Cha ajabu kuna watu watajazana kusema sio korona wakati hakuna aliyesema ni korona.
Kwani wewe umesemaje?
Umenikumbusha hadithi ya std3 au 4 tulisoma zamani: .....kijiji kilivamiwa na maadui, wanakijiji wakaenda kujificha chini ya rundo la majani.
Sasa adui akawa anapita juu ya rundo la majani hayo, raia wa kwanza alipokanyagwa bila adui kujua, raia huyo akalalamika chini ya maficho hayo: 'acha kunikanyaga', hapo hapo adui akasikia sauti, akakita mkuki, jamaa akafa.
Raia wa pili alimposikia mwenzake akilalamika kakanyagwa, naye akasema 'acha kuongea watakusikia', hapo hapo adui akakita mkuki wake, jamaa kwaheri.
Raia wa tatu alivyosikia wenzake wakiongea, yeye akasema 'shauri zenu, mimi siongei', adui akasikia sauti akakita mkuki akaua!......
Ama kusema:.... 'nisingelikuwa ninakuheshimu ningekutukana sana'...
Mifano namna hiyo ni mingi, kwa hiyo wewe ndiye 'kivumishi' unayezusha kwamba kafa kwa korona period
Sent using
Jamii Forums mobile app