Mwanamke


mtoto wa kike na wa kiume wanalelewa na mama aliyekuwa programmed kuwa mwanamke ni dhaifu na mwanaume ni shujaa na kuna mifumo ya kijamii ya kufanya iwe hivyo. Kwa hiyo toka utotoni watoto wote wanakuwa programmed hivyo. Kwa hiyo si ajabu kukuta mwanamke akimdharau mwanamke mwenzie kwa sababu ndivyo wanavyojiona. Mtoto wa kike aliyelelewa katika mazingira ya usawa wa kibinadamu mara nyingi hujikuta akiambatana zaidi na wanaume kuliko wanawake waliolelewa katika mazingira ya "mwanamke dhaifu". Hutamkuta akiomba "favours" - anajua kujitegemea na kusimama mwenyewe. Huyu hawezi kukaa na wanawake walioambiwa na kuamini hawajiwezi bila msaada wa wanaume. Na mwanamke wa aina hii wanaume humgwaya kwa sababu haenei kwenye fremu wanayoijua ya mwanamke; wanawake waliokubali kuwa ni dhaifu pia humbeza na kusema anajitia kufanya mambo ya kiume. Hata akigombea uenyekiti wa kitongoji hawamchagui kwa sababu walishaambiwa na kuamini mwanamke kwake jikoni. Kwa hiyo mwanamke kujiona kiumbe dhaifu si ajabu, na mama kumtukania mwanae sehemu zake za siri ni mwendelezo wa mfumo ule ule wa "mwenye nguvu kumuonea "dhaifu". Mimi siku hizi hata sishangai kuskia mwanamke anajitukana, au yuko ofisi flani ananyanyasa wenzie. Ni kwamba wamerithi mifumo kandamizi.
 
Kiuhalusia sisi ni wadhaifu na ndio maana MWENYEZI MUNGU aliwaamrisha muishi na sisi kwa umakini mkubwa........... Ukiyafata hayo hutoona tabu kuishi nasisi

hapo kwenye "sisi" weka "mimi". Mtu dhaifu unaishi nae kwa umakini ili iweje? Ukiona mtu anahangaika kukukandamiza kwa nguvu au kwa maneno na nyimbo ujue una nguvu kwa hiyo anataka kuendelea kukunyonya. Usimsingizie Mwenyenzi Mungu. Mbona kuna wanawake ndo wanalisha familia na kusomesha watoto na kutunza wazazi na kuendesha vijiji na nchi? Au mungu wao mwingine?
 

Kwa batili mbaya sio mzuri kwenye notes ukitaka tuelewane njoo inbox nikudadavulie
 
Halafu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…