Mwanamke

Mwanamke

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu sana kama mtu kuzaliwa mwanamke ni laana, hususan katika hii jamii yetu. Kwanini nimekuwa nikijiuliza hivyo? Sababu ni nyingi na hapo chini nitazitaja chache.

Uanamke umekuwa ukihusishwa na mambo mabaya mabaya tu. Tusi kubwa kwenye lugha ya Kiswahili linahusu kiungo cha uzazi cha mwanamke [mfano, K ya mamako].

Ukitaka kumtusi mwanaume basi mwambie kuwa 'ana mambo ya kike'. Kwanza, mambo ya kike ni yepi hayo? Na pili, kwa nini kuwa na mambo ya kike kutumiwe au kuchukuliwe kuwa ni tusi?

Cha kusikitisha zaidi ni unakuta wanawake nao wako mstari wa mbele katika kuendeleza hiyo dhana ya uanamke kuwa tusi.Hata humu tumeshaona watu ambao wamejipambanua kuwa ni wadada/ wanawake wakisema waziwazi kuwa wao hawana marafiki wengi wanawake na kwamba marafiki zao wengi ni wanaume.

Mwanamke kuwa na marafiki wengi walio wanawake ni mkosi, au? Vile vile, humu humu jamvini tumeshaona watu wajipambanuao kuwa ni wanawake wakiwatukana watu wajipambanuao kuwa ni wanaume na kuwaita ama kuwaambia kuwa wana mambo ya kike.

Inasikitisha kuona mtu ajipambanuaye kuwa ni mwanamke akitumia hiyo hiyo hali ya uanamke kumtusi mtu mwingine. Wakati mwingine huwa nakubaliana na ule usemi wa kwamba adui wa mwanamke ni mwanamke.

Wadau nyie mna maoni gani?
 
Ni wadhaifu sana sema hatuwadharau ila ndo hali halisi yao kwa mwanaume kuwa dhaifu kama alio nao mwanamke sio vyema.
 
Ni wadhaifu sana sema hatuwadharau ila ndo hali halisi yao kwa mwanaume kuwa dhaifu kama alio nao mwanamke sio vyema. Ila pia nkwadokeze, vijana wawili wa kiume kupanga chumba na kuishi pamoja inawezekana ila kwa wasichana wawili mara nyingi hawawez ishi sehem moja na kuivana.
 
Ni jamii yetu tu au jamii zote?

nafikiri ni universal ...pamoja na kuwa jamii zingine zimefikia hatua hata ya waliozaliwa
wanaume kuwa wazi kuwa wanatamani kuwa wanawake but still kuna watu jamii hizo hizo wana
wa treat wanawake kama watu weak na ni tusi kwa mwanaume kufananishwa na mwanamke...
 
Lakini mbona kila binadamu, awe wa kiume au wa kike, ana udhaifu wake.

Au kuna udhaifu wa kike na wa kiume?
 
Nakubaliana na ww % 100. Na kuna kauli yao moja hua inaniboa sana . Wanawake tukiwezeshwa tunaweza. Why wasisema tunaweza lakini ndivyo walivyojiweka.. unakuta mwanamke anamwambia mwanamke mwenzake K*ma ww m hua nachek sana.
 
Ni jamii yetu tu au jamii zote?

nafikiri ni universal ...pamoja na kuwa jamii zingine zimefikia hatua hata ya waliozaliwa
wanaume kuwa wazi kuwa wanatamani kuwa wanawake but still kuna watu jamii hizo hizo wana
wa treat wanawake kama watu weak na ni tusi kwa mwanaume kufananishwa na mwanamke...

Binafsi nadhani ni jamii nyingi [siwezi kusema ni zote kwa sababu sina ushahidi huo] ziko hivyo.

Na la kustaajabisha zaidi unakuta wanawake hao hao ndo wako mstari wa mbele kutukana watu matusi yahusuyo uanamke.

Bado kabisa sielewi kwa nini uanamke huhusishwa na mambo mabaya mabaya tu.

Mpaka eti kuna 'wivu wa kike'.

Sasa huo wivu wa kike sijui ukoje na upo wa kike, je, ina maana na wa kiume upo?
 
Kwa nini neno bitch!!! asshole na maungo ya mwanamke yanatumika sana na wanaoongea ki zungu wale "wahuni" tena ni kama kiunganishi flani
hadi kwenye nyimbo na kadhalika

sio jamii zeru tu bali dunia yote

bitch..better have my money
 
kwa nini neno bitch!!! asshole na maungo ya mwanamke yanatumika sana na wanaoongea ki zungu wale "wahuni" tena ni kama kiunganishi flani
hadi kwenye nyimbo na kadhalika

sio jamii zeru tu bali dunia yote

bitch..better have my money

Okay, lakini kwa nini iwe hivyo?

Kwani uanamke ni laana?
 
Okay, lakini kwa nini iwe hivyo?

