Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mpaka unaandika humu JF inaonekana hili ni tatizo kubwa na huna pa kutokea maana hujaweza fanya hivyo kwa siku zote ambazo mwenzi wako amekuwa akikuomba msaada huo.
Kuna mambo ya msingi ya kuangalia hasa kwa wapendanao,je kipato chako kinatosha kumpa kila anapohitaji?Kama ndivyo basi angalia ni wakati gani wa kutoa na wakati gani usitoe maana inawezekana kweli akawa na matatizo ambayo labda hamjaweza kukaa chini na kuyazungumza kwa undani na kujua namna ya kuyatatua.
Kwa ushauri kaa chini na mwenza wako mzungumze kuhusu maisha maana hapa inaonekana kabisa hata kama ndoa katangaza ila hakuna mmoja kati yenu aliye wazi kwa mwenzake na hamna mpango wa kushirikiana katika matumizi jambo ambalo ni hatari mkiingia katika ndoa.
duwewe 'umemzoesha' afanye nini?
unam honga na yeye anaenda kuhonga mwingine....
kazi ni kwako