TANZIA Mwanamuziki mkongwe, Said Mabera afariki dunia

Mtunzi na mpiga gitaa la solo mahili sana Mabera!!!! Mungu amlaze pema. Amefariki akiwa na umri gani? Tangu Enzi za Nuta Jazz nyimbo kama Nidhamu ya Kazi, Mpenzi Zarina, Nisingekukimbia Mpenzi na vibao vingine vingi Enzi hizo tutamkumbuka sana Said Mabera na wengine waliotangulia mbele za haki.
Pole sana kwa familia na taasisi na bendi ya Msondo Ngoma.
 

RIP SAID MABELA
 
Upumzike kwa Amani Ndugu Yetu
Hakika mlitupa burudani na muziki wa Msondo Ngoma
"...... hapa nilipofika inatosha nisijefuga ugonjwa nikakosa dawa.... Maringo Binti Maringo......
Zilipendwa kitambo sana
Mungu akurehemu!
 
La, Said Mabera, nilimkubali kwa upigaji wake hasa miziki ya Latino. Pumzika Camarade Mabera.
 
R.I.P
 
Nitakwenda na naani msondo ngooma, nitacheza na nani magoma kitakita.
Kalale mahali pema .
Athumani Momba,
Selemani Mbwembwe,
Maina,
TX Moshi William,
Muhidin Maalim Ngurumo na leo
Said Mabera.
Inatia uchungu sana.
 
Malizia na Isiaka Kibene.
Nitakwenda na naani msondo ngooma, nitacheza na nani magoma kitakita.
Kalale mahali pema .
Athumani Momba,
Selemani Mbwembwe,
Maina,
TX Moshi William,
Muhidin Maalim Ngurumo na leo
Said Mabera.
 
Miongoni mwa binadamu mlioletwa duniani kwa kusudi la kutoa huduma.
Hukupenda kunyenyekewa bali mwenyewe ulikuwa myenyekevu.
Ulikuja duniani kwa lengo la kuburudisha waliochoka na walio na msongo wa mawazo, lakini ukajipa wajibu mwingine wa kuonya, kufundisha na kutahadharisha.
Nenda Mabera, nenda baada ya kutekeleza vema ulichojaliwa na Mungu. Wafuate wenzio waliozitendea haki karama zao za burudani;
Gerry Nashon "Dudumizi",
Hemed Manet " Chiriku",
Moshi William "Tx"
Mbaraka Mwinshehe,
Abdalla Gama,
Remmy Ongalla "Dr"
Mohamed Kipande,
Abdalla Mgonahazelu,
Muhidin Ngurumo "Maalimu"
Seleman Mbwembwe,
Athman Momba,
 
Apate raha ya milele apumzike kwa Amani. Poleni sana Familia, pole ya kupoteza
 

Mebera ndiye aliyemleta Hassan Rehan Bitchuka kweye band ya NUTA wakati huo Bitchuka alikuwa bado mdogo sana kiumri na wote wakawa wanamwita "bwana mdogo"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…