Kwani uanamke ni laana?
Nyani ngabu uanamke sio laana ni zawad nzuri
maana sisi tunasaidiana uumbaji na Mungu(najua uanmini )
maana sisi ndo tunabeba mimba na kuzaa
nadhani jamii inajitengenezea misemo ambayo awali huwa matusi ila baadae ufanywa kama mazoea

hilo neno wivu wa kike nadhani ni kiongozi mkubwa tu aliongea hivyo
so kwa kweli inahitaj utashi wa hali ya juu kujua kwamba hii sio kawaida bali ni udhalilishaji
 
nyani ngabu uanamke sio laana ni zawad nzuri

Huwa nastaajabu sana napoona mwanamke anamtusi mwanaume kwa kutumia hali ya uanamke kana kwamba kuwa mwanamke ni jambo baya sana.

Oh well.....
 
Okay, lakini kwa nini iwe hivyo?

Kwani uanamke ni laana?

Kuna siku nilijiuliza kwenye wimbo wa breezy "loyal"
why alitumia neno bitch almost in the whole chorus
why inakua kawaida namna hii
broke bitch
i dont fu..k broke bitch
why this way
then nikaja na wazo wanawake wenyewe wanaitengeneza hali hiyo kuwa ya kawaida
mavazi yao,wenyewe wanavoitana
wnavyo behave pia wanavyo respond na ku react hayo maungo yakinyambuliwa
kwa mfano mtu anajiita bad bitch
hivi huyu ukimuita bitch inakuaje hapo?

so jinsi wanawale wanavyoliweka hili swala kuwa la mazoea ndivyo hali inaendelea kua mbaya
 
Lakini mbona kila binadamu, awe wa kiume au wa kike, ana udhaifu wake.

Au kuna udhaifu wa kike na wa kiume?

Naamini hivyo ila kwao imezidishwa pia nadharia ya jamii kwa ujumla imeliwekea mkingio jambo hilo kwa ujumla.
 
Ukute mama akimtusi mwanae wa kumzaa kwa kutaja kiungo chake ndio utashangaa...
Upo udhaifu wa kibinadam, lakini pia kuna udhaifu wa mwanamke..ambao kwa maoni yangu, unazidi udhaifu wa mwanaume. Wale tunaofuatilia maswala ya Mungu tunaaminishwa kuwa "mwanamke ni kiumbe dhaifu"...
 
nyani ngabu uanamke sio laana ni zawad nzuri
maana sisi tunasaidiana uumbaji na Mungu(najua uanmini )
maana sisi ndo tunabeba mimba na kuzaa
nadhani jamii inajitengenezea misemo ambayo awali huwa matusi ila baadae ufanywa kama mazoea

hilo neno wivu wa kike nadhani ni kiongozi mkubwa tu aliongea hivyo
so kwa kweli inahitaj utashi wa hali ya juu kujua kwamba hii sio kawaida bali ni udhalilishaji

.kwenye kusaidiana na Mungu kwenye uumbaji hata mie sikuamini, kwani kazi ya kuijaza nchi ni ya wote Me na Ke, tofauti yake ni kwamba mwanamke ana hali ya kumilikiwa, na ndio maana kwenye uzazi mwanaume anatoa MBEGU na mwanamke anatoa YAI na uwanja wa kupanda hiyo mbegu ya mwanaume, na mmiliki mkuu wa kilichopandwa ni mwanaume kwani shamba unaweza kodi..
Kurudi kwako Mkuu Nyani Ngabu nadhani tatizo la haya yote lilianzia pale mwanamke alipotaka usawa na mwanaume alafu mwishoni mwa siku akagundua bila kuwa chini ya mwongozo wa mwanaume mambo huwa yanakwenda ndivyo sivyo, hivyo mwanamke mwenyewe akaanza kujiona duni,na ikitokea anajitusi ni katika kudhihirisha madhaifu yake, kiukweli mwanamke ni kiumbe dhaifu karibu kila kona, na maswali yako mkuu yatakuja kupata majibu tofauti siku akitokea mwanadamu asiye mwanaume lakini awe dhaifu zaidi ya mwanamke!!
 
Nyani Ngabu, hili jambo liko tangu kale nadhani tangu kuumbwa kwa mtu mwanamke na mtu mwanaume, hata ukisoma maandiko ya hizi dini za mapokeo zikiwemo taboo na misingi ya dini za kale zinampa kiumbe wa kike hadhi ya chini sana na wao wakakubaliana na hali hiyo. hata hizo nchi zilizoendelea hali ilikuwa mbaya, Kwa mfano kama sikosei nchi kama Marekani au Uingereza, mwanamke amepewa haki ya kupiga kura miongo kadhaa iliyopita baada ya kunyimwa hki hiyo kwa miongo mingi tu, maisha ya mwanamke yamekuwa ya kukandamizwa kila uchao.

Nilisoma uzi wa lara 1 wa hivi karibuni, kalielezea vizuri sana jambo hilo.
 
Last edited by a moderator:
Wanawake wasingekuwepo dunia ingekuwa salama
 
Vitabu vya mungu vinasema wanawake tuwasamehe x70. Kwa cku, hii inaonesha wanamapungufu mengi,
Wanawake ndo chanzo cha madhambi aliekula tunda ktk bustani ni hawa,
Hata leo ukiangalia mitaani wanawake ndio wenye kutembea uchi, na kusababisha aina nyingi za maasi, pamoja na yote hayo ni kosa kuwadharau au kuwa kashifu nlipo kosea I'm verre sore...

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom