Mwanamme kumuomba pesa mpenzi wake, imekaaje?

Mwanamme kumuomba pesa mpenzi wake, imekaaje?

kusaidiana ndo mpango c isue wewe upokee 2,jua kutoa pia,binafsi napenda kusaidiana nkiwa nacho 2natumia nawe iwe hvyo hvyo,kinyume cha hapo am nt ready.jamaa ako kama kipato chake n chni yko haimaanish always awe tegmez anapaswa naye kuplay role flan
 
Kama unaweza endelea kumsaidia, unaposhindwa kaa nae chini muongee ila inaonesha kama ushamchoka huyo mtu.
 
Joseph, naomba nifafanue vizuri, naona nipost thread kwa haraka sikujieleza vizuri.
Naomba ieleweke kwamba kama kuna wagumu wa kutoa pesa kumpa mwanamme nadhani niko kwenye top 10 kama sio top 5, ndio maana nimekerekwa nikaja hapa mapema kabla tatizo halijawa sugu.
Sina muda mrefu na huyu mtangaza ndoa, tuna kama 5-6 months hivi. Mara ya kwanza na ya pili alikuja na genuine reason ambayo mimi nilioona, nilikwazika kidogo maana kwangu mimi sioni kama ni sawa nimpe mwanamme pesa, but nilimsaidia kwa makubaliano arudishe. hajarudisha hizo mara mbili kaja kuomba tena kiasi kidogo tu, sijampa kwa kweli, pia kuomba omba vitu vya kipuuzi, siwezi kuweka hapa maana itakua kama namdhalilisha. hachoki kuomba pamoja na kwamba sasa hivi simpi, sasa hii kusema kweli mimi inanikera. maana mimi nina maisha yangu ambayo honestly, siishi kwa kutegemea mtu zaidi ya kazi yangu. mtu anipe au asinipe kwangu ni sawa vile I can manage on my own, what i need ni mahusiano mazuri na mapenzi ya kweli.
sijaja hapa jamvini eti kwa sababu nimetoa sana, lah hasha..!!!

Mpaka unaandika humu JF inaonekana hili ni tatizo kubwa na huna pa kutokea maana hujaweza fanya hivyo kwa siku zote ambazo mwenzi wako amekuwa akikuomba msaada huo.
Kuna mambo ya msingi ya kuangalia hasa kwa wapendanao,je kipato chako kinatosha kumpa kila anapohitaji?Kama ndivyo basi angalia ni wakati gani wa kutoa na wakati gani usitoe maana inawezekana kweli akawa na matatizo ambayo labda hamjaweza kukaa chini na kuyazungumza kwa undani na kujua namna ya kuyatatua.
Kwa ushauri kaa chini na mwenza wako mzungumze kuhusu maisha maana hapa inaonekana kabisa hata kama ndoa katangaza ila hakuna mmoja kati yenu aliye wazi kwa mwenzake na hamna mpango wa kushirikiana katika matumizi jambo ambalo ni hatari mkiingia katika ndoa.
 
Kuomba omba ni tabia mbaya tu ambayo mtu hujizoesha,awe mwanamke ama mwanaume! Huyo jamaa si aishi kutokana na kipato chake? Ww kuna watu wamekuzidi kipato,unaishi kwa kuhemea kwao? Hiyo ndoa ni geresha tu,hebu mdanganye umuambie umefukuzwa kazi uone atakavyochukua ndogondogo! Mwanaume hajitambulishi,angeishi kiume kwa kipato alichonacho! Stuka!
 
kwa kua mnapendana nafikiri ni jambo la kukaa na kuongea ila wakati mwingine huwa ni tabia ya mtu kuombaomba, km ndio tabia yake basi ukae ukijua kua mkioana mzigo mkubwa utakua juu yako lakini sio mbaya sana. Naona ni vizuri sometimes uwe unakataa kumpa hela ili ajifunze na asiwe tegemezi na usimwache kwani ukimwacha hujamsaidia ila ukimwambia na kuwa unakataa kumpa hela anaweza kujifunza. Labda kama umepata mtu mwingie ndo mana unamwacha
teh teh teh.Ila ninyi wanawake aise, mkituomba hela sisi hatusemi ila sisi tukiomba mashitaka kotekote, je ktk hili ile gender equality na ile Beijing conference haiziapply? hahahahaha
 
ukimpenda kwa dhati haya mengine hutoyaona. kama na ndoa katangaza we hilo unalionaje.? kama kakugeuza we CHUMIO mtafika mbali..? amekupenda kwa kuwa una kipato kuzidi yeye ama vp . tafakari kisha chukua hatua ushauli utapewa bali wewe mwenyewe ndio mwamuzi. jikune pawashapo.
 
Back
Top Bottom