Mwananchi aomba siku ya Ijumaa iwe siku ya Mapumziko

Mwananchi aomba siku ya Ijumaa iwe siku ya Mapumziko

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Katika Mashindano ya Kuhifadhi Qoran kwa Wasichana yanayofanyika kwenye Uwanja wa Mkapa, Mmoja wa Wananchi alipopata nafasi ya kutoa salamu, Amewaomba wanaohusika kuifanya Ijumaa kuwa Siku ya Mapumziko kama ilivyo Jumapili ambapo amedai badala yake Jumamosi iwe siku ya kazi.

Akitetea hoja yake amesema kwamba, Siku ya Ijumaa Maofisi ya umma yanakuwa hayana wafanyakazi kwa vile wengi wao wanakuwa wakijiandaa na Ibada, jambo linaloleta usumbufu kwa Wananchi, ili kuondoa usumbufu huo ni bora siku hiyo ikawekwa kuwa ya mapumziko na Jumamosi ifidie.

Soma Pia: Rais Samia akishiriki tamasha la Mashindano ya Kuhifadhi Quran kwa Wanawake


Binafsi Naunga Mkono hoja yake
 
Wewe na huyo mwenzio wote n wapumbavu wakubwa, kihistoria sku ya ibada ni jmos kabla hata ya ujio wa uislam na utawala wa rumi kubadili kwenda jpl. Halafu dunia inaendeshwa na matajiri na papa ndo huamua nn n nn si mambo ya dini kama mnavyodhania wao ndo wanaweza wakaamua hata leo sku ya mapumzko iwe j5 tu. Kwa taarifa yenu hlo haliwezekan kwa mataifa ombaomba kama letu. Yan badala tuweke hata sk 1 tu ya mapumzko watu wafanye kaz mnataka ziwe 3 hv waafrika n nani ametuloga na hz dini hz. Wazungu wanapga kaz kila sku 24 hrs halafu eti kuna wapumbavu wamelewa tende za bure toka oman wanataka sku za mapumzko ziongezeke wanasahau huo n mfumo wa dunia na watawala ndo wameweka ivo miaka na miaka.
 
101- UONGOZI KATIKA JAMII
Kusanyiko lamfanya muumini kuona tupo wengi sana, hivyo ni mahala pa kutoa ombi kwa kuwa viongozi wa chama tawala , serikali na vilabu vya michezo wapo, asasi za kijamii na nchi nzima inaangalia mubashara.

Nini tumejifunza kupita kusanyiko hili? Ni kuwa viongozi wasio wa kiimani wasiwe wanahudhuria makusanyiko ya aina hii.

Kwa kuwa serikali haina dini ila wananchi wana dini zao mbalimbali, ni vizuri viongozi wa kiserikali wakawa humble hata wakialikwa wawe waungwana kutoonesha makeke ya kimamlaka ya dunia.

Viongozi wa kuserikali wanapohudhuria shughuli kama hizi wawaachie viongozi wa kidini kutamalaki siku hizo muhimi ziwe za kiimani, kimatambiko, kijamii n.k Ili ijulikane wapo hapo kwa imani zao na siyo kwa mamlaka zao ili kuondoa mkanganyiko wa kuonekana serikali ina dini au ina matambiko ya kijadi ya kichifu au wao ndo waongoza harusi, graduation ya vyuo vikuu, kukabidhi kombe kwa klabu ya mtaa maarufu n.k

Shughuli ya kijadi ya Kuomboka ni kubwa inahudhuriwa na wengi, mfalme wa kijamii akiongoza


View: https://m.youtube.com/watch?v=HPvnTOP-eA8
 
Huyu mwananchi akili yake imejaa upumbavu. Pamoja na kwamba sura yake inaonesha amezeeshwa na umaskini ktk umri mdogo, lkn bado anataka kupumzika. Ni mawazo ya kishenzi na kimaskini kabisa.

Amevamia dini ya mwarabu hii, sasa inampeleka puta.
 
Kuna mambo waislam hayako katika imani ila wanapenda yapa kipaumbele.

Kutaka kudeka deka hovyo.
Waislam Wengi wanahuu ugonjwa pamoja na uvivu. Japo Dini imepiga sana vita uvivu.

Quran imelezea ikiadhiniwa Swala ya Ijumaa watu waende kwenye ibada na ikishaisha watawanyike kujitafutia riziki(Mwenye kukumbuka hi Aya atanisaidia)

Ila hapo anatokea mtu anataka ashinde msikitini yaani ifanywe siku nzima ya mapumziko.

Hapo ni sababu inatafutwa kwanini jumamosi na jumapili Tunapumzika..

Kuna mambo inabidi tubebane sio kila jambo kulalamika.
 
Jinsi viongozi na chama tawala wanavyoweza kuwachanganya wananchi. Na kuona kuwa CCM ina Jumuiya nyingi zaidi ya UVCCM, WAZAZI, UWT na zingine sisizo rasmi .....


View: https://m.youtube.com/watch?v=3_XCxxaCWhE

Ni vizuri viongozi kiserikali na chama tawala wakawa wanatambua uwepo wa mambo ya kijamii lakini wasikubali kutwikwa vilemba vingi vya madaraka kwa kuwa utakuwa ni mtihani mkubwa kwao.
 
Back
Top Bottom