Mwanamuziki mkongwe Kabeya Badu amefariki

Mwanamuziki mkongwe Kabeya Badu amefariki

KIPUMPUSWA

Senior Member
Joined
Jul 16, 2011
Posts
106
Reaction score
35
mwanamuziki Kabeya Badu amefariki leo. Chanzo cha habari TBC fm
 
Weka nyama kwenye habari yako.
Mwanamziki wa nchi gani?
Anafanya mziki wa aina gani?
Ni wa kike au wa kiume?

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Kabeya Badu alikuwa mwimbaji wa Kyauri Voice 1978 akahamia Marquis na baadaye Safari Sound alikodumu tangu Masantula, Duku duku na Ndekule.
ameimba pia na Mk group, Tancut almas, Zaita musica ya Kasheba na Wazee sugu.
 
Ana sauti nzuri sana huyu jamaa. Mara ya mwisho nilimuona akiimba na King Kikii. RIP
 
Kabeya Kapumzike!
Huyu alikuwa mwanamuziki machachari sana, alitamba na nyimbo zake Ziada, Majuto na Mama Kaji
Pia aliuimba wimbo wa Kawelee Anne Marie kwa ustadi mkubwa akiwa na Tancut Almas!
Huyu ni Mzee Sugu aliyemalizia ngwe yake kwa kuimbia Band ya La Capital Wazee Sugu..
Alipoanza kuumwa, alinipigia simu kunijulisha na kwa hakika nilihuzunika sana
 
Angeluu ! Ziada ! Nishike mukono tuonyeshe kweli tunapenda eeh, nilishe nikulishe ni ishara ya upendo oooh !
Ngoma za moghorofani !
 
Aliniambia;
Mwanangu, mimi naumwa, nilikuwa natembea kumbe ndani mwilini kumeharibika, nimeambiwa mafigo yangu yanashindwa kufanya kazi.. Nilivyoambiwa hivyo, nimekata tamaa kbs, nasubiri tu sasa.. Nina siku 3 sijisikii hamu ya kula kbs.
Nilihuzunika sn lkn nilijikaza, nikamfariji na kumuomba ajitahidi kula, ila afuate masharti ya Daktari ktk vyakula.. Nitamkumbuka sn mzee Kabeya, hasa kwa wema na upendo wake kwa watu wote, hakujali umaarufu wake, alimuheshimu kila mtu!
Alikuwa chaguo kipenzi kwa Ndala Kasheba na King Kiki, na mara zote walikuwa pamoja..
Rest in Peace, Kabeya Badu
 
Sauti yake unaipata kwenye nyimbo kama;
ZIADA, MAMA KAJ, KIBWE MUTOMBO, SALZA, MARASHI YA PEMBA, SAMAHANI YA UONGO, MAJUTO, MOKILI, NTALE, NIMLILIE NANI, RAJAY, ANNE MARIE, MASHAKA, KOKOLAY, MARINELLA, KESI YA KHANGA, KITAMBAA CHEUPE NA NYINGINE NYINGI.
Alikuwa ni maridadi katika kuimba na ndio alishirikishwa katika nyimbo nyingi sana hasa za Ndala Kasheba na King Kiki.
Guitarla
 
Namkumbuka kwenye wimbo wa Ziada. Aliimba peke yake mwanzo hadi mwisho. Nakumbuka baadhi ya maneno ya wimbo "Namlia Ziada, nimwite nani sauti inapaa angani bila kujibiwa ee! "
 
RIP Mzee Kabeya,wazee Sugu wanapukutika lakini heshima yao itadumu vizazi vyote.
 
RIP Kabeya Badu... Natumaini ndiye huyu ambaye mchambuzi wa Muziki wa Dansi Zomboko alikasirishwa na wanamuziki kutokujitokeza kwenye mazishi yake.
 
Kabeya Kapumzike!
Huyu alikuwa mwanamuziki machachari sana, alitamba na nyimbo zake Ziada, Majuto na Mama Kaji
Pia aliuimba wimbo wa Kawelee Anne Marie kwa ustadi mkubwa akiwa na Tancut Almas!
Huyu ni Mzee Sugu aliyemalizia ngwe yake kwa kuimbia Band ya La Capital Wazee Sugu..
Alipoanza kuumwa, alinipigia simu kunijulisha na kwa hakika nilihuzunika sana[/shilla chiumbo]
 
huyu ni mwanamuziki wa kikongo, aliyekujaga hapa Tanzania mwishoni mwa miaka ya 70, akaimbia band za Marquis, Safari Sound, Tuncat Almas, Zaita musica na akamalizia kuimba na kina King KiKi, Wazee Sugu.. kwa nyimbo nilizozitaja kuwa aliimbia, kwa mtu makini kabisa anayeujua muziki wetu, atajua tu kuwa ni muziki wa Rhumba.. pata kibao chake cha Ziada au Kimbunga, zote akiwa Safari Sound.. Alijulikana kama Chiriku
 
Kabeya Badu, eighties babies wanaweza wasimjue.

Marquis du Zaire Original loong time enzi za Chinyama Chiyaza, Kikumbi Mwanza Mpango Nguza Viking, Vumbi (jamaa anapiga gitaa mpaka chini panatoka vumbi) nafikiri na Ramadhani "Remmy" Ongala pamoja na Makassy.

May all beings attain enlighenment.

Kifoo kifooo, kifo hakina huruma - Remmy Ongala
 
Back
Top Bottom