The Dictator
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 4,475
- 12,281
Jamaa mmoja mwenye umri wa miaka 26 anayeitwa Leon Gillespie alikamatwa kwa kuvaa vazi la 'Grim Reaper' na kusimama kwenye paa la Hospitali ya Ysbyty Glan Clwyd huko Wales.
Baada ya mahojiano likubali mashtaka mahakamani na kupigwa faini ya pauni 200 (£200) na mahakama ya Llandudno.
Tukio hilo lilisababisha hofu kubwa na taharuki kwa wagonjwa na wageni waliokuwa wakimtazama kutoka chini ya jengo hilo la hospitali.