Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu sana kama mtu kuzaliwa mwanamke ni laana, hususan katika hii jamii yetu. Kwanini nimekuwa nikijiuliza hivyo? Sababu ni nyingi na hapo chini nitazitaja chache.
Uanamke umekuwa ukihusishwa na mambo mabaya mabaya tu. Tusi kubwa kwenye lugha ya Kiswahili linahusu kiungo cha uzazi cha mwanamke [mfano, K ya mamako].
Ukitaka kumtusi mwanaume basi mwambie kuwa 'ana mambo ya kike'. Kwanza, mambo ya kike ni yepi hayo? Na pili, kwa nini kuwa na mambo ya kike kutumiwe au kuchukuliwe kuwa ni tusi?
Cha kusikitisha zaidi ni unakuta wanawake nao wako mstari wa mbele katika kuendeleza hiyo dhana ya uanamke kuwa tusi.Hata humu tumeshaona watu ambao wamejipambanua kuwa ni wadada/ wanawake wakisema waziwazi kuwa wao hawana marafiki wengi wanawake na kwamba marafiki zao wengi ni wanaume.
Mwanamke kuwa na marafiki wengi walio wanawake ni mkosi, au? Vile vile, humu humu jamvini tumeshaona watu wajipambanuao kuwa ni wanawake wakiwatukana watu wajipambanuao kuwa ni wanaume na kuwaita ama kuwaambia kuwa wana mambo ya kike.
Inasikitisha kuona mtu ajipambanuaye kuwa ni mwanamke akitumia hiyo hiyo hali ya uanamke kumtusi mtu mwingine. Wakati mwingine huwa nakubaliana na ule usemi wa kwamba adui wa mwanamke ni mwanamke.
Wadau nyie mna maoni gani?