NANDERA
JF-Expert Member
- Mar 18, 2014
- 2,024
- 2,487
Hata mimi nimeshahitimisha kuwa mwanamke ni kiumbe dhaifu.
Kwa sababu haingii akilini kuona mwanamke akimtusi mwanamume kuwa eti 'ana mambo ya kike'.
Mambo ya kike yangekuwa si 'mabaya' kwa nini sasa hata hao hao wanawake wangeyahusisha na tusi?
Na imani yangu ni kwamba hata wao wanawake [na hapa nazungumzia kiujumla jumla tu] huwa wanajiona ni viumbe duni mbele ya wanaume.
mtoto wa kike na wa kiume wanalelewa na mama aliyekuwa programmed kuwa mwanamke ni dhaifu na mwanaume ni shujaa na kuna mifumo ya kijamii ya kufanya iwe hivyo. Kwa hiyo toka utotoni watoto wote wanakuwa programmed hivyo. Kwa hiyo si ajabu kukuta mwanamke akimdharau mwanamke mwenzie kwa sababu ndivyo wanavyojiona. Mtoto wa kike aliyelelewa katika mazingira ya usawa wa kibinadamu mara nyingi hujikuta akiambatana zaidi na wanaume kuliko wanawake waliolelewa katika mazingira ya "mwanamke dhaifu". Hutamkuta akiomba "favours" - anajua kujitegemea na kusimama mwenyewe. Huyu hawezi kukaa na wanawake walioambiwa na kuamini hawajiwezi bila msaada wa wanaume. Na mwanamke wa aina hii wanaume humgwaya kwa sababu haenei kwenye fremu wanayoijua ya mwanamke; wanawake waliokubali kuwa ni dhaifu pia humbeza na kusema anajitia kufanya mambo ya kiume. Hata akigombea uenyekiti wa kitongoji hawamchagui kwa sababu walishaambiwa na kuamini mwanamke kwake jikoni. Kwa hiyo mwanamke kujiona kiumbe dhaifu si ajabu, na mama kumtukania mwanae sehemu zake za siri ni mwendelezo wa mfumo ule ule wa "mwenye nguvu kumuonea "dhaifu". Mimi siku hizi hata sishangai kuskia mwanamke anajitukana, au yuko ofisi flani ananyanyasa wenzie. Ni kwamba wamerithi mifumo kandamizi.