Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Wameeleza kuwa wafugaji wanavamia mashamba na nyumba zao, kuwaua, kuwavunja mikono na kuwaibia mifugo, huku wengine wakilazimika kuacha kulima kwa hofu.
Katika mkutano huo, wananchi walilalamika kuwa mtu aliyemuumiza mfugaji kidole alikamatwa na polisi, lakini wale waliowaua ndugu zao bado hawajakamatwa.
Wanawake na wanaume walieleza jinsi usiku wanatembea kwa hofu, mazao yanaharibiwa na watoto wanashindwa kwenda shule kwa usalama.
Wananchi wamemsihi Mbunge aingilie kati ili serikali na sungusungu waendelee kufanya kazi ili kurudisha amani kijijini, kwani hali imefikia hatua ya kutisha na kuwaathiri maisha yao ya kila siku.