TANZIA Mwanamuziki mkongwe, Said Mabera afariki dunia

TANZIA Mwanamuziki mkongwe, Said Mabera afariki dunia

Nitakwenda na naani msondo ngooma, nitacheza na nani magoma kitakita.
Kalale mahali pema .
Athumani Momba,
Selemani Mbwembwe,
Maina,
TX Moshi William,
Muhidin Maalim Ngurumo na leo
Said Mabera.
Daaah !! Mm nipo mkoani lakini nashiriki sana shoo zao pale buza,mwembe yanga ,nk nimeteseka sana aiseee hebu tuwakulisheni maziki bana
 
Nitakwenda na naani msondo ngooma, nitacheza na nani magoma kitakita.
Kalale mahali pema .
Athumani Momba,
Selemani Mbwembwe,
Maina,
TX Moshi William,
Muhidin Maalim Ngurumo na leo
Said Mabera.

'Dally Kimoko Virus' anamaliza sana 'Wanamuziki' na sasa baada Kumaliza 'Kupukutisha' hawa wa Msondo zamu ya FM Academia na Twanga yaja.
 
Nitakwenda na naani msondo ngooma, nitacheza na nani magoma kitakita.
Kalale mahali pema .
Athumani Momba,
Selemani Mbwembwe,
Maina,
TX Moshi William,
Muhidin Maalim Ngurumo na leo
Said Mabera.
Pumzikeni kwa amani wasanii wetu Nguli - nyie ni kielelezo cha mziki wa Kibantu hapa Tanzania.

 
Nilivyokuwa mdogo nlikua naskia wimbo unaimbwa "Mabeee mabee mabela[emoji445]" daah RIP
 
Gwiji wa muziki wa dansi na Kiongozi wa bendi ya Msondo Ngoma, Saidi Mabera amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumanne Septemba 29, baada ya kuugua kwa zaidi ya miezi miwili. Mazishi yatafanyika leo saa 10 jioni nyumbani kwake Goba.

Msiba upo Nyumbani kwake Tegeta A maeneo ya Goba jijini Dar es Salaam.

===
SAID MABERA WA MSONDO NGOMA AFARIKI DUNIA

GWIJI wa ukung'utaji gitaa la solo hapa nchini na kiongozi wa bendi ya Msondo Ngoma, Said Mabera amefariki dunia jana saa 6 za usiku.

Mabera ambaye ameitumikia Msondo Ngoma tangu mwaka 1973 bila kuhama hata mara moja, amefariki baada ya kuugua kwa zaidi ya miezi miwili.

Mtoto wa marehemu, Mabera Said amesema kuwa msiba uko nyumbani kwao Goba jijini Dar es Salaam na mazishi yatafanyika leo saa 10 alasiri huko huko Goba.
So sad,pumzika kwa amani baba yetu.Poleni sana wafiwa.
 
sio mbaya kidogo huyu aliku amefaidi faidi hewa safi ya duniani

innalillahi wa innailayhi rajiun...

akavune alichopanda
 
Mkewe huyu mzee mabela,kipindi hiyo wanaishi mburahati kwa jongo alimzulumu mother angu pesa kama 1500000 hiv alikuwa anaitwa mama Tausi

Ila RIP kwako Mabela
 
Mzizi Mkuu wa Bendi nzima ndiyo umeshaondoka hivyo na sina tu uhakika tena kama waliobakia wataisimamisha Msondo kama hawa Walioondoka.
R.I.P mabera. Sema tune ya gitaa lake litapotea ila ukitaka ujue muziki ama melody ya muziki wa msondo ipo katika vidole vya Abdul Ridhiwani Pangamawe huyu alifundishwa gitaa na Kassimu Mbwana Mponda. Na kinanda alifundishwa na Waziri Ally. Kweli msondo itapata pigo ila melody ya kihuni katika gitaaa bado ipo katika vidole vya solo attack Tanzania. Msikilize kwenye Kalunde na ndugu hatuelewani.
 
Back
Top Bottom