Mwanamke

Hata kwa TB Joshua wanaoombewa na kuanguka kwa mapepo ni wanawake wengi.
Ukija kwenye baibo, waliohesabiwa wanaume 5000, bila wanawake.
Ukija kwa waislam, wanawake wametengwa kwenye nyumba za ibada na akiwa kwenye siku zake haruhusiwi kufunga.
 

Hata mimi nimeshahitimisha kuwa mwanamke ni kiumbe dhaifu.

Kwa sababu haingii akilini kuona mwanamke akimtusi mwanamume kuwa eti 'ana mambo ya kike'.

Mambo ya kike yangekuwa si 'mabaya' kwa nini sasa hata hao hao wanawake wangeyahusisha na tusi?

Na imani yangu ni kwamba hata wao wanawake [na hapa nazungumzia kiujumla jumla tu] huwa wanajiona ni viumbe duni mbele ya wanaume.
 

Mimi najiona mwenye nguvu mbele yako
 
Toka zamani huko watu wamekua wakifundishwa kua mwamanke ni sehemu ya matatizo katika jamii. Ndio maana watu husema dunia ingekua salama kama hakungekua na mwanamke.

Watu wa dini wanasema shida ilianza kwa adamu ambae baada ya kupata matatizo yake akamlaumu mungu kwa mwanamke aliemletea kwamba ndio chanzo cha matatizo yake.

Plato alifundisha kwamba duniani kuna mikosi miwili, ya kwanza ni kifo ya pili ni kuzaliwa mwanamke, kwamba kuzaliwa mwanamke ni mkosi mkubwa unaopitwa na kifo pekee.

Socret yeye alikua anafundisha kwamba ukiwa muoga muoga hivi ukifa utazaliwa mwanamke, kwa hiyo watu wakawa na negativity na uanamke toka zamani hizo.

Binafsi sijui tatizo ni nini hasa.
 

Hatari sana..
 
Kitu kingine sisi wanawake hatujiamini na kuueshimu huo uanamke wetu.Mfano ilo tusi la kuutaja kiungo cha mwanamke unakuta hata mwanamke mwenyewe (baadhi) limetamalaki mdomoni kwake kila iitwapo leo.

Mi naona thamani ya mwanamke imekua ndogo tangu kuumbwa kwa ulimwengu, pale ambapo Mungu alichomoa ubavu wa Adam akamuumba Eva.Hii inawafanya wanaume wajione wao ni viumbe kamili na sisi ni kama nyongeza tu.
Ushauri, wanawake twapaswa kujiamini maana Mungu ameshatuinua ya kwamba kila mtu atapita katika tumbo la mwanamke .
 
Hii topic imenikumbusha ambavyo hata lugha ina wa undermine wanawake."language and gender"Neno linakua na maana zaidi ya moja ambapo maana moja inamkandamiza mwanamke.mf.mistress maana ya pili ni concubine/ hawara.
 
Kiuhalusia sisi ni wadhaifu na ndio maana MWENYEZI MUNGU aliwaamrisha muishi na sisi kwa umakini mkubwa........... Ukiyafata hayo hutoona tabu kuishi nasisi
 
Wanasema mwalimu wa mwanamke ni kipofu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…