kwake."
🥺 Mwanamke niliyemtarajia kufunga naye pingu za maisha kaamua kunisaliti.
Nikamuuliza sababu zipi zilizomfanya anisaliti.
Akaniambia mbele ya jamaa kuwa simhudumii vizuri, kuna vitu huwa simpi, kama akitaka nguo mpya.
Nikamuuliza, "Kweli mke wangu, umri wote huo unawaza kuvaa na kupendeza na wala si kufanya maisha yatakayofanya tuishi vizuri hapo baadaye?"
Nikamuambia, "Hata kama ulikuwa unataka nguo, ulikuwa unashindwa kuniambia, 'Mume wangu, kuna nguo nimeipenda nataka uninunulie?' Je, nisingekununulia?"
Sasa kila kitu mpaka nikuambie? Kiukweli nilikosa nguvu sana.
Ukweli ni kwamba huyu mwanamke kanizidi miaka mitano kwa umri. Nilikuwa natarajia kuwa kwa kuwa kanizidi umri basi atakuwa mtu sasa kwangu, akijua kuwa ameshamaliza mambo ya ujana ili tufanye maisha.
Lakini kumbe nimegundua bado hajamaliza mambo yake, na pengine hata huko nyuma alikuwa akinisaliti sana bila mimi kujua.
Hatimaye jana nimeweza kujua kuwa si mwanamke sahihi kwangu.
Usiku wa kuamkia leo usingizi wangu ulikuwa taabu sana huku nikimuangalia na kujiuliza nimfanye nini huyu mwanamke.
Kwa nini kaamua kunifedhehesha sana?
Nitaweka wapi uso wangu nikitembea huko barabarani?
Ndugu zangu, nipo katika hali ngumu sana ya kimawazo.