Mbona akina Diamond wakijaga hawaanguki, standard ya jukwaa nimeiona ni ya kawaida sana, itakua huyo maskini dogo kaalikwa in a low budget event yenye hadhi yake.
Nawaambia tena, huyo Ashlay huku hafahamiki kama mnavyodhania nyie, hana hadhi ya kufanya Wakenya wawaze kumhujumu. Binafsi, kama nilivyosema awali, nilimkumbuka baada ya nyie kuleta mada fulani alivyopokelewa kijijini kule Turkana ambapo huko ni kawaida kwa msanii yeyote kupokelewa na nyomi, hapo ndio nilikwenda Youtube kutafuta ili nijue nani huyo.
Japo nakiri kuna wimbo wake wa hivi majuzi nilikua naupenda bila hata kujua msanii nani, ule wimbo wa 'Muhudumu', nilikua kila nikiuskia kwenye redio nachangamka japo juzi ndio nimekuja kujua kumbe umeimbwa na huyo dogo, mara ya mwisho kumskliza ilikua ule wimbo wake akiwa bado mtoto, ule wa 'nakwenda kusema kwa mama'.
Lakini kama nilivyosema pia, nyie mna tabia za kuleta bifu zenu za kijinga hadi Kenya, yale yenu ya timu Mondi na Kiba, kuna siku meneja wa Diamond alimzimia mike Kiba hapa hapa Kenya, hivyo roho zenu zilivyo nyeusi mnaona kila mtu anafanana na nyie.