Kuna watu wakifariki inabidi ku-celebrate maisha yao kwa urithi wanao acha nyuma. Commandant Josky ni mmoja wao. 1969 alikuwa na Dr. Nico halafu akaingia Continental Orchestra na 1973 rasmi akakaribishwa TP OK JAZZ ya Luambo na Lutumba. Huyu ndio sauti ya OK Jazz kwani ameshiriki kuimba nyimbo nyingi kuliko muimbaji yeyote wa TP OK JAZZ.
Anaimba kwa madaha sana na hupanda na kushuka. Lakini pia ni mtungaji nyimbo wa kiwango cha juu kabisa akiwafuatia Franco na Simaro kwa ubora na wingi wa tungo zake. Ameacha ngoma kama Chacun poir soi, Nostalgie (papa yoyo) na Bimasha ngoma ambazo zilikuwa zinamvuruga mzee mzima Franco akiwa kwa stage. Alikuwa karibu sana na Lutumba Simaro ambaye ndie alimleta TP OK JAZZ. Adios vieux Josky.